Nifahamisheni viwanda hivi viko wapi?


mungu akubariki na wewe kwa kuyaona ambayo wengi wameshindwa kuyaona. watu wanasema hawapigi kura kwa chama au mtu asiotoa chochote,ubarikiwe sana mkuu.
 
kibaya kuliko yote ni kwamba Tanzania imekua soko la kununua vijibidhaa vidogovidogo kutoka nje vingine vilikuwa vinatengenezwa hapahapa na vingine tungeweza kutengeneza.tulichotakiwa kununua toka nje ni mitambo ambayo hatuna uwezo wa kutengeneza lakini sio viatu,nguo,viberiti ,toys n,k
 
Najisikia kulia ungekuta hata tatizo la ajira hakuna ,r,i.p.tanelec,kiko meerschaum,teco,
 

Ni kweli kabisa mkuu
 
Mkuu umesahau kiwanda cha kuanganisha magari ya nyumbu!!
 
kiwanda cha PHILIPS,Tanzania FOOD,kiwanda cha KIKO, NMC

Kiwanda cha ALPHI kilichotengeneza miswaki na dawa za bonamed sasa hivi ni kanisa kuuubwa!! Tunajisalia huko kwa raha zetu kiwanda cha pareto, majembe (arusha) vyote vimeishia kwenye matumbo ya ma bwana wakubwa wa ccm.
 
Ndugu zanguni tunahitaji mapinduzi ya kifikra. Tunajua mbaya wetu katika haya mambo..CCM..! Hiki chama kimetuongoza kwa kipindi cha miaka hamsini, matokeo yake ni hayo. Mimi sishabikii chama chochote cha siasa ila kwa CCM ambayo ndiyo imetufikisha hapa, sina budi ila kuichukia sana. Haionyeshi kukerwa wala kuwa na mbinu mbadala kukabiliana na hali hii. Na mbaya zaidi imewapa vijana elimu ya ajabu ambayo haiwaruhusu kuwaza namna ya kuiondoa madarakani kwa KURA. AJABU KABISA!!
 
waheshimiwa nakumbuka nikiwa mdogo miaka ya 80 hadi 90 kuna kiwanda cha kusindika ngozi, mashirika kama ya usafirishaji, kauma ,kauru, kaudo na mengine mengi kam sukita,n.k
 
Halo, inasikitisha sana, kila nikipita pale General tyre roho inauma sana nikisogea mbele nakutana na Fibre Board, nakumbuka ABB Tanelec, TEMDO, NMC (unga ltd),TFA,ACU,TPRI na vingine. Ndugu na jamaa zetu wengi zamani walikuwa wanafanya kazi humo, ajira zilikuwepo. Wakati tunaenda shule asubuhi tunaona mabasi makubwa yakikusanya wafanyakazi vituoni. Natamani enzi zile zijirudie bt haiwezekani tena. Loh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…