Nifanyeje kuwaepuka wapiga mizinga

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,977
Reaction score
37,879
Nifanye nini kuwaepuka watu wanao niomba omba hela. Naombeni ushauri wenu pls coz its getting in to worse, hazipiti siku mbili bila kupokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa watu tofauti tofauti wakiniomba hela. Nishaurini plz!
 
si uwaambie huna?

Itakua unagawa gawa hovyo hela...mtu akikuomba tu unampa ndo maana wamekugeuza atm....

Wakituma msg waambie hali mbaya huna kitu

ukishindwa badilisha namba ya simu ila hutatui tatizo kwa kulikimbia....

Dawa ni kuwaamnia huna... Ikishindikana wapige wewe mizinga
 
jibu ... sina..AKILAZIMISHA USIPOKEE HATA SIMU YAKE..SIKU HIZI WATU HAWANA UTAMADUNI WA KULIPA MADENI!
 
Wanyime

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
acha uchoyo...ila utoe kama unacho....ukiona unalalama inamaanisha huna uwezo
 
....Lamba ndimu au limao then uwajibu kuwa huna!
 
Ungeweka wazi ni watu wa aina gani,ni ndugu au ni washkaji tu,alafu ni kiwango gani haswa huwa unaombwa sana,kama ni ndugu fikiria opportunity alizo nazo karibu yake kila akikupigia mshauri kutumia hizo opportunity kupata hela,kama ni mizinga ya watu wa mtaani waambie kweli hela unayo ila kulingana na majukum yako haikutoshi,watakuelewa,mtu hadi akuombe hela hovyo kuna point of weakness unayo na umeionyesha katika utoaji,hakikisha unampa mtu kitu kwa sababu anahitaji,sio kwa sababu unacho.
 
Usiombee ukutwe na shida halafu kila unayemwomba akusaidie anasema haiwezekani, kwa hiyo jitahidi kusaidia pale inapowezekana maana hujui kesho yako itakuwaje.
 
Wape za uso! Lakini pia zitafutie hela zako majukumu ili wakati unawajibu usijisikie vibaya. Mfano anzisha project na uweke strategy ya kusave. Kila ukipata mshahara ama faida ya biashara fungua account ya ujenzi labda na usiiguse. Uiweke huko. Ama kama una site yako weka kiwango cha matofali ama mabati ya kununua monthly. Hapo hata kama una huruma kwishney.
 
Inategemea aisee. Kuna mijitu itakitafuta ikiwa na shida tuu. Afu usiombe wewe uwe na shida na jitu linalokuomba kila siku linasema halina!
Usiombee ukutwe na shida halafu kila unayemwomba akusaidie anasema haiwezekani, kwa hiyo jitahidi kusaidia pale inapowezekana maana hujui kesho yako itakuwaje.
 
Pole, inavoonekana hapo awali ulikuwa nazo na ndio maana hukuona ubaya kuwapa, nadhani sasa zimepungua ndio maana unaoiona hiyo kero.

Jitahidi kuzitafuta tena, hutaiona hiyo kero bali utafurahia kutoa kama zamani.
Blessed is the hand that gives...
 
Pesa haiombwi aisee,,mi msimamo wangu sikupi pesa kwani umefanya kazi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…