Ni vitu gani kiongozi afanye ili aheshimiwe?

Ni vitu gani kiongozi afanye ili aheshimiwe?

Marco Seth

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2022
Posts
4,680
Reaction score
5,653
Viongozi wengi wanakuwa wanachukiwa. Ni namna gani abadilike ili watu wamkubali na aheshimiwe?
 
Kiongozi yeyote yule ukitaka uheshimiwe, hakikisha umelisoma somo la ETHICS na kuliishi kwa vitendo.
 
Akipenda inakuaje?
Akipenda sana kuheshimiwa anaweza kutengeneza habari za uongo ili watu wamuheshimu tu, bila ya ukweli heshima haina maana.

Anaweza kulazimisha kila mtu akisema maneno machache amtaje na kumsifia. Anaweza kulazimisha kuweka mabango yenye picha yake nchi nzima bila ya tija.

Mfano, jibu zuri la swali lako linaweza kuwa, ili kiongozi aheshimiwe, anatakiwa kuwaambia watu maneno ambayo yatawafanya wamuheshimu.

Vipi kama maneno hayo ni ya uongo?

Haya, hata tukiondoka kwenye uongo. Vipi kama kiongozi atafanya mambo ambayo yatafanya watu wamuheshinu, lakini kiukweli mambo yale ni ya kijinga?

Vipi kama watu wanaheshimu magwanda ya jeshi, na kiongozi akaamua kuvaa magwanda ya jeshi, akapewa heshima kwa sababu hiyo, wakati kwenye kufanya kazi, kulinda haki, uhuru na uhai kazembea?

98hqoxlj5gkd1.jpeg
 
Kiongozi aheshimike, asijitenge na uhalisia wa anaowaongoza, awe sehemu ya anaowaongoza.

Mf;
1. Kama unapita kwa msafara kukwepa foleni, basi hakikisha changamoto ya foleni inakomeshwa.

2. Kama unakomba pesa za kibubu kwenda kuazimisha mila za kijijini kwenu, usiwafukuze wengine kutoka kwenye vijiji vyao vya asili.

3. Usitunishe misuli ya kuazima kisa, hutaki kusikia ukweli

Mifano ni mingi ila, huwezi kuwa kiongozi wa Simba kama wewe Chura.
 
Kweli
Akipenda sana kuheshimiwa anaweza kutengeneza habari za uongo ili watu wamuheshimu tu, bila ya ukweli heshima haina maana.

Mfano, jibu zuri la swali lako linaweza kuwa, ili kiongozi aheshiniwe, anatakiwa kuwaambia watu maneno ambayo yatawafanya wamuheshimu.

Vipi kama maneno hayo ni ya uongo?
 
Viongozi wengi wanakuwa wanachukiwa. Ni namna gani abadilike ili watu wamkubali na aheshimiwe?
Asijione yeye ni alfa na omega kwenye nchi! Ajishushe na kuelewa haja za wananchi wake bila upendeleo kwa matajiri na kuwasahau masikini ambao sauti zao ni ndogo na.hazizingatiwi! Samia kama unasoma hapa onesha upendo kwa wananchi wenye kuhitaji faraja kutoka kwako. Aache kuwa sikiliza chawa kama kina tlatlaah na lucas mshamba!🙄
 
Back
Top Bottom