wachunie wote jifanye na wewe unaumwa...hongera kwa utunzi, nasubiria mwezi hapa kibarazani
Barubaru umefuturu weye? naona kama futari inafanya kazi tumboni....anyway sikujua kama wewe ni mtunzi mzuri wa mashahiri
basi nivizuri ukaja huku Igunga ili uwasaidie ndugu zako wa cuf na ccm kwa kuimba mashahiri haya majukwaani ili kuvutia watu
Barubaru .... naona umeshiba chui la ilboru .... mzulu hajambo?
Nianze kwenda kwa nani?
- Leo nimepata simu, Huko kwangu ofisini, Zote tena taslimu, Zimefika mikononi,
Na zote hizo muhimu, Nimezisoma yakini,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
2. Simu ya kwanza yasema, Tia mguu njiani,
Mama yako ana homa, Imemuanza kondeni,
Fanya uje hima hima, Kupona si tumaini
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
3. Simu ya pili yasema, Hamza njoo Omani,
Mkweo anakoroma, Kakumbwa na datsani,
Ukweli hana uzima, Ajekupa buriani,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
4. Simu ya tatu yasema, Barubaru harahara,
Mkeo wa huko Doha, leo kaumwa na nyoka,
Waganga wanavyosema, Imebakia dakika,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
5.Simu ya nne yasema, usidharau kufika,
Mwanao Dar isalaama, Mguu umevunjika,
Homa raha alalama, Jinsi anavyoteseka,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
6. Simu ya tano yasema, kaka yako ana kesi,
Kaiba mali ya umma, Wamemzoa polisi,
Majibu ya mahakama, Uje ulipe upesi,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
7Watunzi huo ukweli, msidhani naropoka,
Zimeniruka akili, Nabaki kuweweseka,
Mwanakijiji na Ali, Choveki nipe hakika,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
Dr Hamza Yousuf Al Naamany (Barubaru)
H/N 2436, Umm hays Block.
Minal fahal Street.
Doha.
Qatar
Ndugu Fungu la nne ni lakipekee sana, Adam Hakuwa na kaka wala Mama wa aina yeyote ile lakini alikuwa na mke tu kabla ya kuwa na watoto lakini aliishi. mkeo ni sehemu ya mwili wako lazima apewe kipaumbele kuliko wote. Nenda kwa mkeo!.
Nianze kwenda kwa nani?
- Leo nimepata simu, Huko kwangu ofisini, Zote tena taslimu, Zimefika mikononi,
Na zote hizo muhimu, Nimezisoma yakini,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
2. Mama yako ana homa, Imemuanza kondeni, namba moja muwahi mama, tena atakupa ukweli ni yupi baba yako aliekuzaa.
3. Mkweo anakoroma, Kakumbwa na datsani, wasiliana na mkuu wa dini mahali pale waanze kutoa huduma ya kiroho.
4. Mkeo wa huko Doha, leo kaumwa na nyoka, namba mbili piga simu kwa daktari wake ili utume pesa haraka imtibie.
5.Mwanao Dar isalaama, Mguu umevunjika, piga simu kwa rafiki yako wa dar amuwahishe kijana hospital
6.Kaiba mali ya umma, Wamemzoa polisi, wasiliana na wakili wako awahi kabla hawakamsweka lupango.
wasalaam.

nenda kwa mama.......hakuna anayeweza kuziba pengo la mama......hakuna spare ya mama......

nakuja kwako eid.....niandalie biriani
Nianze kwenda kwa nani?
- Leo nimepata simu, Huko kwangu ofisini, Zote tena taslimu, Zimefika mikononi,
Na zote hizo muhimu, Nimezisoma yakini,
Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.
2. Mama yako ana homa, Imemuanza kondeni, namba moja muwahi mama, tena atakupa ukweli ni yupi baba yako aliekuzaa.
3. Mkweo anakoroma, Kakumbwa na datsani, wasiliana na mkuu wa dini mahali pale waanze kutoa huduma ya kiroho.
4. Mkeo wa huko Doha, leo kaumwa na nyoka, namba mbili piga simu kwa daktari wake ili utume pesa haraka imtibie.
5.Mwanao Dar isalaama, Mguu umevunjika, piga simu kwa rafiki yako wa dar amuwahishe kijana hospital
6.Kaiba mali ya umma, Wamemzoa polisi, wasiliana na wakili wako awahi kabla hawakamsweka lupango.
wasalaam.
Nimeipenda sana. Ahsantum kwa ushauri wako

Nenda kwa mama kwani hakuna kama mama.Mkwe ni mama wa kukopa! At anytime mnaweza kuwa watu mnaofahamiana tu baada ya kuachana na mwanae.Mama mzazi ana radhi zako hata mbele za Mungu,pia kumbuka pepe inapatikana kwa wazazi hivyo haraka nenda kwa mama.