Ni utapeli gani mkubwa ulishawahi kufanyiwa tujifunze kitu

Hilo begi ni chambo tu cha wewe kununua bidhaa zao, na hata hizo nguo zao zinakuwa hazina ubora wa bei anayouza. Yaani ununue nguo za elfu kumi upewe begi la elfu arobaini au hamsini. We ulisikia wapi..?
 
Hilo begi ni chambo tu cha wewe kununua bidhaa zao, na hata hizo nguo zao zinakuwa hazina ubora wa bei anayouza. Yaani ununue nguo za elfu kumi upewe begi la elfu arobaini au hamsini. We ulisikia wapi..?
Ndio maana nikasema walikuwa wanavutia wajinga tuu wanunue.

Na sisi hatukulijua hilo mpaka jamaa alipokuja kutuambia kwamba huwa hawatoi hilo begi,wanatangaza tuu kuwa ni Ofa ila, Hamna Kitu .
 

Wazee wa "tupo Mtendeni Zanzibar" 😂😂

Watu wamepigwa sanaaaa
 
Dah karata tatu sitakuja kusahu huu mchezo na jamaa aliyekuwa anachezasha naikumbuka sura yake japo karibu miaka 20 sasa Hela ya mtaji yote ilipotelea pale maeneo ya mwananyamala hospital
Ilikuwaje mkuu? Funguka
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kisa chako na kinafanana na changu pia kina fanana na cha mtoa mada ....ilikuwa 2011 Buguruni pale nimeshuka kwenye gari jamaa anajifanya kapagawa kama kapoteza na mwenzie akanifata kama ww yahn iyo mbinu yao yahn

Sema me nilishtuka jamaa muonekano wake sio wa kuokota hela hafu anifate tugawane.
 
Nikiwa Darasa la 6 nilienda Mnada mmoja Hivi na UTOTO wangu nikaenda Kuangalia Ile michezo ya Karata na Vibunda vya Viberiti wakivichanganya halafu unabahatisha wapi sahihi. Ss Jamaa Walivyo matapeli wakaniambia Tunakupa Mtaji Dogo Ucheze bure.

Jamaa mmoja akaniambia Haya Bahatisha Hela natoa mimi. Si nikaona Kiberiti chenye Pesa nikaki-point sasa Kumbe ni mtego tu. Wakaniambia Ss. Dogo ongeza Pesa yako uliyonayo maana Ile ilikuwa nimekuwekea mimi tu.

Kumbe wakati wananiongelesha Hivyo Pale chini washabadilisha kile Kiberiti wameweka Kingine. Ss naangaika Kutoa buku 2 yangu mfukoni ili niweke pale kwenye kile Kiberiti cha Kwanza nilicho point. Wakaniuliza Uli point wapi mara ya Kwanza? Nikawaambia Pale.

Haya weka pesa yako, nikaweka buku 2.. Wakafunua Holaaaa nikaliwa kizembe sana na Nilivyokuwa mdogo hata Kupigana Sikuweza nikatembea zangu Maana Nauli walishaila
 
Huku kuna wa design hiyohiyo

Anakuambia kitenge cha elfu ishirini na tano dukani nakupa kwa elfu kumi sasa wapenda mteremko wanakimbilia ukitoa tu hela umeliwa unakuta ni vile vitenge vya kama kuteleza flani halafu vinauzwaga elfu tano kama sikosei.

Pia kuna muda wanauza na kutangaza ofa ya mabegi au chochote kama nyongeza kumbe ndio michezo yao wanapeana wengine mnapigwa. Hua nikikutana na vitu kama hivyo napita kama vile sioni mana unaweza simama ukajikuta victim.
Nikikutana na mtu simjui ananichangamkia huwa wala sisemeshani naye namuangalia tu hasa nikijua nimetembea na hela nyingi yasijenikuta bure.

Kuna wale matapeli nasikia wakikusemesha tu ukawajibu hata kama ni salamu umeenda na maji japo sijui kama ni kweli au story tu za vijiweni.
 
Stori ya mtoa mada na Scars iliwahi nitokea nikiwa naenda kidato cha 3 katikati ya miaka ya 2000's.

