Nifanye nini biashara yangu ikue?

Mkuu, siwezi kukupa breakdown kwa sababu biashara niliyo na uzoefu nayo inahitaji mtaji wa zaidi ya hio 500k. Ila nimewahi kufanya biashara ya genge miaka ya nyuma nilikua nachukua mazaga soko la ilala nauzia mjimwema. Sikumbuki vyema gharama za kipindi hicho, ila nakumbuka nilikua nikiamka na 200k nikaingia ilala narudi na nyanya karoti, nazi, ndizi nk vya kutosha na faida napata. Ni zaidi ya miaka 8 sasa hivyo tunaweza sema 200k ya kindi hicho kwa sasa ni 300k.

Amini kiwa 500k ni nyingi mkuu. Mfikirie naenunua samaki wabichi baharini anawakaanga na kuwauza 500k haitoshi? Fikiria muuza supu ya pweza, fikiria muuza vinywaji baridi stendi
 
Wewe nasbr unipe mkeka wa biashara
Mkuu mkeka hutaupata hivyo unavyotaka. Mfano mtu unataka kuuza mayai ya kuchemaha kitaa, unataka kuniambia 500k haitoshi? Sasa mimi sifanyi hio hivyo sina Hio breakdown. Ila ukiwa serious ni kumtafuta tu anayefanya anakupa maelekezo na hio 500k inatosha. Unahitaji mayai trei moja ni 14,000/- ukichukua trei 20 ni 280k unabaki na 220k weka 120k ya dharura hio 100k haitoshi kupata sufuria, jiko la mkaa, mkaa, chumvi na maji?
 
Sasa milioni inatosha nini jamani mtaji inatakiwa uanzie mil 10
BIASHARA NI VILE MTU ANATAKA KUJIWEKA.


Ukiwa katika low level ya kujitafuta pesa yoyote ni mtaji.



Hii 500k inatosha sana

Atafute watu wanauza grade A mitumba kwa jumla hasa ngua za kike au mashati ya kiume kumbuka WANAUME tunanuniaga sana mashati au t-shirt kuliko suruali na nguo zingine, mtu anaweza kuwa na jeans Moja mwaka mzima lakini t-shirt tofauti au shirt ila ni ngumu kumkuta mwanaume kwa wiki kabadili suruali zaidi ya 3 times isipokuwa shirt au tshirt. So anaweza cheki hizo business.

Anaweza chukua kwa bei ya jumla grade nzuri shirt zisizovuka 5000 kwa jumla kama anaweza chukua kuanzia 30 shirt pesa inayobaki atunze anaweza Anza na 90000 mpaka 150000, kisha pesa inayobaki atunze sio ya kula sababu anajitafuta lengo aiongezee.


Akifanikiwa kufikisha what 2m, anaweza tafuta frame sokoni au eneo changamfu lenye wadada wengi auze urembo na mapambo ya kike kwa 1m, na alipe 150k miezi 3 ,frame ,achinge kabati ndogo na frame 600k inatosha then 250k inayobaki atunze na kuilinda kwa dhati.


Hii ni kama haitegemei hiyo busness.



NB. Azingatie kuwa makini na wadada kwenye hii bishara ni rahisi kufiriska hasa ukiwa mwanaume unaendekeza chini, bishara ya urembo iache ufanye kuliko kwanza ungana na prof mipango



Faida ni kubwa kama atatembeza kwa miguu au bike, town kwa siku hakosi faida ya 10k-25k kwa shati 5 kama atauza kwa buku 7 faida 2000 kama atauza buku 10 faida 5000.
 
We jamaa, umeongea sana point..alafu hapo mwisho umemalizaje, hahah
 
Kaka, naomba connections za mashati ya mtumba mazuri niuze nipo singida.
 
Wewe pia ni mfanya biashara wa mitandaoni yanai ni motivation speaker mkuu..
Nilisubr unipe.mchanganuo tu.
Biashara sio hvo mnavofikili mambo sio simple ...
 
Wewe pia ni mfanya biashara wa mitandaoni yanai ni motivation speaker mkuu..
Nilisubr unipe.mchanganuo tu.
Biashara sio hvo mnavofikili mambo sio simple ...
Hapana kaka, sijawahi kuwa na sitakua motivational speaker. Mm naendesha biashara real mwaka wa 4 sasa. Najua ninachokisema mkuu. Najua seasons, najua kodi zinalipwaje, najua kudhulumiwa na najua kuyumba na kuimarika tena.
 
Hapana kaka, sijawahi kuwa na sitakua motivational speaker. Mm naendesha biashara real mwaka wa 4 sasa. Najua ninachokisema mkuu. Najua seasons, najua kodi zinalipwaje, najua kudhulumiwa na najua kuyumba na kuimarika tena.
Basi hapo umeniacha mbali mi nina mwaka wa pili huu..
Ila mambo nayoona na nikija huku jf kuangalia nyzi za biashara huwa nachoka sana aisee
 
Wewe pia ni mfanya biashara wa mitandaoni yanai ni motivation speaker mkuu..
Nilisubr unipe.mchanganuo tu.
Biashara sio hvo mnavofikili mambo sio simple ...
Unajua mkuu wewe unachanganya mambo ndio maana hunielewi. Kuna tofauti kati ya mtu anayefanya biashara ili apate miambili ya kula leo na anayefanya ili aidhi kidon. Ninachokisema mimi, hio 500 ni nyingi sana hio, sasa ninaposema nyingi wewe unaanza kuwaza afanye biashara ya 500k apate faida anunue gari, ajenge aishi vizuri, hapana. Ukienda uswahilini kuna akina mama wanachoma mandazi, chapati au vitumbua. Mtaji wao hata 100k haufiki. Anaamka asubuhi achoma maandazi, kufika saa5 yameisha. Anachukua faida ananunua unga na fungu la samaki mchana umepita, jioni wali maharage, kesho tena. Hio ni biashara, vipi huyo wa 500k?

Sheria ya biashara ni moja tu, pamoja na kuwa na akili, uendeshaji sahihi nk, ila pia ili upate faida kubwa lazima u wekeze zaidi, hilo halikwepeki. Ukiuza pipi utawekeza kidogo na faida itakua ndogo, ukiuza magari utawekeza zaidi na faida itakua kubwa.

Narudia tena 500k ni hela kubwa sana na biashara za huo mtaji zipo nyingi. Amini kwamba 500k ni dream mtaji wa watu wengi sana, kuna watu wanaitafuta hata nusu tu ya hio ili waamze safari zao. Narudia usichanganye kupata faida kubwa, kubadili maisha na huo mtaji mdogo, havitawezekana kirahisi
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Acha kupotosha watu mkuu
Hapo andaa pesa za kutosha gari kuivuta mpaka hapa toka dubai unaujua ushuru wa TRA kwa kila gari unataka ufungue showroom yenye gari 2? Yard inabidi iwe na gari kuanzia 100 sasa una kamtaji kako ka laki 5 unataka ufungue Yard hio si pesa ya kufungua Genge la nyanya na viazi mviringo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…