Nifanyeje jamani!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifanyeje jamani!!!!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Terimu, Nov 20, 2011.

 1. T

  Terimu Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nina umri wa miaka 30 na mume wangu ana miaka 49, tangu mwaka huu mwezi wa sita amekuwa na tatizo la kutosimamisha uume wake, yaani nashindwa hata kuelewa kwa nini, au ni sababu ya umri? madaktari nisaidieni!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ajaribu kutumia dawa za erectile dysfunction. Ila aende kwanza kwa tabibu.
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Umekosea jukwaa Terimu,
  ilibidi uliweke kwenye jukwaa la JF Doctors!!!

   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Umri si tatizo maana hata wanaume wenye umri mkubwa zaidi ya huo hawana tatizo hilo, labda ana matatizo ya kiafya yanayosababisha hali hiyo. Waoneni wataalam katika mambo kama haya labda wanaweza kumsaidia. Pole sana.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Duh! Poleni sana.
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Waombe MOD's waihamishe hii
  thread jukwaa la JF doctor .. your more
  likely to get anwers over there.. all the best .
   
 7. T

  Terimu Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asanteni sana, tutazidi kuwatembelea madaktari, ingawa tunapata majibu tofauti, hivyo inazidi kutuchanganya! nani anaweza kutushauri the best dr, tunaishi Dsm!
   
 8. T

  Terimu Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Thanx Afrodenzi, nitawaomba waihamishe!
   
 9. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  lol,mtoto bado mbichi kabisa masiki,pole
   
 10. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole sana dada, nahsi ni jinsigani unapata shida, na mumeo nae pia. Muomben mungu huku mkizidi kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu.
   
 11. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  pole sana dada,unaonekana ni mama mwenye busara,mungu atasaidia.
   
 12. T

  Terimu Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Amina, nawashukuru wote kwa faraja zenu!
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pole sana mdada mtegemee Mungu pekee ndo atakuwa jibu peke yake
   
 14. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nimeku2mia PM dadaangu jaribu..
   
 15. T

  Terimu Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Thanx Mtalingolo, nimeiona, nitafanya hivyo na ubarikiwe sana.
   
 16. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Nakupongeza kwa ujasiri wako tu wakutafuta ushauri,big up kwa hilo,kwa umri wako wengi wangekimbilia kuvunja ndoa au kutoka nje ya ndoa!jaribu kuwaona madaktari watakupatia ufumbuzi wa hilo.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Sababu 9 muhimu zinazo sababisha upungufu wa nguvu za kiume
  Zipo sababu nyingi zinazosababisha wanaume kupungua nguvu za kiume katika hizo ni hizi zifuatazo:
  1.ubugiaji wa tumbaku .
  2.uvutaji wa sigara.
  3.utafunaji wa mirungi.
  4.unywaji wa pombe.
  5.kupooza kwa mwili kunakosababishwa na maradhi.
  6.ugonjwa wa kisukari.
  7.kujisaidia kwa njia ya mkono. (Punyeto)
  8.kuwa na mawazo kupita kiasi.
  9.kufanya kazi ngumu.

  TIBA YAKE:
  chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja.

  Chanzo: Mzizimkavu

  [​IMG]


  Au tumia hii Dawa itamsaidia mume wako

  Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}

  Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.
  Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya

  dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo
  wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya

  kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao
  za kufanya mapenzi. MATUMIZI YA ASALI KAMA DAWA YA KUTIBU NGUVU ZA KIUME.

  Pata Asali mbichi ya nyuki, Tangawizi kavu na pilipili Mtama, Asali kipimo nusu kilo,Tangawizi kavu Gramu 50 na pilipili Mtama Gramu 50 Twanga pamoja kisha chekecha upate unga wake changanya na Asali mbichi ya nyuki kula kila siku kijiko kimoja kutwa mara 3 kabla ya kula kitu Asubuhi,Mchana,na usiku. Muhimu hakikisha mpaka umalize Dawa kutumia ndio waweza kukutana na mke wako kimapenzi basi Nguvu zako za kiume zitarudi na utakuwa na nguvu kwenye mechi yako na mke wako. Ukitaka uwe na nguvu zaidi wasiliana na mimi kwa Private message nitaweza kukusaidia zaidi.

  Please give me a Feedback P.h.D. Mzizimkavu

   
 18. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Naomba ufafanuzi wa pilipili mtama,hi ni ipi tena mkuu mzizi?
   
 19. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pole sana dada mungu atawasaidia mtapata suluhisho.
   
 20. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ndio mmeshauri dawa, je jinsi yakumpa uyo mzee iyo dawa hamjamshauri!
   
Loading...