niende tra au nifanyaje wakuu?

niende tra au nifanyaje wakuu?

Status
Not open for further replies.

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,721
Reaction score
25,516
naweza kusema kuwa miongoni mwa watu waliochaguliwa tra kwa nafasi ya custom officer ii is like dreams come true kwa sababu toka nikiwa mdogo mawazo yangu yalikua ni kufanya kazi sehemu tano tu ambazo ni tra,bot,Tic,wizarani na kuwa mwanajeshi,lakini kutokana na kwamba ukizaliwa africa ndoto zinaweza zisitimie basi nilijikuta naingia kufanya kazi ambazo sikuwahi kuzisomea au kuziwazia hata siku moja ingawa kwa naweza kusema zimenijenga na kunipa exposure ya kuelewa ulimwengu wa biashara na pia connection nazo nimekua nazo nyingi sana kwa kipindi hiki kifupi nilichojiingiza kwenye hii kazi,mtoto wa mkulima mimi sikutegemea kama kuna siku ningeweza kufanya biashara na maofisa kutoka ikulu ya Tanzania but kwa sasa ni kitu cha kawaida kwa mimi kuwa na appointment na maofisa wa ikulu kwa ajili ya kufanya biashara,kwa kifupi mimi kwa sasa nafanya kazi za sales katika lampuni moja ya wachina inayojishughulisha na importation ya vifaa vya magari hivyo nimejijengea urafiki na watu wa kila aina hapa nchini.
anway.imetokea issue ambayo inanifanya niwe dilemma katika maamuzi yangu,nami ni miongoni mwa vijana tulioitwa kazini tra lakini mpaka sasa nimeshindwa kuamua,ndugu zangu huko bush wananipigia kelele kwamba niende tra lakini hawa hawana exposure ya nini kinaendelea ulimwengun,wao wanajua nikiingia tra nitakua tajiri siku hiyo hiyo, kumbe kuna mengi ya kufanya huko.kwa sasa kampuni ninayoifanyia kazi wamenipa permanent contract toka mwanzoni mwa mwezi huu,mwanzo mshahara ulikua ni 0.75 gross lakini kwa sasa wameniongezea to 950000 gross,kila week napewa elfu 30 ya transport,elfu 15 ya muda wa maongezi,medical coverage wamenipa,house allowance ya 100000 kila mwezi na pia tunasafiri sana kwenda mikoani na nchi jirani.kwa kifupi maisha sio haba sana na ukizingatia sina majukumu makubwa yanayonikabili,malengo yangu yalikua ni kufanya kazi miaka mitatu na hawa jamaa ili baadae nami nije kufungua duka langu la spea za magari lakini sasa imejitokeza hii issue ya tra na huko kijijini watu naskia wmefanya mpaka sherehe eti kisa mtoto wao nimepata kazi tra,maslahi ya tra mimi siyajui yakoje na wala utendaji kazi wao siulewi ukoje ni kama naenda kuanza upya,halafu mbaya zaidi kuna madeni ya kampuni mengi tu yako nje ambayo natakiwa kuyakusanya hivo inaniwia ngumu kuondoka haraka haraka
kwa hiyo ningependa tushauriane kiundugu wakuu,nibaki na hawa jamaa zangu wachina au nitimkie tra maana wasiwasi wangu wa kwenda huko tra ni kwamba naamini ntapelekwa huko mikoani na mimi nimeshaanza kuset baadhi ya mambo yangu hapa mjini hivo nahofia yatakwama,
 
Wakati unaomba kazi na kufanya interview ulikuwa hujafanya maamuzi? Kama unaamini katika kuajiriwa na kufanikiwa kupitia ajira ya serikali nenda TRA.Kama unaamini kwenye kujiajiri,achana na TRA endelea na wachina,weka malengo na pambana kuhakikisha yanafanikiwa.Kama unapenda bata na kuendesha magari na mademu nenda TRA.
 
kama tra watakupanga hapa dar.. nakushauri nenda tra na usiondoke vibaya na wachina wako.. unaweza ukawasaidia kumalizia viporo vyako vya sales huku umesharipoti tra.. nimekwambia hivi sababu wachina hawaaminiki na biashara zinavurugwa sana awamu hii.

na kama umeshajenga trust na wachina wanakukubali.. endelea kufanya nao kazi part time hata kwa kujitolea tu... ili ukiona tra mizinguo unarudi zako uchinani

mara paap unaweza ambiwa hiyo kampuni ya wachina hailipi kodi ikafungiwa na ukakosa ajira...

ila nakueleza ukweli mdogo wangu tra ya sasa hivi sio kama zamani... nina rafiki yangu amefanya kazi tra kama miaka minne hivi... ameamua kuacha kazi tra kaona hakuna maslahi... ameamua kurudi kpmg..

na huyo jamaa anapenda hela balaa.. ila amekiri tra ya sasa hakuna utajiri wa haraka... ni kama staff wa mashirika mengine tu kutegemea mshahara tu...
 
