Nicola Tesla. ugunduzi wake wa umeme uliobadilisha dunia hadi leo, na jinsi maisha yake yalivyoishia kuwa ya umasikini na upweke

Nicola Tesla. ugunduzi wake wa umeme uliobadilisha dunia hadi leo, na jinsi maisha yake yalivyoishia kuwa ya umasikini na upweke

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
993
Reaction score
1,882
‎Maisha ya Nikola Tesla ni moja ya hadithi za kuvutia sana katika historia ya sayansi, hadithi ya mtu aliyekuwa na akili ya ajabu sana lakini pia maisha yaliyojaa mafanikio makubwa na baadaye upweke na matatizo.

‎Tesla alizaliwa mwaka 1856 katika kijiji kidogo kilichokuwa ndani ya Dola ya Austria-Hungary, eneo ambalo leo ni sehemu ya Croatia. Baba yake alikuwa mchungaji wa kanisa la Orthodox na mama yake hakuwa amesoma shule rasmi lakini alikuwa na kipaji cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya nyumbani. Tesla mwenyewe baadaye alisema akili yake ya kubuni alirithi kwa mama yake. Tangu utoto alikuwa na kumbukumbu kali sana na uwezo wa kufikiria mashine nzima kichwani bila hata kuchora mchoro, kisha kuileta kwenye uhalisia ikiwa imekamilika kabisa.

‎Alipokua kijana alienda kusoma uhandisi na baadaye alihamia New York City alipambana sana mtaani akafanya kazi ngumu ambazo tuseme ni za saidia fundi . Baadae alianza kufanya kazi kwa Thomas Edison baada ya Edison kuona uwezo mkubwa waa Tesla na kumuajiri. Hapo ndipo safari yake kubwa ya kisayansi ilipoanza.

‎Tesla alikuwa na wazo tofauti kuhusu namna umeme unavyopaswa kusambazwa. Edison alikuwa anaunga mkono mfumo wa direct current (DC), na kampunibyake tayari ilikua inasambaza umeme kwa namna hiyo ( hii namna inapoteza umeme mwingi njiani na umeme hauwezi kusafirishwa umbali mrefu, kila baada ya mita kadhaa lazima kuwe na substation.
lakini Tesla aliamini mfumo wa alternating current- AC ( huu tunaotumia sasa kupokea kutoka TANESCO ) aliamini AC ingeweza kusafirisha umeme umbali mrefu kwa ufanisi zaidi, bosi wake Thomas Edison hakuamini katika AC na hakuwa tayari kubalilisha mfumo na ku risk biashara yake ambayo tayari ilikuwa imepokelewa vizuri.

‎Baadaye mfanyabiashara George Westinghouse alimpa msaada wa kifedha, Tesla akaunda mfumo mzima wa namna ya kusafirisha umeme kwa AC, na mfumo wa AC ukawa msingi wa gridi nyingi za umeme duniani mpaka leo.

‎Katika kipindi hicho Tesla alipata mafanikio makubwa sana. Alitengeneza Tesla coil, alikua maarufu sana akafanya majaribio ya umeme wenye voltage kubwa, na akaonyesha uwezekano wa kusafirishaa umeme bila waya. Wakati Vita ya umeme ikiendelea kati ya wafuasi wa Edison na Tesla, dunia ilianza kuona kwamba mawazo ya Tesla yalikuwa na nguvu sana sana...

‎Tesla alikua na akili za kipekee sana ambapo mawazo yake watu wengi hadi wanasayasi wenzake waliona haiwezekani, alikua ni mtu wa kupenda maisha ambayo ni luxury na aliwaza mambo luxury ambayo kwa kipindi hichilo yalionekana haiwezekani.
aliwaza kuongea na mtu wa mbali papo kwa papo bila kutembea ( kama simu au redio leo ), aliwaza kutuma picha kwenda sehemu nyingine ya dunia, aliwaza kusafirisha umeme dunia nzima bila kutumia waya.
‎vitu vingi vilionekana haviwezekani na kumfanya aanze kupuuzwa na watu wengi kwani ilionekana anaongea kuhusu imagination zaidi na vitu vusivyoweza kuwa uhalisia.

‎Wakati fulani alisema alipokea ishara za ajabu kupitia vifaa vyake vya umeme na akasema zilikuwa zinatoka kwenye sayari ya Mars. Wanasayansi wengi waliona labda ilikuwa ni mawimbi ya kawaida ya redio au kelele za vifaa vya umeme, lakini madai hayo yalifanya watu wazidi kumchukulia kama mtu aliyekuwa anapoteza muelekeo wake katika sayansi...

‎Mojawapo ya mradi maarufu wa Tesla ulikuwa mnara ulioitwa Wardenclyffe Tower, ambao Tesla alitaka atume umeme na mawasiliano bila kutumia waya. duniani kote,
mradi huo mwanzo uliungwa mkono mfanyabiashara tajiri duniani kwa wakati huo, J. P. Morgan, na akaufadhili kwa kuweka hela nyingi. Lakini baada ya muda Morgan alikata msaada wake wa fedha hili lilichangiwa na Tesla kuonekana na mawazo qmbayo ni magumu kuwa uhalisia, kwaiyo mradi huo ukasimama, na hapo ndipo anguko la Tesla likaanza kuonekana wazi.
Tesla aliuza maeneo aliyokua ameyatenga jwa project zake aliuza na eneo alipojenga mnara huo wa wardenclyffe na mnara huo ulibomolewa na vyuma vyake kuuzwa... Tesla akapoteza karibu kila kitu pia hakukia na tajiri aliyeweka hela kufadhili project zake kutokana na mawazo yake kuonekana hayawezekani na yangegarimu pesa nyingi sana....

