Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,474
- 4,007
Wana JF,
Kuna haja ya kutenda mema siku zote ili kuandaa maisha yetu ya badae, ukitenda mema usiweke kichwani songa mbele wema wako usikupe kiburi cha kwenda unasema na kutaja wema kwa wengine unaharibu. Tenda wema nenda zako.
Niseme kwamba mtu yeyote aliyeko kwenye ofisi yoyote ile ikiwemo na na watoa huduma wote lazima awajibike kuwa mwema kwa wengine na sio kuwakandamiza na kuwaonea. Kuna haja ya kutenda mema bila ya kuangalia huyu nani na huyu nani, kila mtu ana haki ya kupewa chochote kile ambacho kinamfaa, hakuna kisipolipwa hapa duniani, MISALA, MATATIZO, SHIDA, vyote vile vinavyo tutokea katika maisha yetu tuwe na muda wa kutafakari mara mbili KWANINI HILI LIMENITOKEA na KWANINI MIMI lazima utapata jibu aidha umetendwa kwa kuonewa au ni kosa ulilolifanya ila umesahau na usipopata jibu basi subiri.
Ukitendewa na mtu kwakuwa anataka akukomoe bila sababu basi ipo siku yake tu, hatakimbia labda AJE AKUOMBE MSAMAHA ndio itakuwa pona yake si vinginevyo. Kila unapomtenda mtu au kumfanyia kitu kibaya ni rahisi kusahau, na ukipokea kwa mabaya uliyoyatenda lazima utasahau tu hutakumbuka utakachofanya ni kwenda kuwaona waganga wakusaidie na penginepo mwisho wa siku unapewa vitu vya kuishi navyo au kutembea nacho ili usaidiwe kuendelea kuishi.
Huu ni ushauri wangu kwenu acheni wenye roho za kuwatendea watu mabaya waendelee, kama umetenda mema usinagalie nyuma kuhusu malipo songambele, Baraka za mwenyezi Mungu utakazo kutana nazo utasahau kuwa uliwahi kutenda mema na ndio malipo yake hayo, ukipokea hizo Baraka usizitumia vibaya na usitumie kwa uwanyanyasa wengine au kuwa na chuki na wengine vinginevyo utanyanganywa.
Wito huu nautoa kwa wote au wengi dunia nzima watakao bahatika kusoma kwamba WAACHE KUWATENDEA WENGINE MABAYA cheo chako, ofisi yako na mamlaka uliyo nayo isikuagize uwatendee watu mabaya chondechonde, utavuna tu HAIKWEPEKI NA HUTAKWEPA KAMWE.
Kila mwenye tatizo, mkasa na anayepitia maisha magumu na yenye utata akae chini awe na muda mzuri lazima atapata jibu kujua ni wapi alikokosea, na kama kuna mtu kakufanyia ili akukomoe kaa karibu na mwenyezi Mungu akusaidie upone au utoke huko uliko. Ila MUOMBE MWENYEZI MUNGU AKUELEKEZE NA AKUONYESHE NI WAPI ULIPOKOSEA kama kuna mtu uliyomkosea nenda kwake au tuma ujumbe kuomba AKUSAMEHE si vinginevyo. Vifo vibaya vinawakuta wengi kwakuwa wanayo yasiri waliyoyafanya na hawawezi kusema, mateso ya magonjwa kwa muda mrefu na mengineyo yanawaacha wengine na ulemavu wa kudumu au wa muda. LAZIMA TUTAFAKARI KUJUA NI WAPI TULIPOKOSEA NA NI NANI TULIYEMKOSEA basi si vinginevyo.
Wasalaam.