Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,614
Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania NIDA ina uhalali na ulazima gani kuwepo?
Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Research ICT Africa iliyochapwa 16 Julai 2021, NIDA imefikia tu 6.2% ya wananchi tangu mwaka 2008 kilipoanzishwa (zaidi ya miaka 14, mtoto anazaliwa hadi anafika kidato cha 3 au 4).
Kama kuna taasisi zimependelewa nchi hii na awamu za JK na JPM NIDA ni ya kwanza.
NIDA wamepewa vifuatavyo:-
1. Kasma.
2. Rasilimaliwatu.
3. Miundombinu ya majengo.
4. Teknolojia.
5. Ulinzi.
6. Mafunzo.
7. Magari.
8. Mpigachapa wa Serikali.
9. Mikono ya shirika toka RITA, Hazina, Polisi, Uhamiaji, Bunge, TAMISEMI, Mambo ya Ndani, Sheria na Katiba, Mahakama, Media, Elimu Sayansi na Teknolojia nk.
NIDA imebadilishiwa uongozi, teknolojia na bajeti zaidi ya mara 2 tangu 2008.
NIDA imeishalalamikiwa na hata kukaripiwa na Mamlaka zifuatazo kwa utendaji wa hovyo na dhaifu:-
1. Ofisi ya Rais.
2. Mambo ya Ndani.
3. Bunge.
4. Wananchi.
5. Media.
6. TAKUKURU.
7. CAG.
8. PAC.
Taasisi zinazoweza kufanyakazi inayofanywa na NIDA; kwa tija kubwa ni hizi:
1. Uhamiaji.
2. Idara ya Takwimu.
3. NECTA.
4. TISS.
5. Kanisa (hasa Roman Catholic).
Mambo-chechefu yaliyo kwenye utendaji wa NIDA:-
1. Rushwa.
2. Ucheleweshaji (tangu 2019 wengi hatujapata vitambulisho na tuliambiwa vina uhai wa miaka 2 tu tangu muda unapoomba siyo muda unaokabidhiwa).
3. Kutobuni mfumo wa kuhakikisha pasina shaka uhalali wa uraia wa mwombaji.
4. Kutojitambua kuwa NIDA ni Mamlaka siyo Idara (Mamlaka na Idara viko tofauti). Mamlaka ina meno Idara ina mapengo. Sasa kwa NIDA imekuwa vice-versa.
5. Kwenye No.4 hapo juu, taasisi nyingi nchini hazitambui na zinabeza Mamlaka ya NIDA pale zinapokataa kutambua matumizi ya namba za kitambulisho zinazotolewa kihalali na NIDA kabla IDs hazijachapwa. NIDA inaagiza kwamba namba za IDs zitambulike na wenye nazo wapewe huduma sawa na walioishapata IDs kamili lakini wananchi wengi wananyimwa haki zao sehemu za kutolea huduma pale wanapotoa namba za IDs badala ya IDs zenyewe (imekuwa kama nyumba ya kambale)
Ni dhahir shahir kwamba NIDA hawana vigezo na sababu za kujitetea. Utetezi pekee ninaodhani NIDA wanaweza kutumia ni huu: "Itungwe Sheria ya kuwazuia Watanzania wasizaliane kuanzia sasa hadi hapo waliopo wawe wamemaliziwa kupewa IDs; ili kukidhi spidi ndogo ya NIDA"
Ni hakika kwamba hivi sasa NIDA hawamuhofu mtu yeyote wala taasisi yoyote tena, kwa sababu kama wamekwishakemewa na wafuatao na hawajabadilika basi labda tusubiri Dahari itimie:-
1. Ofisi ya Rais.
2. Mambo ya Ndani.
3. Bunge.
4. Wananchi.
5. Media.
6. TAKUKURU.
7. CAG.
8. PAC.
NB.
Hata tukikusanya saini za wenye nchi na kupeleka shauri Kortini (kwamba hizo namba 1- 8 hapo juu zimeshindwa kuidhibiti NIDA) bado NIDA itaibeza Korti kwa sababu labda pia inajuwa bei ya Korti ili iweze kushinda shauri.
Tz haijajuwa umuhimu wa vitambulisho vya taifa kwa usalama wake. NIDA nayo haijijui kama ni moja ya taasisi za usalama wa nchi (watchdog institution) ambayo nayo inadhibiti mipaka ya nchi kwa njia ya vitambulisho.
NIDA ni White Elephant Project iliyoingia kwenye historia ya nchi.
Nadhani tukubaliane kwamba:
Tanzania haijawa tayari kwa Vitambulisho vya Uraia kama ambavyo haijawa tayari kwa Katiba Mpya.