‎Tesla baada ya kuuza vitu vyake alirudi kuishi peke yake katika hoteli ndogo ndani ya New York City. Hakuwahi kuoa, na pia marafiki wengi wa zamani walikuwa tayari wamepotea katika maisha yake.

‎pia Tesla alikuwa na tabia nyingi za ajabu sana. Tesla alipenda sana namba 3, 6 na 9, na mara nyingi alihakikisha vitendo vyake vinafuata mpangilio huo. Inasemekana kabla ya kuingia kwenye jengo angeweza kulizunguka mara tatu pia kwenye hotel aliku anakaa kwenye chumba chenye namba inayogawanyika kwa 3

moja ya misemo inayohusishwa naye ni huu:
‎" if you know the magnificence of 3, 6, and 9 you have the key to the universe" akimaanisha kua ukitambua umuhimu wa namba 3, 6 na 9 tayari una ufunguo wa kujua siri za ulimwengu.

‎pia Tesla alikua na usafi uliopita kiasi na aliogopa sana vijidudu. kadri alivyozidi kuwa mzee tabia hizi ziliongezeka na maisha yake yakawa ya upweke zaidi.

katika uzee wake ‎Tesla alikuwa anafuga njiwa wengi, lakini kuna njiwa wake mmoja alimpenda sana na alizoeana nae sana, ni kama mwanamme anavyompenda biti mzuri sana aliyeuteka moyo wake.
‎Tesla alikuwa na mapenzi ya dhati kwa huyo njiwa na walizoeana sana.
‎Siku moja njiwa huyo alikufa, Tesla katika interview moja alisema kuwa baada ya huyo njiwa kufa aliona kama mwanga mkali sana umemmulika machoni na baada ya hapo alihisi maana ya yeye kuishi duniani imeondoka kabisa. kuanzia hapo aliona maisha hayana maana yoyote.

‎Mtu ambaye ameiwasha dunia kwa mawazo yake mapya ya umeme aliishia kufa mwaka 1943 akiwa maskini na mpweke aliyesahaulika kabisa kwa wakati huo.

‎mawazoyake ya ugunduzi wa AC aliyafanyia hatimiliki ya ugunduzi ( patent ) ila mwanzoni tu wakati bado kamupuni inapata upinzani mkubwa aliuza hakimiliki yake kwa dola chache sana, ili kuruhusu kampuni iendelee yenyewe na isianguke.
‎Bila kuuza hatimiliki yake angekua mmoja ya ma bilionea wakubwa zaidi katika historia ya dunia, kwaajili ya ugunduzi wa AC mfumo wa kusafirisha umeme unaotumika dunia nzima.

‎pia mawazo yake ya Radio na simu ambayo pia hakuyafanyia hatimiliki, yakachukuliwa na wengine.
( imagine radio na simu kipindi hicho hazikwepo, saivi ni kitu cha kawaida kila mtu anamiliki. ingemuingizia mabilioni ya dola )

‎pia moja ya mawazo yake makubwa ambayo bado hayajatimia hadi sasa... kusambaza umeme bila kutumia nguzo au waya, ( witeless ) ambayo kwa sasa yanaonekana hayawezekani au inaonekana Tesla alikua wrong ! ( hakua sahihi )

‎pia kosa lingine kubwa kwa Tesla likikua ni kuwaza tofauti na wafanyabiashara. mfano Tesla alitaka asambaze umeme na mawasiliano bure au kwa garama ndogo na sio kuifanya iwe biashara. pia mawazo yake mengi aliyafanya kama uvumbuzi utakaosaidia watu bure na si kwa mantiki ya kibiashara, kitukilicho changia kutokuungwa mkono na kutopataufadhili kutoka kwa matajiri na wafanyabiashara wakubwa wa kipindi hicho.

‎Lakini baada ya kifo chake dunia ilianza kumkumbuka tena ( hasa baada ya maono yake waliyoona hayatekelezeki, kuanza kutelelezeka na kuwa sehemu ya kawaida ya maishanya kilasiku kama simu na redio ).

Leo jina la Tesla linahusishwa na uvumbuzi mkubwa katika historia ya umeme, na hata kampuni ya magari ya umeme Tesla, Inc. Ya bilionea Elon Musk ilichukua jina lake kumuenzi.
‎Hadithi yake imebaki kuwa mfano wa ajabu wa jinsi akili kubwa sana inaweza kubadilisha dunia, lakini maisha ya mwanasayansi huyo yakabaki kuwa magumu na ya upweke.
 
images (7).jpeg

Nicola Tesla
 
Tesla ni moja wa wanasayansi wa muhimu zaidi ambao dunia iliweza kupata mawazo yake, alikua mtu wa kipekee sana. ( akili yake haikuweka hela mbele bali ililenga kubadilisha namna ya maisha )
Hilo ndilo kosa lake
 
Hilo ndilo kosa lake
kosa kwa mtazamo huo, saivi unatumia umeme kwa kilakitu. Unachukulia "for granted" angeweka hela mbele kwa kila kitu kiasi kwamba angeacha idea ya umeme wa AC ifutike kwasababu hela haikumtosha, je saivi ungekua unatumia nini kuchaji simu na kuingia JF ?
 
Back
Top Bottom