NIDA ni jipu lingine, ikiwezekana hili tulitumbue wenyewe

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Apr 3, 2018
336
559
Ofisi ya Vitambulisho vya Taifa NIDA hususani ya hapa Kibamba (Manispaa ya Ubungo) inayosave Ubungo, Sinza, Kimara hadi Mbezi yote na Kibamba.

Process ya kuanza kujiandikisha hadi kupata kitambulisho ni hapa na Morogoro kwa mguu. Mara umeme umekatika mara Network imekata, unafika saa kumi na mbili asubuhi kuwahi foleni wanafungua saa mbili na mnaambiwa network iko down mmara mashine ya picha haitoi vizuri, mnaondoka saa kumi au kumi na moja bado mmepigwa kalenda ya njoo kesho.

Kama hawa jamaa hawakujipanga mbona wasiache tu hili zoezi la Ubungo kwanini wasiwe na plan b ya uhakika kama jenereta au hata wangeliacha eneo lenye uhakika wa mtandao na umeme basi.

Hakyanani wale watu wazima wanaoacha shughuli zao, biashara na kuenda kufuatilia vitambulisho, wagonjwa na wahangaikaji kama sisi wanatuchosha.
 
Back
Top Bottom