Ni wakati gani maisha yaliacha kuwa magumu?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,850
32,060
Habari za jioni wana JF

Nikiwa nimeshikilia balimi yangu inayotoka jasho (unyevu nyevu) natafakari majaaliwa ya mwanadamu. Ni kawaida kusikia watu wakisema maisha sasa yamekuwa magumu. Kwa msemo huo nimewaza kiundani na kujiuliza ni lini maisha ya mwanadamu yamewahi kuwa rahisi?

Ninachokiona mimi maisha ya mwanadamu hayajawahi kuwa rahisi. Wanadamu kwa utofauti wao wanakabiliwa na madhila tofauti tofauti. Mathalani mtu mwenye pesa anaweza akawa ana maradhi au akapatwa na madhila ambayo yakamfanya asione thamani ya pesa yake, hali kadhalika mtu hoe hae naye akataabika kutafuta pesa ili kumudu mahitaji yake ya kila siku.

Kimsingi, maisha ni mtihani, tena mtihani mgumu kweli kweli. Hakuna kipindi ambacho mwanadamu anaweza akajinasibu kwamba maisha ni rahisi. Ila la uhakika ni kwamba vipo vipindi katika maisha yetu tunjisahau na kufurahia kile tulicho nacho na kuyapa kisogo matatizo yanayotuzunguka. Huu ndiyo ule wakati tunadhani maisha ni rahisi. shabash balimi imeisha na nasaha zimeisha. alamsiki
 
Kweli hakuna siku maisha yalikuwa marahisi au yatakuja kuwa marahisi....Ukitaka kuamini linganisha awamu ya nne na ya 5 utaona.
 
Awamu ya II ya Mzee Ruksa
Maisha hayakuwa rahisi, ila alitutoa kutoka uchumi wa ujamaa akatupeleka wa ubepari. Awali watu walikua na hela vitu havipo ila wakati wa mzee ruksa vitu vilianza kuingia na watu wakaanza kuvifurahia wakapata unafuu kwa wakati fulani
 
Kwa hiyo zile ahadi za mara... "maisha bora"..au.. "kureta maendereo ya viwanda vya vyerehani"...huwa tunabugizwa viepe vikavu kinywaji mate yako?
 
Maisha yatakuwa magumu mpaka pale tutakapoacha kujilinganisha na wengine na kufurahia alichotujaalia Mungu huku tukifanya kazi kwa bidiii tukitumainia makubwa
 
Back
Top Bottom