Ni vigumu sana kufanya maandamano kwa mpango wa GenZ, vyombo vya usalama vimedhibiti njia za mawasiliano na wafanya "Phone Tracking" kukamata watu

Ni vigumu sana kufanya maandamano kwa mpango wa GenZ, vyombo vya usalama vimedhibiti njia za mawasiliano na wafanya "Phone Tracking" kukamata watu

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,630
Reaction score
25,586
Nimeeleza kwenye moja ya mada za Britannica namna vyombo vya usalama vinavyofuatilia na kuteka watu wasipatikane kwa muda au hadi uchaguzi utakapokamilika. Mimi soma profile yangu nipo kama mchambuzi fulani hivi lakini baada ya kuona mambo fulani hivi imebidi niingie in details kuongea na Gen Z ili niwape moja mbili za kuwa uanaharakati wa kidijitali.

Kuna sehemu ntaingia more technical lakini mtanielewa naomba mnivumulie ndo mambo yalivyo wakutana na "somehow expert opinion".

Gen Z wamekuwa nyuma ya muda katika kufanya matayarisho na wamekosa stratejia ya namna ya kuandaa maandamano kama vile ilivyokuwa hivi karibuni katika nchi za Nepal na Madagascar, kwani maofisa usalama wa Tanzania walikwenda hatua tatu mbele kwa kuwahi kudhibiti njia za mawasiliano.

Hivyo inakuwa vigumu kutumia Tik-Tok, Facebook na X ambazo sasa zipo chini ya uangalizi maalum wa TCRA na hata huyu msichana aliekamatwa juzi aitwae Frida alitumia Tik-Tok ambayo imefanyiwa "phone tracking" hadi alipokamatwa.

Tokea mwanzo kulitakiwa kuwe na stratejia kwamba zipo njia tatu za mafanikio katika mitandao hii mitatu ambayo imetumika kifasaha kule Nepal na Madagascar. Njia ya kwanza ni majadiliano (Discussion) kupitia Discord ambapo katika majadiliano hayo huja mpango au "planning" ambapo coordinator anaanda vijana ambao tiyari kitambo walitakiwa wawe wamejiandaa kwa ajili ya siku hiyo au "D Day".

Discord yasisitiza kwenye kupanga au planning, kujadili au "debate" na kuandaa au organise katika muda huo yaani Real -Time and Live Stream Events", njia ya kukwepa udhibiti au bypass censorship ili kuweza kuingia barabarani kwa wakati mmoja.

Pia maandamano kukosa "Context" au sababu za msingi za kuandamana na kuleta vurugu, hii ni muhimu kwani Context ni tofauti katika kila nchi na kwa kwetu itawawia ugumu waandamanaji kwani tiyari raisi kasema yeye ni Amiri Jeshi Mkuu akimaanisha kuwa vyombo vyote vya usalama vimepewa nyenzo zote na zana kwa ajili ya kukabiliana na yeyote ataekwenda kuandamana na si kupiga kura.

Naomba nieleweke nikisema kukosa "Context" yaani mazingira yote, mawazo na mipango inopelekea kuwepo maandamano na hayo mazingira yakaeleweka yote kwa umakini. Hii ya kukosa "Context" imepelekea maandalizi ya maandamano haya kukosa support hata ya jumuiya ya kimataifa ambayo hadi sasa haijatoa kauli yoyote ile ya kuuliza au kuhoji hali ya utekaji na ukandamizaji inofanywa na vyombo vya usalama nchini.

Gen Z kukosa uwezo wa fedha na kutegemea VNP na bure nalo ni tatizo kwani VPN za bure hazina usalama wa uhakika na zipo wazi kwa ajili ya kuingiliwa na wataalam ambao wapo TCRA wanoweza kufanya "hacking" na "penetration" ili kuweza kuingilia mawasiliano na mitandao ya kijamii.

Kuzimwa kwa mitandao siku ya uchaguzi au kuwa limited kwa watu wachache tu itakuwa ni vigumu ka Gen Z kufanya matayarisho yoyote na mawasiliano baina yao. Mitandao ya Tik-Tok, Facebook na X yote ipo chini ya TCRA kwa ajili ya ufuatiliaji au "surveillance".

Watu/Jamii na vyombo vya habari.

