Mkuu huko ulikojikita kutafuta mafanikio ya serikali kwenye maendeleo ya wananchi siko. Ukitaka kutafuta mafanikio ya serikali yetu jikite kwenye Esrow, epa, richmond na maufisadi ya namna mbalimbali yanayofanywa na viongozi.
Na research yako wewe ni kuhudhuria mikutano yao. Kule utakuta wanajisifu mambo ya majoka yenye makengeza, hela za mboga nk.
Ukitaka kutafuta serikali ilikoshindwa 100% ndo ujikite kwenye hizo mada zako 6.
Mapya yaibuka sakata la Escrow.
http://www.globalnewztz.com/2015/05/mapya-yaibuka-sakata-la-escrow.html
Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed.
Kashfa ya Escrow imeibuliwa upya bungeni baada ya wabunge kudai kuna kampuni ya Simba Trust inayomiliki asilimia 50 za kampuni ya Pan Africa Power (PAP), ambayo inadaiwa kuhusika katika ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Hayo yaliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba yake ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2015/2016 ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Msemaji wa kambi hiyo, Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, alisema wakati umma wa Watanzania unataka kuelewa wamiliki wa kampuni ya Simba Trust lakini katika hali ya kushangaza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), umegoma kutoa majina ya wamiliki wa kampuni hiyo.
"Kambi rasmi ya upinzani tunaitaka serikali ieleze kwanini taasisi hii ya Brela iliyo chini ya wizara hii bado inakataa kutoa majina ya wamiliki wa Simba Trust, imekuwa kama ilivyokuwa makampuni yaliyohusika na uchotaji mabilioni ya Epa na fedha za mradi wa Meremeta," alisema.
Mnyaa alisema hatua ya Brela kukataa kutoa majina ya wamiliki wa kampuni hiyo kuna unganisha na dhana kwamba wamiliki wa kampuni hiyo ni viongozi wandamizi wa serikali ya CCM.
Alisema matatizo ya kiutawala yaliyopo katika sekta ya umma nchini yamesababisha sekta ya viwanda kushindwa kujiendesha kiushindani.
Aliongeza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), limebainisha kuwa viwanda vingi vinaendeshwa kwa hasara kutokana na kuwapo kwa gharama kubwa za uzalishaji, tija ndogo, riba kubwa za kibenki,tatizo la umeme na urasimu.