Ni zipi Faida za kwenda JKT?

Ni zipi Faida za kwenda JKT?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,613
Nimejaribu mno kujaribu kuelewa faida za watu waende kujiunga JKT SIJAZIONA. Na nimejaribu sana kuona faida za wabunge nao kujiunga na mafunzo ya JKT sijaona!

Wanasema eti wanafundishwa uzalendo? Seriously? Uzalendo unafundishwa JKT kwa miezi hiyo michache?

Binafsi naona hasara kwa Taifa:

Kwanza pesa za walipa kodi zinazotumika, Pili JKT ni PIKNIKI tu fulani kwani nionavyo mimi haina tofauti na watoto wa shule ya msingi na skauti.

Sanasana kuna hatari ya kuandaa majambazi kwa kupitia hayo mafunzo! Watu watakuwa majasiri while hawana ajira so watajikuta wana skillz za kufanyia ujambazi na kwa wabunge wanachopata ni cheap publicity tu as if wamefanya la maana saana; ni ujinga mtupu....
 
Haki na usawa vitafanya tuipende nchi yetu bila kwata la JKT.

Kama jeshi lingekuwa ni funzo la uzalendo tusingesikia huko siasa wala ufisadi!

Waste of time! very sorry!
 
Nadhani faida ni kukamua vitambi na kusafisha damu zilizojaa tusker lite!!
 
Serikali ina pesa za mchezo. Wange2mia tht money kuslv the prob's zilizopo nchini. UZALENDO HUO UPI?? Buree! Bado cjaona faida ya jeshi cjui hw thy cn convince me...
 
SAM_3536.JPG

Mama Maria Nyerere akiongoza wanamgambo wenzake wakati wa kufunga mafunzo ya mgambo katika viwanja vya Ikulu DSM mwaka 1973.Hii leo inawezekana?​

c4.jpg
Kama enzi zile inawezekana leo?
 
Wakati wafanikazi wa Tanzania hawajalipwa mshahara wa mwezi february serikali ya magamba inahadaa na jkt. hii mijitu kweli ni mitaahira, bila kufanya tathmini ya mafanikio au athari za mipango ya jkt kwa kipindi cha nyuma, inakurupuka tena kurudia utumbo. Hakuna mahali popote pale ambapo wawezapata taarifa kuhusu manufaa ya jkt kwa taifa au kundi la watu au mtu binafsi. Huu ni upuuzi mwingine katika nchi yetu.
 
Kwa upande wangu naona haina faida yoyote. Kama ni uzalendo mbona wanaotorosha raslimali za nchi walienda JKT? Sioni faida hata moja. Kwa kipindi hiki ambacho maambukizi ya HIV ni makubwa sijui itakuwaje huko JKT?

.......

Hi ni kweli kabisa, kwani mwenye kiti wa chama naye si ni mwanajeshi? aliyekua katibu mkuu wa magamba nae je,si alikuaga na cheo cha kutosha tu huko jeshini?

Vipi mzee Mboma, or sorry, nilitaka kumsahau huyu, mzee wa weka mbali na Tembo, hivi nae huyu si alikuaga mjeshi? Nakubaliana na mleta uzi pamoja na wewe, JKT ni upotezaji wa fedha tu!
 
Kama jeshi lingekuwa ni mahali pa kujifunza uzalendo, tusingesikia hivi karibuni kwamba jeshi la Tanzania linanuka rushwa kwa kufanya mambo yao kwa usiri, pia tusingesikia kashfa ya meremeta.

Nakubaliana na mleta mada kwamba JKT ni upotezaji wa fedha za walipa kodi.
 
Hamna kitu, kama zaidi ni kung'atwa na chawa tu na kuzoea mazingira machafu sana. Uzinzi njenje, upende usipende hasa kwa mabinti. Labda wakati Israel alipoanzisha lilikuwa na maana. Lakini mazingira niliyopita wakati wangu duhhh. Zoezi langu la Karate lilikuwa bora kuliko hiyo JKT.
 
ndio mwisho wa kufikir wa gambaz au?
 
Kwa upande wangu naona haina faida yoyote. Kama ni uzalendo mbona wanaotorosha raslimali za nchi walienda JKT? Sioni faida hata moja. Kwa kipindi hiki ambacho maambukizi ya HIV ni makubwa sijui itakuwaje huko JKT?
Mkuu unamaanisha nini unapohusisha maswala ya jeshi na maambukizi ya UKIMWI.?
 
Masomo ya uzalendo ya fundishwe shuleni kuanzia msingi. Hao wanaofundisha wenyewe hawana elimu ya uraia.isitoshe mafisadi wengi walikuwa wanajeshi lowassa.kinana kikwete mkuchika mboma shimbo hawa wote ni mafisadi papa na walikuwa wanajeshi.
 
Nimejaribu mno kujaribu kuelewa faida za watu waende kujiunga JKT SIJAZIONA. Na nimejaribu sana kuona faida za wabunge nao kujiunga na mafunzo ya JKT sijaona!

Wanasema eti wanafundishwa uzalendo? Seriously? Uzalendo unafundishwa JKT kwa miezi hiyo michache?

Binafsi naona hasara kwa Taifa:

Kwanza pesa za walipa kodi zinazotumika, Pili JKT ni PIKNIKI tu fulani kwani nionavyo mimi haina tofauti na watoto wa shule ya msingi na skauti.

Sanasana kuna hatari ya kuandaa majambazi kwa kupitia hayo mafunzo! Watu watakuwa majasiri while hawana ajira so watajikuta wana skillz za kufanyia ujambazi na kwa wabunge wanachopata ni cheap publicity tu as if wamefanya la maana saana; ni ujinga mtupu....
Nakiri kwamba faida ya JKT hii mpya kwa wabunge hata mimi sioni. Kwa nielewavyo JKT ni Sehemu ambapo vijana hujifunza
  • Nidhamu
  • Uvumilivu
  • Ukakamavu
  • Umoja
  • Uzalendo/utaifa
  • Kujitegemea
  • Heshima kwa watu bila kujali tabaka la kiuchumi
 
nafikiri lengo la mwalim those days ilikuwa kutengeza umoja wa kitaifa, vijana kuwa pamoja kwa mwaka mmoja bila kuulizana dini wala kabila ilikuwa kitu muhimu sana ambapo leo matunda yake tunayaona.

Kwa sasa hata mimi sidhani jeshi hili lina manufaa, cha msingi pesa hizi zingetumika kununulia madawa hasa kwa kinamama wanaojifungua, vituo vya watoto yatima nk

Haya yote yanajitokeza sababu as a nation hatuna priorities, mtu akishapata cheo cha uongozi tu anaibuka ya mambo yake anayoona yeye ni ya msingi. hili ni tatizo.
 
Nakiri kwamba faida ya JKT hii mpya kwa wabunge hata mimi sioni. Kwa nielewavyo JKT ni Sehemu ambapo vijana hujifunza
  • Nidhamu
  • Uvumilivu
  • Ukakamavu
  • Umoja
  • Uzalendo/utaifa
  • Kujitegemea
  • Heshima kwa watu bila kujali tabaka la kiuchumi

hapo juu umelist vizuri faida za kijana aliye pitia JKT anatakiwa kuwa,hizi issues za ufisadi na kukosa uzalendo kwa baadhi ya watu waliopita JKT isiwe kigezo cha kuhukumu maelfu ya Watanzania waliopita mafunzo hayo kwamba kwamba siyo wazalendo,ni kupoteza muda na rasilimali za nchi. Kwa maoni yangu JKT ni muhimu zaidi sasa kama sehemu ya kuwaunganisha vijana wa Tanzania ambao wametenganishwa ktk matabaka elimu,shule za kata na academy. Ningependa hata itengenezwe programu maalum kwa watumishi wa serikali,taasisi na mashirika ya umma ambao hawakupitia mafunzo haya,wapelekwe huko sasa! Inaweza ikawa ni programu ya miezi mitatu kwa intake.
 
Back
Top Bottom