Ni yapi madhara ya kuwapa wanajeshi vyeo vya kisiasa?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Kuna wakati Ccm iliamua kwamba makada wake wenye vyeo vya kijeshi waviweke kando na watumie majina yao halisi,kuna kipindi Ccm ilikuwa ni kama chama kinachoongozwa na wanajeshi

Mfano mzuri ni kipindi cha JK,Makamba na chiligati.

Baadae waliamua kutotumia vyeo vya kijeshi kama utambulisho.

Hili lilikuwa na mantiki.
Sasa naona kasi ya kuwaingiza wanajeshi katika vyeo vya kisiasa inakuwa sana.
Je hili halina athari yeyote kwa jeshi na taifa?

Mipaka ya kuwaingiza ipo ?vigezo gani hufuatwa na mashauriano gani hufanyika?
 
Tatizo katiba ya Ccm mkuu wa wilaya ni kada wa chama na mkulu kasema MTU hawezi kuwa na Nazi mbilimbili
 
Kwa sasa pengine hatuwezi kuona madhara hadi miaka mitano hivi. Ila sikuona mantiki ya kuingiza jeshi kwenye siasa na siasa kwenye jeshi
 
Mtamuelewa tu JPM baada ya miaka 10.

Hebu chunguza na ujue hao wajeda wote wamepelekwa wapi? Yaani Wilaya zipi?

Hawa wote wamepelekwa Wilaya zinazopakana na Nchi jirani kama ilivyokuwa kwa wakuu wa Mikoa ya mipakani.

Huo ni uteuzi wa kimkakati zaidi na sio wa kikada. Na hawa wanaendelea kuwa wajeda na hata pale wakifanya makosa na kuondolewa ukuu wa Wilaya wanarudi jeshini.

Mambo mengine tuyaache tu, ni ya kimkakati zaidi na mimi naona yuko sahihi. Hebu angalia sasa hivi silaha zilivyozagaa, zinatokea wapi?
 
Urahisi wa kutumika kisiasa kwa manufaa ya wanasiasa hasa walio madarakani....
 
Wee mleta thread bhana Rais wa Nigeria alikuwa Mwanajeshi angalia huko nchini kwake sa hvi anavyo lala sambamba na wahujumu uchumi! Hapa kwetu kupewa vyeo mim sioni kama kutakuwa na madhara yoyote isitoshe tena watakuwa ni wazalendo!
 
Wee mleta thread bhana Rais wa Nigeria alikuwa Mwanajeshi angalia huko nchini kwake sa hvi anavyo lala sambamba na wahujumu uchumi! Hapa kwetu kupewa vyeo mim sioni kama kutakuwa na madhara yoyote isitoshe tena watakuwa ni wazalendo!

Tatizo ujue mkuu hapa nchini kwetu kila kitu kinaangaliwa kisiasa siasa kwanza kisha mambo mengine yanafuata. Unachosema ni kweli kabisa. Na inabidi tubalike kidogo kimtazamo, tuepuke kuwa mitizamo ya kisiasa zaidi. Ns hapa ukiangalia, ni kwa nini hawa wajeshi hawajapangiwa Dar au Dodoma, kwa nini wote wamepelekwa mipakani.?
 
Kwa hiyo kwa sasa ndani ya vikao vya kamati za siasa za mikoa na wilaya za ccm zitakuwa na wajumbe Ma meja generali, makanali na makepteni wa jeshi kwa vyeo vyao.
Basi ni haki kwa wanajeshi wengine kuwa wanachama wa vyama vingine na kupewa vyeo? Mfano Gen Mwamunyange akawa Chadema na kupewa ujumbe wa Kamati kuu? Kuwa DC au RC na ukawa mjumbe wa kamati ya siasa wilaya au mkoa maana yake tayari ni mwanachama wa ccm sasa wanajeshi wana vyama?
Hili jambo ni zito ingawa linachukuliwa kwa uzito mdogo, utawazuiaje wengine ndani ya jeshi kujiunga kwa uwazi na vyama vya siasa wakati wengine mumewapeleka ndani ya chama?
 
1467348985697.jpg
 
Tatizo katiba ya Ccm mkuu wa wilaya ni kada wa chama na mkulu kasema MTU hawezi kuwa na Nazi mbilimbili
Kada ni yule aliyemwanachama wa ccm. Asiyemwanachama haingii kwenye vikao vya ccm kwenye eneo lake la utawala mkoa au wilaya. Hawa wanajeshi ni askari na uteuzi ukibatilishwa wanarudi kazini kwao na huko waliko wataendelea kupanda vyeo vyao vya kijeshi.
 
Back
Top Bottom