Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,884
- 50,741
Nimetafakari sana kwamba tunakoelekea taarifa zetu zilizoko NIDA ndizo pekee zitakazotumika kufanya usajili wa mambo mbalimbali. Kupata Passport, kuandikishwa kuwa mpiga kura, kufungua akaunti Benki, usajili wa Laini za Simu, usajili kwenye taasisi zote za umma zilizoko kwenye co.tz na mambo mengine mengi sana.
Hivi ikitokea taarifa zako zikasiasishwa (Politicized) na hatimae kufungiwa, mwananchi wa kawaida atafanya nini ili taarifa hizo zifunguliwe na yeye apate haki yake ya kiraia? Fikiria unataka kumwekea dhamana ndugu yako na unaambiwa taarifa zako kwenye tovuti ya NIDA hazipo!
Nimewaza hayo baada ya kugundua kwamba sasa hata unapokwenda kusajili laini ya simu anaekusajili anaingiza tu namba ya kitambulisho chako cha NIDA na mengine yanafanywa na tovuti ya NIDA. Vivo hivo hata kwenye kujisajili BRELA kupitia mtandaoni.