Nifanyeje niweze kuangalia Bongo Movies?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,389
38,667
Nina bidii sana ya kununua filamu zinazotengenezwa na wasanii wa hapa nyumbani kiasi kwamba wauzaji wake wanajua kuwa kila ikitoka Movie mpya ni lazima waniletee ninunue. Lakini tatizo langu ni kwamba sijawahi kuangali filamu hizo mpaka mwisho kabla hazijanichefua kuangalia.

Sasa hela ninazotoa kununua zinaniuma sana na pia kuacha kuwa- support wasanii siwezi. Nitumie njia gani niweze kuziangalia hizi filamu mpaka mwisho?
 
Alikuja dogo akaniuzia moja inaitwa "mto wangu" nikabishana naye sana kwamba nanunua tu ili asilale njaa lakini filamu zao hazina viwango. Basi aliimwagia sifa hatari, kwenda kuiweka kwenye deki kuanza tu hata dakika tano hazijapita nikaitolea mbali!!
 
Alafu unawezaje kuangalia muvi ya kibongo mpaka mwisho akati ukiangalia mwanzo tu ushajua inaishiaje
 
Nunua ndimu zikikuchefua unakula ndimu kidogo kisha unaendelea kutizama ,utamaliza tu
uwe unanitumia izo hela mikununulie pilipili kichaa unafuna uku unamalizia bongo bashite zako

Ha ha ha a

Tafuta kundi la majangili walipe wawe wanakutesa na kukulazimisha uangalie mpaka mwisho, mana kwa hiyar yako huto weza,

Tafuta waganga wakupe maelekezo kwamba zinaongeza nguvu za kiume, hapo utaangalia hadi mwisho na hutopata kichefuchefu


Ha ha a dah!
 
Rudi shule za msingi za serekale au penda kukaa vibarazani na akina mama mnasimuliaana utapata mzuka wa kuziangalia
 
Bongo muvi ukiangalia katika tv za kizamani utaona haifai lakini nunua LED TV 32 INCH kitu cha Sanyo mtu unamuona kama mlima, we unakitivii 18inch kama cha saloon alafu upo katika nyumba ya kupanga alafu kodi inakaribia kuisha utaonaje raha ya muvi, kwanza bongo muvi sio muvi za watazamaji wenye njaa, eti unatoa 5000 alafu unajuta siku nzima.
 
kwanza bongo muvi sio muvi za watazamaji wenye njaa, eti unatoa 5000 alafu unajuta siku nzima.
Kwani hizo zingine si naziangalia kwenye "TV Screen" hiyo hiyo ninayotumia kuangalizia Bongo movie? Silalamikii hela ninayotoa bali ubora wa kile ninachonunua!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom