Nyetk
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,648
- 1,701
Wakuu naona mida ya maakuli ndo hiyo. Waswahili husema ukimchunguza sasa kuku anavyotaga hilo yai utashindwa kulila; au kwa kifupi siri ya mtungi aijuaye kata. Kila mmoja anajua anakopata msosi hasa wa mchana. Hapa ofisini kwetu kuna mjasiliamali mmoja wa kisasa huwa anatuletea kwa gari na hilo pekee yake pamoja na vyombo anavyotumia vinatupa matumaini kuwa "standard" ya mlo wetu yumkini ni wa kiwango. Lakini hakuna anayefahamu mazingira chakula hicho kinapotayarishiwa.
Nawatakia mlo mwema; ila naomba kila mmoja aniambie ukweli; leo lunch unakula/umekula wapi?
Nawatakia mlo mwema; ila naomba kila mmoja aniambie ukweli; leo lunch unakula/umekula wapi?
