Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,243
Wiki iliyopita nilipita mahali na mtoto wa kike wa "Class mate" wangu, jamaa zangu waliniuliza kama "natoka" naye, nilishangaa sana. Kweli binti yuko mwaka wa tatu Chuo Kikuu na kwa umbile lake anaonekana ni "mkubwa" lakini haiondoi kwamba ni sawa na mtoto wangu kwani mama yake ndiyo tulikuwa tunakaa naye dawati moja, zama zilee!!
Tukio lile limenifanya nijiulize ni wakati gani hasa mwanaume anatakiwa aonekane amezeeka kujihusisha na mahusiano mapya. Maana kama Binti yule ndiyo angekuwa mama yake anapita na mwanangu bila shaka watu wangemuuliza "huyo ni mwanao?" kwa nini kwangu watu wawaze kwa umri huu naweza kuwa na mpenzi kama binti yule?
Inawezekana Mama wa miaka zaidi ya hamsini kuwa na uhusiano na mvulana wa miaka 25 na jamii ikaona sawa? Kama si sawa kwa nini iwe sawa kwa mwanaume, au ni wakati gani tunaweza kusema sasa huyu mwanaume amezeeka na hatakiwi kujihusisha na mahusiano mapya na watu walio chini ya umri wake? Ni sawa kwa mwanaume kuwa na mahusiano na mtu waliyepishana naye zaidi ya miaka 25 au 30?