Wyatt Mathewson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 10,772
- 25,413
This is confusingHabari wakuu
Naimani wote wazima Mungu anatupigania
Iko hivi Nimeletwa mkoani kikazi baada ya kufika nilipokelewa na workmate wenzangu ofisi na kazi zikaendelea.
Sasa kuna Pisi moja ya kwenda sana nimeikuta hapa tunafanya nayo kazi lakini huwa sio muongeaji kabsa ndio alivyo lakini toka nimefika hapa huyu dada ni mchapakazi sana muda mwingi yuko bize hapa ofisini lakini ni kwa muda mfupi focus yake ya kufanya kazi ilipungua sana.
Kuna kitu nilianza kujiuliza shida nini coz tunafanya kazi ofisi moja lakini nilikuwa kila wakati namfumania akiwa ananiangalia sana, ikaenda hii hali mpaka ikafika stage wafanyakazi wengine wakaligundua hilo mpaka baadhi wakikaa na mimi tukipiga stori wanaliongelea hilo jambo.
Kuna siku nikasema ngoja nijitoe akili nikamfuata kwenye meza yake nikaanza kupiga nae stori, kiukweli alifurahi sana kipindi namuacha pale nikamuomba namba akakubali akanipa
Basi tukaanza kuwasilia mdogo mdogo siku zinakwenda kuna siku nikamuomba nimtoe dinner kweli alikubali bila hata kuguna kweli na alikuja fresh lakini sasa pale ofisini wakaanza kunishangaa kuwa imekuaje kwa muda mfupi yule dada kanizoea sio mtu wa mambo mengi na huwa yuko streight na hapendagi mazoea na watu japokuwa ni mpole na yupo loyalty.
Basi mambo yakaendelea kila siku mwanamke akawa anazidi kuwa happy akiniona tu nimefika ofisi na hata nikichelewa akawa anapiga simu na kuuliza niko wapi. Basi maisha yakaenda japo watu wakawa wanashangaa sana imekuaje kwani.
Basi kuna siku tulikutana nikamtongoza japo alikuwa anaonesha sio mwepesi fulani lakini aliniambia ana changamoto tu fulani hivi ataniambia, nikakaza uzi na akakubali fresh hapo hapo na kesho yake tulivotoka ofisini akahitaji twende wote ninapoishi nikamchukua tukaenda na alijikuta tunalala mpaka kesho yake kwa kuwa siku inayofuata ilikuwa weekend.
Sasa ofisini wakawa wanazidi kushangaa imekuaje sasa bhana nikaja kupata majibu kamili kumbe huyo dada wafanyakazi wapale ofisini karibia wote wa kiume walikuwa wanamfukuzia lakini aliwachomolea wote ndio maana walikuwa wanashangaa kwangu imekuaje, bhasi maisha yakaenda .
Basi sasa kuna siku akawa hayuko sawa nikamuuliza nini shida ndio akaanza kunielezea ile changamoto kuwa ni kweli ana mwanaume lakini hawajaoana kabisa na hawajazaa na hadi kwao wanamjua na alishapeleka mpaka posa na kila kitu lakini kiukweli hawako sawa kabsa na anasema hana furaha kabisa na maisha anayoishi na jamaa na ilifikia stage kila mtu anakaa kwake mpaka now
Duuh nikamtuliza na kumuweka sawa na kumwambia asijali kila kitu kitakuwa sawa.
Sasa ninachokihitaji wakuu huyu mwanamke mimi nataka kumchukua mazima na ikiwezekana kumuoa kabisa
Sasa sielewe nifanye nini akili imestuck lakini yote kwa yote ametokea kuniamini sana huyu mwanamke
Kwahiyo "wamkuambia" wanaume wa ofisini wamemtongoza sana "kawakatalia"......and then ukaamini kabisa?
Unasema walikua wananiangalia na kunishangaa ofisini,na ukaamini walikua wanakushangaa umepata dem mkali?
This is really confusing to me