Nianzeje kumwambia mke wangu kuwa nimezaa nje?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,906
mimi ni mwanaume wa miaka 35 sasa, nilioa miaka 4 iliyopita, kisha nikaghaflika nikazaa na mwanamke mmoja baada ya mke wangu tu kujifungua.

Sasa mwanamke huyo anataka kuolewa na anayemuoa amemwambia ni vyema akamkabidhi mtoto kwa baba yake halisi na hata kama ni
kuishi naye yuko tayari, em nisaidie njia ya kumueleza mke wangu na wadau wako maana nashindwa pa kuanzia, namhurumia mke wangu sana.

Nisaidieni
 
Tafuta mzee halafu uwatume wazazi wako wakamueleze huyo mzee, naye aende kwa wazazi wa mkeo halafu kwa pamoja waende kwa mkeo...
 
Pambana kiume kitaeleweka tu hakuna kinachoshindikana. Washirikishe wazazi wako kwanza then wao watajua namna ya kufanya kumweka sawa. Haya mambo yapo toka zamani hakuna jipya wala hujainvent kitu kipya
 
nimejitolea kuwa mshenga wakati akitoa maelezo yaliyonyooka kwa mkewe haki ya mola nimewavulia baadhi ya wanaume kofia yaani mke kajifungua mume anaenda kugawa dushelele nje.

hahahahhahaha. Alighafilika
 
nimejitolea kuwa mshenga wakati akitoa maelezo yaliyonyooka kwa mkewe haki ya mola nimewavulia baadhi ya wanaume kofia yaani mke kajifungua mume anaenda kugawa dushelele nje.

we acha tu, unaweza usitamani kuolewa kama mambo yenyewe ndio haya.
Unaishi na mumeo ukidhani familia aliyonayo ni hiyo tu kumbe mwenzio anafamilia kama 5 nje mambo yakishaharibika bi mkubwa ndio unakuja kutupiwa watoto ambao hakuwategemea.
 
nimeamini kwanini kuna huu msemo "Don't take life too seriously. You'll never get out of it alive. ''
 
mimi ni mwanaume wa
miaka 35 sasa, nilioa miaka 4
iliyopita, kisha nikaghaflika nikazaa
na mwanamke mmoja baada ya
mke wangu tu kujifungua. Sasa
mwanamke huyo anataka kuolewa
na anayemuoa amemwambia ni
vyema akamkabidhi mtoto kwa
baba yake halisi na hata kama ni
kuishi naye yuko tayari, em nisaidie
njia ya kumueleza mke wangu na
wadau wako maana nashindwa pa
kuanzia, namhurumia mke wangu
sana. Nisaidien

Bujibuji
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom