MartinCoder
JF-Expert Member
- Feb 20, 2018
- 700
- 630
Simu kwa asilimia kubwa ni kitu cha kwanza kwa wengi wetu kukitazama asubuhi na kitu cha mwisho kukiangalia usiku kabla ya kulala. Simu zetu haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika kadhaa. Ni mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo nakudokeza mambo muhimu ya matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini.
1.Kutozungumza na simu wakati wa kula chakula na mikutano
Ni vizur zaid kuzima Simu wakati wa chakula na mikutano . Mojawapo ya nidhamu ya chakula ni kutoongea na simu wakati wa kula (hasa unapokula na wenzio).Kwa sababu ya kuheshimu chakula, baadhi ya watu pia huzima televisheni wakati wakiwa kwenye meza ya chakula.
2. Kutosikiliza radio/muziki n.k wenye sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma
Kitaalamu huitwa sodcasting yaani tabia ya kusikiliza muziki/radio kutoka kwenye simu au vifaa vingine kwa sauti kubwa bila kujali wanao kuzunguka.Hii inahusisha pia kutazama video au kucheza michezo ya kwenye simu kwa sauti kubwa.
3.Kutozungumza na simu wakati unapotakiwa kumsikiliza mtu mwingine
'Kutuma ujumbe au kuzungumza na simu ni tabia mbaya sana wakati unapokuwa unazungumza au una msikiliza mtu mwingine. Kutopeana muda na wenzio ni kupoteza nafasi kubwa sana ya kufahamiana au kuelewana vizuri''.
4. Kutotembea huku umeinamisha kichwa ukitazama simu yako
Matokeo ya kutembea wakati umeinamisha kichwa na macho yakiwa kwenye kioo cha simu ;ni kujikwaa , kugongana na watu njiani, kukosea njia, kugongwa na gari/pikipiki/baiskel n.k, kuanguka kwenye mitaro ,kugonga ukuta /mti n.k. Epuka tabia hiyo
5. Kutozungumza na simu yako kwa sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma
Kuzungumza na simu yako kwa sauti kubwa wakati upo kwenye usafir wa Umma ni Kero sana kwa wengine.
6. Kutomuegemea mwenzio kwenye usafiri wa Umma (Hasa Dar es salaam kwenye mabasi ya mwendokasi/daladala za mbanano) wakati we mikono yako iko busy na kuchat kwenye simu badala ya ku-control mwili wako mwenyewe kwa kushikilia juu katika sehemu za kushikilia.
MWENYE NYONGEZA ALETE HAPA !