Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,335
- 72,799
Mwenye uelewa mpana wa maamuzi ya Mkuu na kamati yake atusaidie hapa. Mkuu jana akihitimisha ripoti ya pili ya Makanikia ametuaminisha kuwa ACACIA ni wezi wakubwa, wanafanya biashara kinyume cha sharia kwani hawajasajiliwa hapa nchini na waongo wakubwa.
Lakini kinacho shangaza ni kuwa kilichozuiwa ni kusafirisha mchanga tuu, ila uchimbaji, uchakataji na usafirishaji wa dhahabu uko palepale kwa hawa watu wanaofanya shughuli kinyume cha sharia bila kusajiliwa. Matumaini ya wengi yalikuwa shughuli zao ambazo hazipo kisheria baada ya kugundulika zingesimamishwa ile ile jana, sasa kulikoni?
Sasa hao wakina Chenge na wenzake tutawaita wa nini kuwahoji wakati wezi na wasiopo kisheria bado tupo nao? Mie naona kama drama Fulani hivi na kama kawaida tunalishwa matango pori na malengo ya kiki za kisiasa yametimia na hali kubaki ile ile.