Nifanye nini ili nimpate mwanangu?

Kitombise

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
8,518
25,430
Habari zenu.

Baada ya kumaliza form four nilibahatika kupata mtoto wa kiume na student mate mwenzangu. Baada ya kujifungua ndo mkataba wa baba yake kufanya kazi hapa nchini ukawa umeisha hivyo wakarudi kwao Olso Norway. Tuliendelea kuwasiliana na hata akawa ananitumia picha za maendeleo ya mtoto jinsi anavyokuwa na kuniahidi atarudi siku za mbeleni ili tujenge familia yetu.

Basi ikapita zaidi ya miaka kadhaa huku bado tukiwa tunawasiliana na tayari hapo mimi nikawa nimeshapata mtoto mwingine na niliyezaa na mwanamke mwingine tena.

Basi siku moja kuna msela wangu akaniambia amemuona Dar yule demu wa kizungu niliyezaa naye na amemfwatilia na amegundua anapoishi. Kwakuwa mimi niko huku Kaskazini basi nikaamua kumfungia safari hadi anapoishi na kufanikiwa kukutana naye na nkamuuliza kwanini amekuja bila kunitaarifu?

Akaniambia kwa sasa ameolewa hivyo asingeweza kunifahamisha.

Ok, nkamwambia kuolewa siyo tatizo ila kwa sasa namtaka mwanangu. Akasema "atanipatia soon". Ila nashangaa sasa kunipiga chenga hataki hataki mwanangu na kuona kuwa naendelea kumsumbua kumsumbua kaamua kumsafirisha mwanangu kwenda huko kwao. Baada ya kumuuliza kwanini hutaki kunipa mwanangu na umemsafirisha ili nisimpate basi ndo kaanza kunijibu shit na kusema kuwa hatakaa anipe mwanangu kamwe.

Sasa sijui nitumie njia gani ili nimpate mwanangu japo natambua kuwa sikuweza kumuhudumia mwanangu kwa chochote kutokaa na umbali uliokuwepo ila NAMTAKA MWANANGU, NA SIKO TAYARI KUONA MWANANGU ANALELEWA NA MWANAUME MWINGINE ZAIDI YANGU MIMI BABA YAKE. Mwanangu sasa hivi ana miaka 4.

Sorry mtanisamehe kwa kuandika hovyo coz niko na ghadhabu sana ndio maana nimeshindwa kuandika kwa mpangilio unaotakiwa.

Nahitaji msaada nitumie njia gani ili niweze kumpata mwanangu?

Nawasilisha......
 
Watu wengine bana miaka 0-4 mbona kalelewa bila wewe
Je ulishawahi toa matunzo yoyote ktk kipindi hiko??
Ahhh basi jibu nshaliona
Sasa hujawahi toa hata kumi gadhabu ya nini,basi japo ungekomaa ukadumisha mawasiliano mana malezi sio pesa tu
Ilhali huna mchango wowote muache mama ake alee tu sanasana mkubaliane uwe unamuona mwanao baaas
 
Kama yuko bongo nenda ustawi wa jamii japo upewe muda wa kuwa na mtoto likizo....cha msingi asije kuwa anampa sumu kwamba wewe ni baba mbaya na wewe usifanye hv.... mkubaliane kwamba mtoto asilishwe maneno...
 
Sasa ndo huyo kashamkimbiza huko kwao..
Unafikiri mkuu hapa ntumie njia gani ili niweze kumpata?
 
Mtoto atamtafuta baba wewe kama baba tafuta pesa ili mwanao aje aone kile kilichofanya muwe mbali nae.
 
Kama yuko bongo nenda ustawi wa jamii japo upewe muda wa kuwa na mtoto likizo....cha msingi asije kuwa anampa sumu kwamba wewe ni baba mbaya na wewe usifanye hv.... mkubaliane kwamba mtoto asilishwe maneno...
Na ndo hichi sasa nnachokihofia. Ila ushauri wako nitaufanyia kazi
 
Mtoto atamtafuta baba wewe kama baba tafuta pesa ili mwanao aje aone kile kilichofanya muwe mbali nae.
Mimi sana sana ninachohitaji ni kuwa na mwanangu na kumlea katka mazingira nnayoishi mimi na siyo alelewe huko abroad
 
Kuwa na mtoto ni zaidi ya kumwaga shahawa!!! Wewe unmpa mwanamke mimba hutunzi mtoto miaka minne then unasema una mtoto!!!!

Duc In Altum.
Ningewezaje kumuhudumia wakat yuko mbali nami?
Sasa ndo mana namuhitaji ili niweze kumuhudumia mwenyewe
 
Kaeni chini mjadiliane mjue cha kufanya kwakweli hata mimi mtoto wangu simpeleki kwababa yake.. No Way nimemsafirishia kaskazini huko, though huyu mwana mwenyewe anakiherehere na babake anaweza kutuwekea mgomo kuanzia kwenda shule mpaka kula ni kulia tuu anamtaka babayake, hahaha na akishaongea naye anaridhika anasahau mpaka huo wazimu wa kwao umrudie tena.

Sisi tumekubaliana aishi na mimi mpaka ajitambue kisha ataamua pa kwenda kwakweli, sijawahi kumzuia mtoto wangu kuwasiliana na babake napenda wawe na ukaribu japo walionana mara ya mwisho dogo akiwa na miezi 9 sasa ana miaka 5 kasoro..

Na kutokana na mazingira nahisi wataonana akiwa na 10 years or more
 
Kama vile Mahesabu hayaji, chuo ulimaliza 2011, ila ulivomaliza form four ukawa na mtoto, na sahivi ana miaka minne......
Ulisoma chuo kwanza ndo ukarudi o'level?

Screenshot_2016-05-16-16-12-54.png
 
Kaeni chini mjadiliane mjue cha kufanya kwakweli hata mimi mtoto wangu simpeleki kwababa yake.. No Way nimemsafirishia kaskazini huko, though huyu mwana mwenyewe anakiherehere na babake anaweza kutuwekea mgomo kuanzia kwenda shule mpaka kula ni kulia tuu anamtaka babayake, hahaha na akishaongea naye anaridhika anasahau mpaka huo wazimu wa kwao umrudie tena.

Sisi tumekubaliana aishi na mimi mpaka ajitambue kisha ataamua pa kwenda kwakweli, sijawahi kumzuia mtoto wangu kuwasiliana na babake napenda wawe na ukaribu japo walionana mara ya mwisho dogo akiwa na miezi 9 sasa ana miaka 5 kasoro..

Na kutokana na mazingira nahisi wataonana akiwa na 10 years or more
Huo utaratibu mliojiwekea ni mzuri sasa huyu wa kwangu hataki kabosa niwe na mtoto wangu karibu
 
Ningewezaje kumuhudumia wakat yuko mbali nami?
Sasa ndo mana namuhitaji ili niweze kumuhudumia mwenyewe
Wewe si umesema mlikua mnawasiliana? Sasa ulishindwa nini kutuma matumizi? Miaka minne!!!! No matumizi from no where eti namtaka mtoto wangu seriously? Hata yeye hataki alelewe Na mwanamke mwingine sawa.
 
Back
Top Bottom