Niachie Mchungaji wangu

kitororondo

JF-Expert Member
Jan 17, 2018
598
699
Soma yote

Tunaishi Taifa huru, kila mtu anauhuru wa kuabudu anachotaka, ni Taifa ambalo hakuna sheria wala sharia ya kuwaua wasiomcha Mungu. Ni Taifa huru kwa wapagani na wachamungu pia, lakini naona kuna matumizi mabaya ya uhuru.

Kuna makundi ya watu ambayo yananajaribu kuingilia uhuru wa wengine na kuwapangia cha kufanya wakati kinachofanywa huku hakiwaathiri chochote.

Narudia tena, kila mtu ana uhuru wa kuamini anachokiamini na kuabudu anachoabudu, basi UCHAGUZI wangu pia uheshimiwe. Ni rahisi kwako kumtukana Mchungaji wangu na kumuita tapeli, ananiibia, anatafuta hela kwa sababu wewe una mfumo mwingine wa kuendesha maisha yako katika masuala ya Imani.

Kama ambavyo wewe ukipata changamoto unaenda kwa mganga, na unaamini katika hilo, na mimi nikipata changamoto naenda kwa Mchungaji wangu. Kama ambavyo wewe ukiwa na msongo unakunywa pombe kutuliza mawazo na kupata amani, na mimi pia nikiwa na msongo nikienda kwenye maombi narudi niko sawa kabisa.

Kwa jinsi hiyo hiyo unayotaka maamuzi yako yaheshimiwe, na mimi pia natamani maamuzi yangu yaheshimiwe. Jinsi ambavyo unaona mimi kutoa sadaka natapeliwa, na mimi pia naona kumpa mganga pesa ni kutapeliwa, kwa maana kama angekuwa na nguvu ya kutoa UTAJIRI si angeanza kutajirika yeye!

Basi niachie Mchungaji wangu, sijakopa hela yako kutoa sadaka wala mbegu, sijatumia mwili wako kwenda kukaa kanisani unakoona napotezewa muda. Kama najisumbua ni maisha yangu. By the way, Imani iko moyoni, na ndio inayonipa matokeo.

Hayo hayo unayoyadharau, ndio yanayonipa matokeo, na kila kitu kina umuhimu wake, tajiri mwenye machimbo ya madini anamuhitaji mama muuza mboga ili kupata mboga kwa urahisi kulinda afya yake.

Usidharau kitu cha mtu, usikebehi Imani ya mtu. AMINI unachoamini na mimi niamini ninachokiamini. Tafadhali sana usimtukane Mchungaji wangu mbele yangu!

-Apostle Nick Shaboka Jr.
#Heshima_ni_kitu_cha_bure
#Tuheshimiane
#Uhuru_wa_kuabudu
 
Back
Top Bottom