Watanzania wengi wamekuwa katika hali ya kuamini kuwa amani iliyopo ndo hiyohiyo inowapa kula. Halikadhalika vyombo vya habari vimeacha majukumu yake mawili katika majukumu matatu yaani kuelmisha na kuhabarisha jamii na kubakia kufanya jukumu moja tu la kuhabarisha tena habari za upande mmoja tu.

Kwa mfano vyombo vya habari vikieleza tu kwamba fulani kakamatwa na polisi au leo Tundu Lissu kafikishwa mahakamani na kujaza mapicha, lakini vyashindwa kuleta vichwa vya habari za watu kutekwa. Kwahiyo habari zikiwa ni fulani kakamatwa au Tundu Lissu leo Kisutu habari zile zaogofya kwa umma au jamii itakayosoma na hovyo kuingiwa tiyari na hofu.

Kutokana na hayo ujumbe wa "October Tunatiki" umeingia kwenye jamii na pia miji mingi sasa hivi nchini ina ina mapicha kila kona ya mgombea mmoja tu ambae ndiye atarajiwa kushinda uchaguzi wa October na hivyo ndo jamii inavyoaminishwa.

Sasa ni nyenzo zipi ni muhimu kuzitumia katika kuandaa kufanya maandamano?

Katika mazingira magumu yalowekwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudhibiti mitandao ya kijamii nyenzo pekee ambao zitatoa ulinzi na kufanya mawasiliano yawe salama ni zile ziitwazo Advance Cryptographic technology. Ingawa wamechelewa sana, Gen Z waweza kutumia njia za Signal na Tor ambazo zasaidia kuweza kutumia internet kufanya browsing na pia kuandaa shughuli za maandamano kwa usalama zaidi. Hii itafaa zaidi kwa baadae ikiwa hali ya October 29 itakuwa kama inavyokusudiwa.

Sina uhakika kama ntaeleweka lakini hali ndivyo ilivyo na nipo hapa Dodoma mjini naona mitandao imeanza kusumbua na hapa Dodoma Hoteli pana watu wengi sana wapitapita tu lakini hawanunui hata kahawa wala kashata wang'aang'aa macho tu.

Vijana wa GenZ wale "tech savvy" kazi kwenu wekeni mambo sawa nimewapa dondoo muhimu.
 
Gen z wanakosa mbinu kidogo wanatumia mitandao ila wanajisahau padogo sana kudanganyika, ukuamua kufanya harakati za mtandaoni acc unayotakiwa kutumia hakikisha haina connection na mtu yoyote wala detail zako fanya harakati ukiwa off logout
 
Na waliyo Nyumbu watu wawili tu wanakuja kumteka mmoja wao alafu wao wako kama 50 ila hawawezi hata kumtetea mwenzao wanajificha kwa mbali wanachungulia huku wanawasha data ili wapige mikwara mtandaoni
 
Gen z wanakosa mbinu kidogo wanatumia mitandao ila wanajisahau padogo sana kudanganyika, ukuamua kufanya harakati za mtandaoni acc unayotakiwa kutumia hakikisha haina connection na mtu yoyote wala detail zako fanya harakati ukiwa off logout
Labda utumie device ambayo unaitumia kwa harakati tu usiwahi kuwasiliana na mtu hata mmoja kupitia hicho kifaa
 
Halafu what's the psychology behind mtu ambaye ameamua hatoandamana lakini kutwa kuongelea maandamano na waandamanaji? Like mna matatizo gani? ? ? Embu jichunguzeni.
Wapi kasema hataandamana? Ndo maana mi nawaita Nyumbu.
 
Sasa kufuatilia kila Gen Z ni time consuming, na ukizingatia wapo sehemu tofauti tofauti, tatizo hivi sasa kila kona watu wanatoa sauti za maandamano, kwa siku zilizobaki hao wafuatiliaji/hackers na hivyo vikosi vya utekaji wana kazi ya ziada. Plus 29 Oct ni kesho kutwa.
 
Tuahirishe maandamano ya AMANI kutoka tarehe 29/10 mpaka siku ya kuapishwa kwa Samia kwasababu ujumbe wetu ni ule ule kuwa uchaguzi huu haukua HURU na wa HAKI.

Wadau mnasemaje?
 
Na waliyo Nyumbu watu wawili tu wanakuja kumteka mmoja wao alafu wao wako kama 50 ila hawawezi hata kumtetea mwenzao wanajificha kwa mbali wanachungulia huku wanawasha data ili wapige mikwara mtandaoni

Kama watu ni wajinga hivo basi wawe wanakuja mchana
 
Back
Top Bottom