Nifanye nini hapa jamani ushauri wenu

Oldaganje

Member
Apr 9, 2014
33
0
Nilizaa mtoto na mwanamke (miaka 10)iliyopita,kwa kipindi chote hicho kila mtu alikua na maisha yake na hatukua na mawasiliano mpaka mwaka huu nilipopata mawasiliano nakufanikiwa kumkomboa mwanangu ambaye yupo kwa wazazi wangu na aonasoma darasa 3.Yeye alikua anaishi na mwanaume ambaye amezaanae watoto 2(miaka 7kwa 3) bila ndoa wala kutolewa mali na mimi nilishi na mwanamke tukazaa watoto 2(miaka5kwa1.5)bila ndoa wala mahari tumetengana kwa sasa.Yeye katelekeza watoto kwa mumewe kakimbilia kwangu na mimi nikampokea kwani mimi nakaapekeyangu kwani mkewangu yupo kwao na wanangu 2,Sasa napokea vitisho vya kurogwa na hatakuvamiwa na kuliwa kutoka kwa mumewe.Naomba ushauri wenu kwani anasema bora anywe sumu na si kurudi kwa yule mwanaume je nifanyeje hapo wana mmu.
 
utafiti

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
12,797

Teh teh hapo ndio hatari zaidi
 
Sweet16

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
3,579
2,000
hhaahaaahahaaaaaaaaaaaaaa haajaahaajajahahajahajahajajaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
missa

JF-Expert Member
May 24, 2012
363
0
Kwan we ulipompokea una lengo gani nae na hali unajua tayari ni mke wa MTU???

Na amekimbilia kwako nawe ukampokea kwani we ni mjumbe wa nyumba kumi??au mzazi wake?

Kama ulizaa nae na hukumuoa badala yake ukagomboa mtoto kwa nini kama na yeye anakuhusu usimgomboe awe mkeo??

Na we we mkeo kaenda kwao na watoto kwa sbb gani?

Inaonesha we we na huyo mwanamke mlipanga njama tu ya we we kufukuza mkeo na yeye kumtoroka mumewe kwa visingizio vya uongo mana hata huyo mwanamke anajua una mke na watoto kwa nini akimbilie kwako wakati mkeo hayupo???kwani kwenye ndoa watu huwa hawagombani na wake zao wakaenda kwao kwa muda na baadae hasira zikiisha wakarudi??

Halafu unasema walioana bila mahari na we we ulioa bila mahari,mbona kauli yako kama inataka kulazimisha uhalali wa we we kumpokea huyo mke wa MTU wakati nawe ni mume wa MTU!!

kwani we hujui kukaa na mwanamke au mwanaume kwa muda Fulani ndani ya nyumba moja na watu wakajua,hata kama hamkutoleana mahari au kufunga ndoa kisheria mnakuwa mume na mke hujui hilo???

Nahitimisha kwa kusema huyo ni make wa MTU na we we ni mume wa MTU,hivyo hakuna cha kunywa sumu wala nini rudisha mke wa mwenzio,usione vyang'ara vimegharamiwa!!!

kama ulikuwa unampenda toka mwanzo ungemchukua enzi hizo ulipomzalisha,sio mpaka wenzio wampendezeshe ndo ujifanye kurudisha majeshi,shauri zako UTALIWA KWELI watu wana uchungu na Mali Zao!!!
 
BRO LEE

JF-Expert Member
Dec 25, 2011
767
500
Mwambie mke wa mtu arudi kwa mumewe au usubiri kuliwa tu, we ni mwizi km wezi wengine yy amkimbie mumewe atelekeze watoto aje kwako we unachukulia poa tu!!!

We patana na mkeo mlee watoto wenu, vinginevyo km unataka kuishi nae hakikisha anamalilizana na mumewe, vya kunyonga vina madhara ndugu.
 
jichopevu

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
404
250
Nashukuru kwa ushauliwako missa.Sasa nitumia njia gani kumshawishi ili arudi kwani namimi simuhitaji.
Ni kweli humuhihitaji na hujui ufanyaje? Kwa nini ulimpokea sasa na kuishi nae? Hebu tumalizie kutuelezea hayo yaliyopo nyuma ya pazia maana inaonekana hii stori haijakamilika
 
Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
14,683
2,000
Dah watu wanachukuliaga kuzaa watoto kama ni fasheni au?

Hivi mnakuwaga na uchungu na hao watoto?

Is there a point in time munatangulizaga mahitaji ya watoto kabla ya kwenu?

unaeleza ukiwa relaxed kabisa eti katelekeza watoto na mimi nikampokea.

So sad.
 
Baby is Mad

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
279
0
Kwan we ulipompokea una lengo gani nae na hali unajua tayari ni mke wa MTU???

Na amekimbilia kwako nawe ukampokea kwani we ni mjumbe wa nyumba kumi??au mzazi wake?

Kama ulizaa nae na hukumuoa badala yake ukagomboa mtoto kwa nini kama na yeye anakuhusu usimgomboe awe mkeo??

Na we we mkeo kaenda kwao na watoto kwa sbb gani?

Inaonesha we we na huyo mwanamke mlipanga njama tu ya we we kufukuza mkeo na yeye kumtoroka mumewe kwa visingizio vya uongo mana hata huyo mwanamke anajua una mke na watoto kwa nini akimbilie kwako wakati mkeo hayupo???kwani kwenye ndoa watu huwa hawagombani na wake zao wakaenda kwao kwa muda na baadae hasira zikiisha wakarudi??

Halafu unasema walioana bila mahari na we we ulioa bila mahari,mbona kauli yako kama inataka kulazimisha uhalali wa we we kumpokea huyo mke wa MTU wakati nawe ni mume wa MTU!!

kwani we hujui kukaa na mwanamke au mwanaume kwa muda Fulani ndani ya nyumba moja na watu wakajua,hata kama hamkutoleana mahari au kufunga ndoa kisheria mnakuwa mume na mke hujui hilo???

Nahitimisha kwa kusema huyo ni make wa MTU na we we ni mume wa MTU,hivyo hakuna cha kunywa sumu wala nini rudisha mke wa mwenzio,usione vyang'ara vimegharamiwa!!!

kama ulikuwa unampenda toka mwanzo ungemchukua enzi hizo ulipomzalisha,sio mpaka wenzio wampendezeshe ndo ujifanye kurudisha majeshi,shauri zako UTALIWA KWELI watu wana uchungu na Mali Zao!!!
Sure,wanaume wote wenye akili za kumimina na kupooza wajifunze hapa.Wakiishia kupata wanawake magarasa wanarudi nyuma kuharibu nyumba za wengine
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom