Wanawake wamepewa uwezo wa kuwaelewa wanaume tena kwa haraka hata pale mnapokutana kwa Mara ya kwanza tuu! Kabla hujaonyesha au kutamka neno, mwanamke huwa tayari amejua na huwa anasubiria muda ufike ujilete mwenyewe.
Mwanamke mwenye miaka 20 huwaza na kufanya sawa na mwanamume wa miaka 40 au zaidi! Ni ajabu kwamba dunia inawaona wanawake kama viumbe wanyonge na wasio na akili, kinyume chake ndio ukweli.
Kuna wakati wanawake hufanya maamuzi magumu yasiyo na maelezo kwetu wanaume! Fikiri kuna wakati mwanamke huamua kuolewa sii kwa sababu amempenda mwanamume bali kwa kubeba jukumu kubwa kijamii.
Tuna mifano lukuki hata kwenye biblia ambapo Ester aliolewa na mfamle Astanasta sii kwakumpenda Bali kwa ajili ya ukombozi wa Taifa lake yaani wayahudi.
Jiulize ni wanawake wangapi ambao wanaishi kwenye ndoa lkn kile kilichomleta ktk ndoa ni jukumu zito kama kuiokoa familia yao iliyo kwenye shida nk.
Juzi tuu nimemtembelea mwanamke ambaye nilisoma naye shule ya msingi miaka ya 1980, tulipendana sana na hata tulipomaliza form four bado tulikuwa pamoja! Wazazi wake hali zao ki!maisha ilikuwa mbaya na hawakunipenda kwakuwa na Mimi ni mlala hoi. Binti huyu baadaye aliolewa na MTU mwingine mwenye uwezo japo moyo wake upo kwangu hadi Leo.
Ninachoweza kusema nikwamba maisha aliyo nayo Leo nisingeweza kumpa, kwakuolewa na kibosile yule amepata kila kitu na wazazi wanaishi vema!
Naanza kuwaelewa wanawake kwa mbali!
Je wewe unawaelewa wanawake vema?
Tujuze!!