Shozylin
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 298
- 607
Yanga ni timu bora hapa Tanzania kwa sasa, wala hili halina ubishi. Tusiwabeze Yanga eti tu kwasababu hakupata magoli mengi yaliyomuwezesha kushinda baadhi ya michuano.
Tuanze na rekodi ya kimataifa, tukiwatoa Zalan FC:
~ Yanga dhidi ya Al-Hilal: Yanga walimiliki mpira kwa umiliki wa juu kuliko Al-Hilal.
~ Yanga dhidi ya Club Africain: Bado Yanga walimiliki mpira umiliki wa juu kuliko Africain kwa mechi ya nyumbani na ugenini.
Tukija ligi za ndani, kiuhalisia anayefuata kwa ubora nyuma ya Yanga ni Simba na Azam, sasa tuangalie wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Yanga dhidi ya Simba na ubora wao.
Fikiria wewe unamiliki timu (X) na upo sokoni kununua wachezaji hawa, utamnunua nani kulingana na ubora wake pamoja na uzoefu (hapa acha ushabiki)?
Beki
~ Namba 2: Israel Mwenda dhidi ya Djuma Shaban.
Kiungo
~ Namba 6: Kanoute dhidi ya Bangala.
~ Namba 8: Mzamiru dhidi ya Aucho.
~ Namba 9: Kibu Denis dhidi ya Fiston Mayele.
Kwa upande wangu mimi kulingana na namba pamoja na uzoefu wa wachezaji hapo juu nitawachukua waliyo upande wa Yanga.
Na huo ndiyo ukweli, hakuna mchezaji niliyemtaja hapo juu anayemzidi ubora mchezaji wa Yanga, ukibisha njoo na rekodi zao wote.
Wakati huo jiulize, mara ya mwisho timu yako kuifunga Yanga ilikua mwaka gani? Una muda gani hujaifunga yanga? Kwanini hujaifunga?
Msianze kuongea ugoro mkaonekana ni mashabiki maandazi/mihogo. Ukweli ni kwamba Yanga anaugusa mwingi, hii inatokana na aina ya wachezaji aliyonao.
Wakati huo Simba mpinzani wa Yanga hakua na Kocha wa Mazoezi kwa muda mrefu. Kocha Mkuu walisema wamemuazima kutoka Coastal Union ila baadaye Coastal walikanusha kuwa hawakuwa na mkataba naye. Wakati huo huo pia walikuwa wameazima Kocha wa Magolikipa.
Kama tu timu ina benchi la ufundi la namna hii itajilinganishaje na timu yenye benchi la ufundi bora? Kinacho itafuna Simba nadhani sasa mmekielewa.
Siamini kweye bahasha.