Mkuu hapo uko njia panda, nina uhakika chochote utakachichagua kuna mahali utafika utawaza kama ulikosea.

Zote ni best positions, lakini the best one ni hii uliyonayo sasa, huhitaji rushwa kutengeneza hela, ile ya TRA utahitaji kupewa rushwa ili uweze kuwa na maisha mazuri, otherwise utakuwa wa kawaida tu. Na ukikaa kwenye kitengo kigumu unafifia mazima.

Fanya uamuzi kutoka moyoni mwako, angalia moyo unataka nini ili hata ikitokea mambo yakawa tofauti usiwe na mtu wa kumlaumu, uichukulie kama ni ajali tu.
 
sina uhakika kwa kuangalia avatar inaonesha wewe ni wa kike..

wewe umewaza kufukuzwa kwake tu.. jamaa goal yake ni kufungua duka lake la spare miaka mitatu ijayo aache kazi hapo... na sehemu anayopata experience ya spare ni hapo kwa wachina... unamwambia aende tra bila kufikiria... je tra atapata experience na connection za hizo spare siku awe na kampuni yake ya spares???

au unawaza kuajiriwa tu hadi kustaafu kupata kiinua mgongo??

nimekumbuka jamii nyingi africa wanawake hawahusishwi kupanga maamuzi ya jamiii sababu wana ujinga mwingi...

ndio maana maamuzi magumu wanawake wanawekwa pembeni... mambo ya kuomba kazi kwake sio hoja kwa kikao hiki

Tatizo kampuni binafsi kufukuzwa nje nje tofauti na serikali.

Ulifanya interview ya nini ikiwa ulikua huna shida nayo nyie ndiyo mnazibia wenzenu nafasi.
 
sina uhakika kwa kuangalia avatar inaonesha wewe ni wa kike..

nimekumbuka jamii nyingi africa wanawake hawahusishwi kupanga maamuzi ya jamiii sababu wana ujinga mwingi...

ndio maana maamuzi magumu wanawake wanawekwa pembeni... mambo ya kuomba kazi kwake sio hoja kwa kikao hiki
Una uchungu sana mimi kucomment vile? Jifungue basi
 
Mkuu kama unataka kufanya kazi full time na kwa job security TRA uhakika ila kama unasema unampango wa kujiajiri after 3 yrs unaweza kubaki huko huko tu lkn mwamuzi wa mwisho ni wewe subiri na maoni ya wakuu wenginee
 
Nenda TRA acha ujinga,hata kama mshahara mdogo nenda TRA hata kama utapangwa Lindi nenda TRA....ushauri ndo huo kuna mambo mazuri yamefichwa hayapo ndani ya mkataba ukiyajua utanitafuta kunishukuru......Nenda TRA!!
Tena akipangiwa mpakani atakuja kukumbuka maneno yako.
 
Nenda TRA acha ujinga,hata kama mshahara mdogo nenda TRA hata kama utapangwa Lindi nenda TRA....ushauri ndo huo kuna mambo mazuri yamefichwa hayapo ndani ya mkataba ukiyajua utanitafuta kunishukuru......Nenda TRA!!
Ikiwezekana mwambie hayo mazuri yaliyo fichwa ili afanye maamuzi mazuri mkuu.
 
Ushaur wangu mkuu ni huu " Kaa uwaze Unachokitaman leo na utakachokihitaji Kesho" Ukijua vyote viwili then itakusaidia kwenye maamuz yako.
 
Mkuu kama unataka kufanya kazi full time na kwa job security TRA uhakika ila kama unasema unampango wa kujiajiri after 3 yrs unaweza kubaki huko huko tu lkn mwamuzi wa mwisho ni wewe subiri na maoni ya wakuu wenginee
TRA kufukuzwa nje nje,kuna jamaa yetu alikuwa tra mtukula alifukuzwa kazi kwa fitna akafungua kesi sijui iliishia wapi ila akapata kazi Aghakan Mtwara.Siku hizi sijui yuko wapi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom