Nifanyeje na huyu jamaa

Nifanyeje na huyu jamaa

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Ni jambo la kiungwana kuomba ushauri kwa wana JF wenzangu kabla sijafanya maamuzi fulani.

Kuna jamaa yangu hapa Mwanza (fundi kompyuta) ambaye nilifahamiana naye kwa mara ya kwanza kupitia nyumba niliyokuwa naishi (tulipanga nyumba moja) baada ya miaka miwili yeye alikuwa wa kwanza kuhama lakini tumeendelea kuwa na mawasiliano ya karibu hadi hivi leo.

Mwezi wa nov. mwaka jana, kompyuta yangu (laptop) ilipata matatizo hivyo nikampigia simu akaniambia niende kwake, baadaye akaniambia tatizo na gharama yake ikawa laki na nusu, nikamwambia kwa muda huo nimetingwa ngoja niache kwanza hili swala baadaye nitashughulikia na kwa kuwa yeye ni fundi atanitafutia mteja aiuze nikaondoka na kompyuta yangu.

Mwezi wa Dec. akanipigia simu, akaniambia kile kifaa kinachosumbua kwenye kompyuta yangu anacho, nikamwambia sina pesa na kwakuwa aliniambia anashida na pesa (alikuwa na msara polisi) nikamwambia kama anataka afanye repair auze then anipe pesa niliyomtajia, akakubali na akachukua kompyuta akafanya hivyo na baada ya muda akaniambia kunamtu anakuja kuilipia pesa kesho yake.

Lakini nikamwambia asimpe kwanza kwani inatakiwa nitoe data zangu hasa research, akaniambia ameweka window nyingine, nikamuuliza kwanini umeweka window upya bila kunitaarifu na tatizo lenyewe kwa vyovyote vile halikutakiwa kuhusisha window? akakosa jibu, nikamwambia basi nitakwenda kuichukua nifanya data recovery akasema sawa, nilipompigia simu kuwa nataka kwenda akaniambia hayupo siku hiyo, kesho yake nikaenda bila kumtaarifu akaniambia kunamtu anaitumia anataka ainunue hivyo atanitafuta baadaye, lakini hakunitafuta.

Nikamwambia siku nyingine naenda kwake akasema anaenda magu atanijurisha akirudi jamaa hakufanya hivyo hadi siku mbili mbele, baadaye nikaenda kwake akaniambia kompyuta anayojamaa magu anaicheki na aliiacha kule jana yake, jsikumuelewa nikamjibu unataka tuanze kupelekana polisi na wakati juzi ulikuwa na msara? Jamaa akacheka akaniambia sio hivyo, baadaye akaniambia jamaa wa magu amepata ajali na pikipiki akiwa anakuja mwanza kavunjika miguu yuko bugando, da! nilicheka sana, kiufupi hadi sasa kompyuta siioni, pesa sizioni, jamaa ninauhakika kwa hii milolongo ameuza kompyuta na pesa amekula, mi nataka nimpeleke polisi.

Waungwana naomba mnisaidie mawazo yenu, hali yenyewe ngumu halafu mtu anataka ale kwa raha zake kwa kweli sikubali!
 
Sasa wewe ulijua huyo mtu ana kesi polisi
probably kamtapeli mtu mwingine
na wewe ukaunga tela?tukusaidiaje?
 
Peleka Polisi zimtoke na huko, mijitu mingine huwa siyo mistaarabu
 
Pole sana huyo jamaa ni tapeli kabisa cha kufanya ni kumpeleka taratibu kwanza kabla ya kwenda polisi! Maana unaweza kwenda polisi na akakuahidi kukulipa kazi ikawa hilehile!

Siku nyingine kabla ujapeleka computer kwa fundi utoe vitu vyako muhimu, maana unawza kumlahumu kumbe hajui umuhimu ya research!

Pole sana!
 
Nenda kwake na simu au tape recorder muhoji huku unamrecord kwa siri,then hapo unakuwa una ushahidi wa kutosha kumpeleka police!bila hivo anaweza kukukana mkuu!
 
Fuata ushauri wa kamanda moshi with no evidence no right to talk about the matter other wise find something to prove beyond reasonable dought
 
Pole sana huyo jamaa ni tapeli kabisa cha kufanya ni kumpeleka taratibu kwanza kabla ya kwenda polisi! Maana unaweza kwenda polisi na akakuahidi kukulipa kazi ikawa hilehile!

Siku nyingine kabla ujapeleka computer kwa fundi utoe vitu vyako muhimu, maana unawza kumlahumu kumbe hajui umuhimu ya research!

Pole sana!

kuna ubovu mwingine hauwezi kukuruhusu kuzitoa data zako muhimu kutoka kwenye computer unless uwe na utaalam zaidi.
 
Nenda kwake na simu au tape recorder muhoji huku unamrecord kwa siri,then hapo unakuwa una ushahidi wa kutosha kumpeleka police!bila hivo anaweza kukukana mkuu!

Kamanda Moshi nashukuru kwa ushauri, mawasiliano yetu kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni kwa massage na zipo kama ishirini hivi, sijafuta hata moja nadhani zitanisaidia!
 
Back
Top Bottom