NIDA Arusha ni jipu

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Wana Jamvi habarini za kazi.

Nimefika hapa Arusha wiki moja iliyopita katika kufanya maandalizi ya safari na jamaa zangu. Kwa masikitiko sana jamaa yetu mmoja anayefanya kwenye taasisi moja hapa Arusha anaelekea kukwama kwa kukosa passport kiini cha tatizo kikiwa ni madudu ya Uongozi wa NIDA Arusha. Nimelifuatilia hili suala kwa karibu nikaona mambo mengi yanayofanywa na ofisi ya NIDA Arusha ambayo kuyafumbia macho si rahisi.

Hatuwezi kunyamaza tunapoona ofisi zinazoendeshwa kwa kodi zetu, zikiendeshwa kama idara za familia. Kuendelea kufumbia macho uchafu kama niliouona ni kuhalalisha mfumo unaotugharimu Watanzania wa kutokuwa na uwajibikaji na watu kutumia madaraka kwa utashi wao huku wakihujumu haki za kiraia za watu wengine.

Niaomba mwenye mawasiliano ya kiongozi wa juu wa NIDA asiyekuwa mchaga, anitumie ili niwasiliane naye. Sitaki kuweka hapa undani wa nilyoyakuta hapa kwa sababu naogopa kutoa mwanya kwa wahusika kuharibu ushahidi. Ninataka matatizo hayo yabaki kama yalivyo ili vyombo vinavyohusika vijionee na kuweza kuchukua hatua sahihi za kukomesha hizi tabia za matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa wananchi katika kupata haki zao za kiraia.

Narudia kusema, nainaomba mawasiliano ya Simu ya kiongozi wa juu wa NIDA asiyekuwa Mchagga, nikiwa na maana kamili ili niwasiliane naye juu ya hali iliyopo, kabla sijalifikisha hili suala kwenye vyombo vingine.

TUMECHOKA. NI WAKATI WA WATANZANIA KUDAI HAKI ZAO MCHANA.
 
Nida sio huko tu, ni kama hawajajipanga tu nchi nzima wapo tu ilimradi siku zinasogea
 
Kwanini wayafanye hayo , taasisi nyeti kama hiii kweli ????

Sasa tunakwenda kuwapa madudu yanayofanywa na kiongozi wao Arusha ili wakiamua waelewe kwamba watu wanahitaji huduma na si upumbavu mwingine wowote.
 
  • Thanks
Reactions: sab
pole sana mkuu ila kuhusu nida jipu kubwa si arusha tu ata morogoro akuna wanacho fanya alafu wizara husika imefumbia macho

Tatizo lilik o Arusha ni siyo la kitaasisi bali ni suala la mtu binafsi anayefanya atakavyo kwa maslahi yake biinafsi bila hata hisia kwamba anayoyafanya ni kinyume na misingi ya kazi popote pale. Nimeambiwa kwamba kwa kuwa ni wachagga, hakuna mtu atawafanaya kti maana hata wakubwa wa NIDA ni wachagga na wamekuwa wakiendsha hivyo mambo kwa muda mrefu. Sasa nataka kuona kama uovu huu nitakaokwenda kuwapa wataufumbia macho kwa kuwa ni Wachagga.
 
Nida huku kwetu pia ni chenga2 watu wa wilaya ya kinondoni tuliochaguliwa baada ya usaili hatujui project imekwamia wp almost ni mwezi wa 5 nw hatujui inaanza lini kazi
 
Hili halina ukweli njoo inbox
 
Nida huku kwetu pia ni chenga2 watu wa wilaya ya kinondoni tuliochaguliwa baada ya usaili hatujui project imekwamia wp almost ni mwezi wa 5 nw hatujui inaanza lini kazi

Halafu pamoja na kujua kwamba NiDA ufanisi uko hivyo, bado serikali inaambatanisha upatikanaji wa pass za kusafiria na vitambulisho vya NIDa ambavyo vinapatikana kwa utashi wa watu na si kwa mahitaji ya jamii. Hii ni ajabu kweli
 
Wana Jamvi habarini za kazi.

Nimefika hapa Arusha wiki moja iliyopita katika kufanya maandalizi ya safari na jamaa zangu. Kwa masikitiko sana jamaa yetu mmoja anayefanya kwenye taasisi moja hapa Arusha anaelekea kukwama kwa kukosa passport kiini cha tatizo kikiwa ni madudu ya Uongozi wa NIDA Arusha. Nimelifuatilia hili suala kwa karibu nikaona mambo mengi yanayofanywa na ofisi ya NIDA Arusha ambayo kuyafumbia macho si rahisi.

Hatuwezi kunyamaza tunapoona ofisi zinazoendeshwa kwa kodi zetu, zikiendeshwa kama idara za familia. Kuendelea kufumbia macho uchafu kama niliouona ni kuhalalisha mfumo unaotugharimu Watanzania wa kutokuwa na uwajibikaji na watu kutumia madaraka kwa utashi wao huku wakihujumu haki za kiraia za watu wengine.

Niaomba mwenye mawasiliano ya kiongozi wa juu wa NIDA asiyekuwa mchaga, anitumie ili niwasiliane naye. Sitaki kuweka hapa undani wa nilyoyakuta hapa kwa sababu naogopa kutoa mwanya kwa wahusika kuharibu ushahidi. Ninataka matatizo hayo yabaki kama yalivyo ili vyombo vinavyohusika vijionee na kuweza kuchukua hatua sahihi za kukomesha hizi tabia za matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa wananchi katika kupata haki zao za kiraia.

Narudia kusema, nainaomba mawasiliano ya Simu ya kiongozi wa juu wa NIDA asiyekuwa Mchagga, nikiwa na maana kamili ili niwasiliane naye juu ya hali iliyopo, kabla sijalifikisha hili suala kwenye vyombo vingine.

TUMECHOKA. NI WAKATI WA WATANZANIA KUDAI HAKI ZAO MCHANA.
Nida ni jipu sana hawa wadada wa nida unaenda kuulizia kitambulisho utafikiri umeenda kuwaomba kazi aisee wana jiskia na hali wana sura za mbuzi tu wanaboa sana kwa kweli
Kuna siku nimeenda mkoani songwe hapa vwawa kuulizia kitambulisho wamenijibu shombo sana mpaka nikasema siji kufatilia tena hicho kitambulisho wakae nacho tu
 
Kwa Arusha ni uozo wa majibu lakini kuna makubwa zaidi ya majibu.
 
Back
Top Bottom