niende tra au nifanyaje wakuu?

niende tra au nifanyaje wakuu?

Status
Not open for further replies.
Cjui ulipitaje katika huo mchujo wa tra kama akili yenyew ndo hii...
 
thanx bro..nimejikuta naipenda sana kazi ya sales ingawa haikuwahi kuwa ndoto yangu

Unafanya Sales za bidhaa gani?? Kama ni Heavy Duty Machines na upo Avic Shantui, hapo nakushauri usiondoke. Serikalini ni pagumu sana kwa kipindi hiki cha Uncle Magu .... Hawa wachina ni wachina wazungu,wanajali sana maisha ya mtanzania.... Lakini kama upo company nyingine.... Dadavua mwenyewe....
 
TRA wana SACCOS Kubwa Sana Net Assets zake ni 65billion Baada ya Kuchukua barua ya Appointment tuu ya Kazi Una uwezo wa Kupata Mkopo wenye Riba Nafuu Sana

Yaani Kila Mtu Anayetoa Ushauri amejikita katika Wizi/rushwa ,Fananisheni na Taasisi za Wachina

Ukifanya Kazi kwa Uaminifu Utadumu kwenye Ajira.
 
naweza kusema kuwa miongoni mwa watu waliochaguliwa tra kwa nafasi ya custom officer ii is like dreams come true kwa sababu toka nikiwa mdogo mawazo yangu yalikua ni kufanya kazi sehemu tano tu ambazo ni tra,bot,Tic,wizarani na kuwa mwanajeshi,lakini kutokana na kwamba ukizaliwa africa ndoto zinaweza zisitimie basi nilijikuta naingia kufanya kazi ambazo sikuwahi kuzisomea au kuziwazia hata siku moja ingawa kwa naweza kusema zimenijenga na kunipa exposure ya kuelewa ulimwengu wa biashara na pia connection nazo nimekua nazo nyingi sana kwa kipindi hiki kifupi nilichojiingiza kwenye hii kazi,mtoto wa mkulima mimi sikutegemea kama kuna siku ningeweza kufanya biashara na maofisa kutoka ikulu ya Tanzania but kwa sasa ni kitu cha kawaida kwa mimi kuwa na appointment na maofisa wa ikulu kwa ajili ya kufanya biashara,kwa kifupi mimi kwa sasa nafanya kazi za sales katika lampuni moja ya wachina inayojishughulisha na importation ya vifaa vya magari hivyo nimejijengea urafiki na watu wa kila aina hapa nchini.
anway.imetokea issue ambayo inanifanya niwe dilemma katika maamuzi yangu,nami ni miongoni mwa vijana tulioitwa kazini tra lakini mpaka sasa nimeshindwa kuamua,ndugu zangu huko bush wananipigia kelele kwamba niende tra lakini hawa hawana exposure ya nini kinaendelea ulimwengun,wao wanajua nikiingia tra nitakua tajiri siku hiyo hiyo, kumbe kuna mengi ya kufanya huko.kwa sasa kampuni ninayoifanyia kazi wamenipa permanent contract toka mwanzoni mwa mwezi huu,mwanzo mshahara ulikua ni 0.75 gross lakini kwa sasa wameniongezea to 950000 gross,kila week napewa elfu 30 ya transport,elfu 15 ya muda wa maongezi,medical coverage wamenipa,house allowance ya 100000 kila mwezi na pia tunasafiri sana kwenda mikoani na nchi jirani.kwa kifupi maisha sio haba sana na ukizingatia sina majukumu makubwa yanayonikabili,malengo yangu yalikua ni kufanya kazi miaka mitatu na hawa jamaa ili baadae nami nije kufungua duka langu la spea za magari lakini sasa imejitokeza hii issue ya tra na huko kijijini watu naskia wmefanya mpaka sherehe eti kisa mtoto wao nimepata kazi tra,maslahi ya tra mimi siyajui yakoje na wala utendaji kazi wao siulewi ukoje ni kama naenda kuanza upya,halafu mbaya zaidi kuna madeni ya kampuni mengi tu yako nje ambayo natakiwa kuyakusanya hivo inaniwia ngumu kuondoka haraka haraka
kwa hiyo ningependa tushauriane kiundugu wakuu,nibaki na hawa jamaa zangu wachina au nitimkie tra maana wasiwasi wangu wa kwenda huko tra ni kwamba naamini ntapelekwa huko mikoani na mimi nimeshaanza kuset baadhi ya mambo yangu hapa mjini hivo nahofia yatakwama,
Wewe inaonekana u have a plan nzuri sema unataka kutuzuga umesema u want to own ur own business in 3 yrs TRA unafata nini? Stay ur game 3 yrs is kesho utapata ulichokitaka ....kuajiriwa na kampuni au serikali sio maisha trust me do your own utafika mbaaaali sana get married hauta chezea mkwanja this is from experience forget TRA hakisha u get ur own shop hutajutia ever ever
 
Mkuu mafanikio ya kufanya kazi tra kwa sasa inategemea na kiti ulichokikalia/ utakachokikalia.
 
kwani una mda gani tokea uanze kupiga kazi na wachina, kama ushatengeneza connection za kutosha nakushauri nenda TRA huku ukipiga business zako taratibu, unaweza kutafuta kijana uka mtrain wewe ukawa msimamizi hii itakupunguzia majukumu bila kuathiri utendaji kazi wako serikalini
 
Fuata Moyo wako, unataka nini ni wapi utadumu kwa furaha wakati unafanya kazi.

Na unaonekana kwa wachina ni Bora zaidi kuliko serikalinini kwa maana ya Experience uliopata na network ulionayo kwasasa kiasi chakuona fursa ya ziada, ama ndoto iliojitokeza ya kuwa Boss wa maisha yako katika bishara amabyo umeipanga kuifanya. Nafikiri huku ni kuzuri zaidi ya huko unapotaka kwenda. (TRA)

Otherwise ukichagua kwenda TRA, uje ututonyee tupate hiyoo fursa unayo ikataa kwa wachina mkuu
 
Ndugu yangu kama ni kweli haya uyanenayo Mungu anakuona...



Kama hufahamu maslahi ya TRA ulifanya usaili wa nini sasa? Au ndo kuwabania madogo wasipate kazi
 
kweli hata hiyo interview ya TRA sijui ulipitaje, hata aya hakuna...!!
ama kweli kua uyaone, hapa kwel nayaona mengi
 
Mkuu unaonaje unapoenda enda tra uniunganishe kwa wachina
 
VETTING

investigate (someone) thoroughly, especially in order to ensure that they are suitable for a job requiring secrecy, loyalty, or trustworthiness.
"each applicant will be vetted by police"
mkuu pamoja na kwamba uzi ni wa muda mrefu,, VETTING haifanywi na Police ni TISS
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom