Nifanyeje hapa? Nichukue uamuzi gani?

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,655
Mwaka jana mwezi wa 7 hivi..nilipata seke seke kazini hivyo nikaachishwa kazi ghafla - Huku nyuma nilikua na mwanamke naishi nae na tulikua na mtoto mmoja, Wakati naondoka kazini kodi katika hio nyumbatuliyokua tumepanga ilikua inakaribia kuisha ilikua imebaki kama siku 20 hivi.

Sasa nikaongea na mwenzangu kuhusu suala la kuhama pale kwenye nyumba sababu tulikua hatuna uwezo tena wa kulipia ile nyumba.Tukakubaliana kwamba tutahama kabla ya siku zilizobaki kuisha maisha yakaendelea zile siku zikaendelea kukatika mpaka nikafanikiwa kupata chumba kimoja nimalipia miezi 3. Niliporudi nyumbani nikamweleza mwenzangu kuwa nimeshapata chumba singo hivyo tutahamia humo, Mwenzangu akanijibu sawa.

Asubuhi ya hio siku ilikua Jumamosi nikaamka mapema nikamuachia mwenzangu Hela kiasi ili awalipe watu niliokua nimewapa kazi ya kubeba vile vitu vya ndani ilipofika mida ya saa nne asubuhi nikawatuma wabebaji mizigo waende wakapakie vile vitu ili wavihamishie kwenye chumba ambacho tungehamia,Wale wabebaji wakaenda na kurudi mapema nikawauliza mbona mmemaliza hivyo mapema wakati vile vile havikua vya kumaliza mapema Hivyo? Wakasema wamelikuta godoro na begi la nguo na ndio ambavyo wamevihamisha.

Nikampigia mwenzangu simu nijue ni nini kimetokea simu yake ikawa haipatikani, Ilipofika jioni nikarudi zangu nikaelekea kwenye kile chumba nilichokua nimekichukua ila sikumkuta mwenzangu nilipoingia ndani nakuta begi godoro na ndoo mbili.Vitu vingine sikuvikuta.

baadae nikapokea meseji kwenye simu yangu, Ilisema" Samahani kwa kuchukua vitu vyako. Kumbe mwenzangu alichukua vitu vingine akaenda kupanga chumba mahali pengine akaniachia hili godoro na ndoo mbili. Nikasema isiwe tabu nitapambana hivo hivo kwa vile anatumia hivyo vitu na mwanangu haina tatizo.

Sasa imefika karibu miezi sita hatuna mawasiliano mazuri na mzazi mwenzangu kwa sababu ya hili tukio. Mimi sina tatizo na yeye ila kila siku ananisumbua kwenye anataka hela ya matumizi - wakati wakati mimi nimeshaanza maisha mengine na nimeshamsamehe kwa kile kitendo.

Nilimwambia arudishe mtoto kwa Baba yake hataki anasema mpaka miaka 18.

Naombeni mawazo yenu wajuzi wa haya masuala..nifanyeje nimchukue mtoto wangu nichukue hatua zipi?
 
sidhani kama Hiyo ndo sababu

kuna mengine umeyaficha.

weka utaratibu wa namba ya kuhudumia mwanao,kwa maandishi.
 
Mkuu jf umejiunga 2011, kwa vyovyote vile umri wako utakuwa sio haba. Ushahidi mna mtoto wa miaka 7, na mmeachana na "mzazi mwenzako" miezi 6 tuu iliyopita.

Kuna madukuduku mengi sana ninajiuliza kichwani mwangu:

1. Ni kwa nini mmeco-habit kwa miaka mingi hivyo vila kuoana ama taratibu za kurasimishana japo kwe level ya familia zenu tuu.

2. Imekuwaje mmekaa miaka 6/7 bila mwanenu kupata mwenzake, kuna shida kwako ama kwake?

3. Kwa nini alipokimbia hujafanya hata juhudi za kumtafuta ama kupambania penzi lako!

Kiufupi inawezekana shida kubwa iko kwako, hebu ongezea nyama kwenye andiko lako uweze kupata ushauri wa maana mkuu wangu.

Cc: matindek
 
Kutokuramisha iwe ndoa ilitokana na sababu nyingine nyingi huko nyuma mpaka nikasita kufanya hivyo. hatukuacha kufunga ndoa tu kulikua na sababu ambazo zilinifanya nisite kufunga ndoa.
 
Kuleta maelezo pungufu au kuficha baadhi ya mambo kunatupa wakati mgumu wa sisi wasomaji kutoa ushauri,maana tunajikuta tunajiuliza maswali mengi bila majibu.

Hali hii inafanya tusiweze kukupa ushauri sahihi.funguka kila kitu asee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mahali nimeficha jambo yote yako wazi mkuu.
 
Mkuu jf umejiunga 2011, kwa vyovyote vile umri wako utakuwa sio haba. Ushahidi mna mtoto wa miaka 7, na mmeachana na "mzazi mwenzako" miezi 6 tuu iliyopita.

Kuna madukuduku mengi sana ninajiuliza kichwani mwangu:

1. Ni kwa nini mmeco-habit kwa miaka mingi hivyo vila kuoana ama taratibu za kurasimishana japo kwe level ya familia zenu tuu.

2. Imekuwaje mmekaa miaka 6/7 bila mwanenu kupata mwenzake, kuna shida kwako ama kwake?

3. Kwa nini alipokimbia hujafanya hata juhudi za kumtafuta ama kupambania penzi lako!

Kiufupi inawezekana shida kubwa iko kwako, hebu ongezea nyama kwenye andiko lako uweze kupata ushauri wa maana mkuu wangu.

Cc: matindek
Inaonekana kama ni piece of information tumashindwa kushauri vyema.
 
Back
Top Bottom