Ilikua hivi; Nimetoka zangu melini ndani ya MV Victoria naelekea stand kufika mitaa ya makoroboi nikakutana na hao wapuuzi, staili ni hiyo hiyo ya kudondosha. Ile jamaa kadondosha kanifata kanipiga Bega oya mzee tukagawane mzigo huu jamaa kaangusha, kuangalia ndani ya bahasa kuna risiti imeandikwa Sh. Laki tatu malipo kwa ajili ya jezi za JWTZ.

Sasa na akili zangu za kianafunzi nikasema yes hapa ndio pa kuongeza pocket money. Jamaa akaniseti tukapita kule relini nyamagana kwa chini kama unaenda ziwani, na mida ile asubuhi kila mtu yuko busy kuwahi kibaruani kwake.

Sasa ile tumefika tu relini chini karibu na ziwani, mara wakaibuka jamaa kama 8 hivi wanatuambia wao ni maaskari na tuko chini ya ulinzi tukitoroka tu wanatupigia filimbi. Tukaulizwa hela zikowapi, jamaa akasema hizi hapa akaulizwa kulikuwa na risiti ipo wapi akaasema tumeitupa njiani na ni kweli alitupa nikaona.

Jamaa wakasema kusanyeni kila kitu hapa, nikaweka kimotorola changu na pocket money 50,000 na begi la vitabu na begi la nguo, halafu wakaamuru nifate ile risiti, sasa ile nimetembea tu kama mita 5 naona jamaa kila mtu anasepa kivyake na mizigo yangu ndio akili ikarudi inaniambia we mshenzi ushaibiwa embu anza kupiga mwano.

Piga mwano wapi masela washapandisha Sahara na wengine ziwani na kila mtu yupo na time yake, wakupiga mabango wanapiga tu mabango dogo Acha tamaa. Ikawa ndio hivyo na safari ya shule ikabidi iishie pale kwanza.
 
Dah
 
Akijua umemshtukia tu utaskia unashangaa nn? Anakua mkali
 
Kuna siku nilkua nanunua nguo za kuuza pale Boma Kuna jama hata sielewi nilijikwaa vipi na kuniambia dogo mbona unanikwaa?

Nikamwambia samahani ile kufika mbele najiangalia mfukoni hata mia Sina.

Nikagungua wale jamaa hua wanakua kikundi cha hata watu 4 wanavyotembea hawakuachi salama.
 
Waliwahi kuja na gia ya kusema wana mgonjwa wanamtafuta dr special.
 
Huu mchezo wa kurushiwa kibunda cha pesa....😞

Bwana tapeli alirusha kifurushi nikajua kweli mtu kadondosha pale juu kuna risiti kwamba zile ni pesa za kununua sare za mgambo, akaniambia sista shhhh usiseme twende tukagawane, kwani hapo umebeba nini nikamjibu maziwa napeleka pale akasema okay nenda halafu uje tugawane...

Nilikimbia chap nikarudi pale chocho namtafuta tapeli tugawane hela za mgambo 🙄
 
Dodoma hiyo mjtqa ya majengo jamaa kategesha kasimu kqje njiani mjda ya saa mbili usiku,ile kupita tu akaipiga ikawa inawaka taa,fqster niaokota jamaa akatokeq eti njoo tuione kuna mtu kaidondosha,aliona vumbi mbwa yule,nikasepa na simu
 
Aisee
 
Nilituma laki mbili kwa watu wa kukopesha fedha taslimu ama dhamana ya kukopesha milioni mbili ile tu nimeituma hiyo lakimbili nikablkiwa kwenye kundi la Facebook na kwenye namba ya simu niliyowasiliana nao ndipo nikapata akili kuwa nimetapeliwa.


Dedication.
Wale wanaosema tunakopesha fedha taslimu huko Facebook na kukutaka ufanye friend request nipo muanze mawasiliano ya namna ya kufanikisha mkopo wako Mara baada ya kuwatumua Amana ya asilimia flani ya mkopo unaoutaka ujue unaandaliwa mazingira ya kutapeliwa.

Huwa najicheka Sana nikikukumbuka namna nimetapeliwa kizembe namna ile tu kwakuwa nilikuwa nahitaji hiyo 2m Ili niboost kabiashara kangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…