Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,896
- 4,495
Kufuatia wito wa Mh. Rais kwamba vijana tutumie mitandao kukosoa lakini pia tupendekeze suluhisho la yale tunayoyakosoa, leo nina pendekezo juu ya suala zima la utoaji wa vitambulisho vya utaifa kupitia NIDA.
Utangulizi;
Ninafahamu hali ya kifedha ya baadhi ya watanzania wenzetu ni ngumu sana na hivyo nikiri wazi kuwa wazo la kutoa vitambulisho vya utaifa BILA MALIPO lilikua ni jema kabisa. Ukizingatia mahitaji ya kitambulisho hiki katika huduma mbalimbali, ni hakika kuwa kila Mtanzania stahiki anatakiwa kukipata bila makwazo yoyote ya kifedha
Hivyo basi,
Kwa kutoa vitambulisho bure kabisa, tumetengeneza "gharama" kubwa zaidi. (Time is Money):
1. Mtaani kuna malalamiko ya wananchi juu ya muda wanaotakiwa kusubiri ili kupata vitambulisho vyao mara baada ya kujisajili katika ofisi za mamlaka (NIDA). Wapo waliosubiri miaka miwili, miaka mitatu, mwaka mmoja, n.k
2. Ripoti ya CAG (iliyosomwa hivi karibuni) inaonyesha kwamba, kwa kasi ya utengenezaji vitambulisho wanayokwenda nayo NIDA, ni wazi zile materials zilizopo stoo zitafikia muda wa kuharibika kabla ya kutumiwa, hivyo kuipa serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.
3. Ukipoteza kadi yako, ukataka nyingine yaani ku-Renew, mara baada ya kulipia Tshs 21,000/= na kukamilisha taratibu zote za kipolisi za kupotelewa mali, utatakiwa KUSUBIRI kadi hiyo kwa MIEZI MITATU (kama mtu anayejiandikisha upya).
Kutokana na hoja tatu tajwa hapo juu, ni wazi kwamba mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA, inakosa ufanisi kwa maana ya uchache wa VIFAA na uhaba wa RASILIMALI WATU kuweza kuendana mahitaji utoaji wa vitambulisho KWA WAKATI.
Suluhu:
1. Tuijengee uwezo NIDA kibajeti, nilisikia wakati fulani waziri Simbachawene anasema wataiwezesha taasisi hii kwa kuiongezea mashine zaidi.
2. Wananchi tuchangie kupata vitambulisho hivi. Iwekwe gharama nafuu (Hata elfu 5 au elfu 10), mtu alipie na apate kitambulisho chake angalau ndani ya wiki MOJA.
Hizi fedha zitumike kuongeza mashine, kuajiri watumishi ili kuongeza ufanisi wa NIDA kama taasisi.
Je, tozo hii itakua ni mzigo kwa mwananchi?
Ndiyo, ukilinganisha na BURE, tozo yoyote ile ni mzigo.
Lakini ukilinganisha na adhabu ya kusubiri kwa mwaka mmoja au hata miaka miwili kuelekea mitatu (mzigo wa sasa), tozo ninayoipendekeza si lolote, si chochote.
Wasio na uwezo watafanyaje?
Wale wasio na uwezo wa kuilipa kama wazee vikongwe, hawa watatuomba hukuhuku kwenye jamii hiyo elfu 5 au elfu 10, kitambulisho sio suala la dharula, siku akipata hiyo pesa na akaenda NIDA basi alipe na apate kwa wakati.
Je, utaratibu wa kulipia huduma ni mgeni?
Hapana. Tunalipia vyeti vya kuzaliwa, tunalipia hati za kusafiria, tunalipia huduma kedekede ambazo ni haki zetu za msingi kuzipata.
Kama huduma inapatikana kwa wakati, hamna mtu anaweza kulalamikia malipo ya huduma hiyo.
Kwa sasa kitu pekee wanachoweza kijivunia watu wa NIDA, ni kutoa "namba za NIDA" yaani NIN.
Kimsingi hii ni "nusu huduma", tunataka mamlaka inayoweza kutupatia vitambulisho (physical ID) kwa wakati.
Burebure ya NIDA inatuchelewesha.
Asubuhi njema kwenu.