Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,372
- 81,814
Kichwa cha habari kinajieleza. Wenzetu Azam fc wameamua kufikia muafaka kwa kuachana na mwalimu wao kipenzi Ettiene Ndairagije, na hivyo kumkabidhi timu mwalimu mpya raia wa Romania.
Sababu ya kufanya hivyo ni moja tu, timu isimamiwe na mwalimu kwa muda wote na siyo kama ilivyokuwa imejitokeza siku za katikati, mara mwalimu yuko na timu ya Taifa, mara Azam! Maana jambo hilo linaweza kuleta athari kwa upande mmoja au pande zote! Na kuna usemi usemao mshika mawili, moja humponyoka.
Ukija kwenye timu ya Yanga, mambo ni yale yale kama ya Ndairagije! Mwinyi Zahera ni mwalimu wa timu ya Yanga, na wakati huo ni Mwalimu msaidizi wa timu ya Taifa ya DRC! Mara nyingi amekuwa akiiacha timu na kwenda kuwajibika kwenye timu yake ya Taifa, na hivyo kumuachia majukumu mwalimu msaidizi Noel Mwandila.
Je, viongozi wa Yanga hawaoni athari zozote za kuendelea na mwalimu mwenye majukumu mawili kwa wakati mmoja? Kwa nini wasiangalie namna ya kuwa na mwalimu wa kudumu na asiyeshikamana na upande mwingine kwa wakati mmoja?
Kama Zahera anaipenda sana Yanga, kwa nini asijiuzulu na yeye kuifundisha timu ya Taifa kama alivyofanya kocha mwenzake mkuu na anayeifundisha klabu ya As Vita, (somebody Ibengwe) ili ahamishie nguvu zote kwenye klabu yake ya Yanga?