Ni wapi kwa Dar es Salaam mizani inapatikana?

baiser

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
1,487
Reaction score
2,261
Habar ndugu wana jf.hivi kwa dar mizani inapatikana wapi kwa wingi na kwa bei gani.na nitatambuaje ubora wa mzani na kama umepigwa chapa ya Wakala wa vipimo?
 
Nenda Kariakoo sokoni ndani kwenye lile jengo kuna mizani ya kila aina. Ipo ambayo imethibitishwa na ambayo haijathibitishwa. Iliyothibitishwa inakuwa na stika ya mwaka husika imebandikwa.
 
Ahsanteee sticker inasomekajee
 
Ile stika lazima ionyeshe alama ya Vema au tiki kwenye mwezi iliofanyiwa service na mwaka pia, na sio kila mzani unaouzwa madukani umehakikiwa na WMA- weight and measure agency. Ukisha ununua waweza pia kuwapelekea kwenye ofisi zilizo karibu nawe kwa garama ya elfu Kumi tuu. Kumbuka mzani kila mwaka lazima uhakikiwe na hao jamaa. Natumai umenisoma
 
Nenda mitaa ya Kisutu afuu tambaa na ile Morogoro road kuna maduka mengi ambayo ya asili ya biashara hiyo
 
Ile stika lazima ionyeshe alama ya Vema au tiki kwenye mwezi iliofanyiwa service na mwaka pia, na sio kila mzani unaouzwa madukani umehakikiwa na WMA- weight and measure agency. Ukisha ununua waweza pia kuwapelekea kwenye ofisi zilizo karibu nawe kwa garama ya elfu Kumi tuu. Kumbuka mzani kila mwaka lazima uhakikiwe na hao jamaa. Natumai umenisoma

Katika watu wanaokula mshahara bure ni hawa WMA, nashangaa zaidi ya kupima ujazo/uzito na kukagua mzani/ machine za ujazo baada ya hapo muda mwingi utawakuta wamekaa ofisini wakisoma magazeti tu wakati mtaani kwenye masoko yetu mizani karibu zote zimechezewa hasa kwenye mabucha ya nyama
 
Mkuu labda huna bahati ya kukutana nao... Lkn wanajitahidi kukagua mpk viwandani zinakotoka bidhaa... Ukienda pale Ofisi zao za Ilala utawaona kila siku asubuhi wanatoka na gari zao kwenda site! Kuhusu mizani ya butcher na madukani huwa wanaelimisha wananchi kuwa hakikisha kabla hujapimiwa kitu mzani umekaa balanced! Pia wanafanya calibration ya mita za Maji hata kwa ww mwananchi wa kawaida na ukibahatika pita pale Ofisi ya Misugusugu uone calibration za malori zinavofanyika!
 
Kuna mdau kasema nenda Kariakoo sokoni! Wale jamaa watakuanzia bei 170,000+ kwa Mzani wa mawe, usiogope... Ongea nao mpk 140-150k! Unachukua! Kuna mzani wa digits ule bei inafika 200,000! Huu unahitaji maintanance ya Mara kwa Mara!
Habar ndugu wana jf.hivi kwa dar mizani inapatikana wapi kwa wingi na kwa bei gani.na nitatambuaje ubora wa mzani na kama umepigwa chapa ya Wakala wa vipimo?
 
Habar ndugu wana jf.hivi kwa dar mizani inapatikana wapi kwa wingi na kwa bei gani.na nitatambuaje ubora wa mzani na kama umepigwa chapa ya Wakala wa vipimo?
Pia mkuu unaweza kuwa-check jamaa wanajiita Wintech kwa namba hizi 0767914991 ni wauzaji wa Mizani sina zote, maana hapa hatujakuuliza unataka mzani wa aina gani! Hapo utapata Mizani ya kila aina! Wapigie wakuelekeze ofisi zao zilipo!
 
Mkuu labda huna bahati ya kukutana nao... Lkn wanajitahidi kukagua mpk viwandani zinakotoka bidhaa... Ukienda pale Ofisi zao za Ilala utawaona kila siku asubuhi wanatoka na gari zao kwenda site! Kuhusu mizani ya butcher na madukani huwa wanaelimisha wananchi kuwa hakikisha kabla hujapimiwa kitu mzani umekaa balanced! Pia wanafanya calibration ya mita za Maji hata kwa ww mwananchi wa kawaida na ukibahatika pita pale Ofisi ya Misugusugu uone calibration za malori zinavofanyika!

Kukagua viwandani ni sawa tu kama kazi hiyo inafanywa kila siku na kutoa ripoti zilizosahihi lakini hapo hapo tujiulize je kazi za TBS naye anafanya nini? kuhusu kutoa elimu mimi binafsi sijaona mahali wakiitoa hiyo elimu mtaani zaidi ya kutikisa mizani, kufutafuta vumbi na kurekebisha kidogo then unawalipa chao hapo ndio mmeachana mpaka mwakani, ukienda kwenye vituo vya mafuta ni vivyo hivyo na kuwa mwangalifu nao kwani wengi wanaenda field kutafuta kipato haramu tu, Pale Misugusugu sawa pana kazi ina fanyika pale lakini hebu tuangalie hili kwa mapana ya kitaifa je kuna umuhimu wa kuwa na Agency kama hii wakati wanaweza kufutiliwa mbali na kuwa watumishi wa Mkurugenzi mahala husika? Hebu jaribu kwenda ofisi zao za mikoani ndio utajifunza mengi mkuu
 
kama unataka mizani halisi na nzuri japo bei zao ziko juu
nenda mizani tanzania
pale stendi ya mwendkasi kisutu
 
Hao jamaa ni waharibifu TU wa mizani.
Yaani mzani ukishawapelekea wakaufungua ndo ushakufa.

Back
Top Bottom