NIC vituko vitupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NIC vituko vitupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  NIC vituko vitupu
  MASIKINI Mary Mtengeti. Uteuzi wake kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) umefutwa kabla hajamaliza hata saa 24 kwenye kiti.

  Badala yake serikali imemteua J.P Mwandu, ambaye amekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Idara ya Usimamizi wa Bima wa NIC kushika nafasi hiyo.

  Mtengeti ambaye amekuwa mwanasheria wa NIC kwa miaka tisa, aliteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi kushika wadhifa huo Alhamisi iliyopita kuziba nafasi ya Margret Ikongo, Mkurugenzi Mtendaji aliyehamishiwa makao makuu ya wizara ya fedha.

  Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na serikali kuhusu kuenguliwa kwa Mtengeti ambaye uteuzi wake ulifanywa chini ya mwenyekiti wa Bodi ya NIC, Dk. Hamis Kibola.

  Margret Ikongo alitema ukuu wa shirika hilo wiki iliyopita baada ya madai ya muda mrefu, kutoka kwa wafayakazi na wadau wengine wa NIC, kuwa utawala wake umekosa dira, usimamizi na umesababisha shirika kuporomoka kibishara.

  Kubanduliwa kwa Mtengeti kitini kunahusishwa na taarifa ofisa mmoja wa shirika alivujisha maswali ya usaili kwa Mtengeti, jambo ambalo wachunguzi wanasema lilifanya Mtengeti aporomoshe majibu kama aliyekariri.

  Mmoja wa watu waliotuhumiwa kuvujisha maswali kwa Mtengeti ni Harun Mgude ambaye hata hivyo, MwanaHALISI lilipomuuliza kuhusiana na hatua hiyo, alikana katakata kujua lolote juu ya vitendo hivyo.

  Alipoambiwa kuwa ni yeye aliyekuwa kaimu katibu wa bodi iliyoteua Mtengeti, alikana na kusema “Sihusiki. Sijui” na kisha kukata simu yake ya mkononi.

  Ingawa serikali haijatoa taarifa juu ya hatua yake ya kumkataa Mtengeti, imefahamika kuwa mwanasheria huyo wa NIC amekuwa karibu sana na Mkurugenzi Mtedaji (Ikongo) aliyeng’olewa na kwamba mmoja asingekuwa mchafu na mwingine kubaki “safi.”

  Katika taarifa yake ya ukurasa mmoja aliyoitoa kwa wafanyakazi, Ikongo alitaka wafanyakazi waliobakia NIC kutoa ushirikiano kwa Mtengeti huku akiahidi kuwa balozi wa shirika huko aendako.

  “Naomba ushirikiano mlionipa mimi, pia mumpe Bibi Mary Mtengeti aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. Nami nitaendelea kuwa balozi wa NIC,” alisema.

  Toleo la wiki iliyopita la MwanaHALISI liliripoti kuwa tayari serikali imemwagiza Ikongo kukabidhi ofisi za NIC kwa mwenyekiti wa Bodi, Dk. Hamis Kibola na yeye (Ikongo) kuripoti wizara ya fedha kitengo cha usimamizi wa shughuli za bima (ISD).
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hili shirika limeshajifia, watu wanataka kuuana kwa sababu gani?
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kweli watauana ila shirika lina rasilimali ya majengo mengi sana .....wasije wakaliacha life kirahisi...
   
 4. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hili shirika halijafa kiasi hicho linachoitaji ni strategist ambaye anaweza kuturn around operation zake na kuwa zenye manufaa, yeyote atayeingia kama hawezi kusoma nyakati na kukabili hali ya biashara kwa ushindani, hataweza.

  Shirika hili wangelikabidhinkwanza kwa mtu mpya kabisa kwenye mashirika ya umma wampe muda aonyeshe ni jinsi gani anaweza kuturn around hili shirika kabla ya kumwani na kumpa mikoba yote.

  wasiogope watu wapya ambao damu zao bado zinachemka ambaye hawezi kulala nyumbani wakati shirika liko taabani, unampa mtu ambaye hata kama shirika linakufa hajari unafikiri litafika wapi.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  Wanapigana vikumbo wakati ceo mtarajiwa -mattaka ametulia anakula juice na mrija wake pale opp na ppf kazi kwelikweli....wasichinje albino tu ndi sala zetu kugombania cheo
   
Loading...