Ndugu zangu wana JF.
Haja yangu na kiu yangu ilikuwa kuoa mwanamke wa Kichaga kutokana na sifa yao ya kutokaa tu Nyumbani na badala yake kutafuta pesa kwa biashara halali.
Mchaga mmoja binti mzuri alinitaka nami nikamkubali. Kazi yangu ni ya kawaida sana ingawa inaweza kummudu mtoto wa Fisadi yoyote Nchini na kumsahaulisha kwao.
Dada huyu alilazimisha sana tufunge ndoa haraka na mimi nikachelewa kukubaliana naye nikimuomba tuyape muda mapenzi yetu. Nimelala kwake mara mbili ingawa si kwa kuvunja amri ya sita kwa sababu tulikuwa hatujapima,tukapotezana kitambo.
Ulipopinduka Mwaka huu nikaona nimtafute ili sasa nifunge naye Ndoa kwani nimesema Mwaka huu usipite bila kufunga ndoa. Kabla sijamtamkia hilo kaniomba Pesa. Nikamjaribu kwa kumuambia kuwa sina labda mwisho wa mwezi.
Kanijibu kuwa kwake yeye mapenzi ni Pesa,bila Pesa nisiwaze kuwa nitakuwanaye maishani. Nikamuuliza ni kweli ndivyo mlivyo wachaga. Akasema hiyo ni asili yao na hawataacha kuwa hivyo. Sasa nimeduwaa ndugu zangu.
Nishaurini wababe wangu wa michambuo ya maisha niendelee kutafuta mchaga ama niachane nao na nijaribu kabila jingine. Mimi ni Mmakonde pure wa mahuta Umri chini ya 40.
Nisaidieni ndugu zangu.