Ni utapeli gani mkubwa ulishawahi kufanyiwa tujifunze kitu

Mwezi huu huu wiki iliyopita nilikuwa na jamaa yangu mmoja hivi ni mgeni wa jiji , sasa nilikuwa namtafutia sehemu za nguo za mitumba.

Tukapita pale Ilala Boma Kwenye ule ukuta wa TBL ambao kuna njia ya vumbi kuelekea Mchikichini. Sasa pale hua kuna Jamaa anafanya mnada wake Kwenye kijukwaa kidogo hivi , ambacho kakizungushia kitambaa kwenye hilo jukwaa lake , kiasi kwamba hata bidhaa alizo kuwa nazo huwezi ata kuziona.

Sasa mimi na jamaa yangu tukaona ngoja tumsikilize huyo jamaa wa mnada hapo, maana alikuwa ananadi nguo kisha kuna baadhi ya muda anatangaza kutoa ofa ya begi buree kwa atakaye nunua baadhi ya Nguo zake.

Jamaa wa mnada alitoa Pensi na Flana kisha akasema , Ofa kwa atakaye nunua hizo atapata na Begi , na hakika yale mabegi baadhi yalikuwa mapya kabisaa , basi jamaa yangu akanyoosha mkono ,yule jamaa akamrushia hizo nguo bila hata kumpa begi, kisha anakuwa na mkusanyaji hela wake anakusanya hizo hela .

Mara ya pili tena yule muuza nguo akatoa tena Flana 2 kisha akasema bei ni 10000 na begi la bure, sisi tukachukua tena bila hata kupewa lile begi .

Kumbe pale Kwenye ule Mnada pale hua kuna watu wengine wanakuwepo pale ambao ni kikundi kimoja na hao wapiga mnada, na hao kazi yao kubwa ni kupokea Ofa ya begi kisha wanaenda Kwenye mabanda ya pembeni wnaakusanya kishawanayarudisha tena, na wana sheria zao ukigombania begi na wenzako basi wanalichukua wao kwa maana kuwa hamtakiwi kugombania.

Tumekuja kushtukia jamaa kashatoa 15000 na bila hata begi kupata . Kumbe pale wanawatapeli tuu watakaokuja kununua kwa kisingizio cha kusema ni Ofa ya begi, ila mabegi wakitoa Ofa wanawapa watu wao pale pale kisha wanarudisha Kwenye kile kijukwaa . Na kuna wengine wamewekwa ili kugombea hilo begi ili mteja asipate na wapokonywe wote.

Huo mchezo tumekuja kuushtukia baada ya Jamaa mmoja kuniambia kwamba huyo mwenzio hapo anaibiwa na wala hapati begi.Dohhh hapo jamaa alichoka sana mana kanjnua nguo na yeye shida apate hilo begi na wala hakupata .Na ndio mchezo wao kila siku Huo na Mpaka leo bado wapo pale.
Hilo begi ni chambo tu cha wewe kununua bidhaa zao, na hata hizo nguo zao zinakuwa hazina ubora wa bei anayouza. Yaani ununue nguo za elfu kumi upewe begi la elfu arobaini au hamsini. We ulisikia wapi..?
 
Ndio maana nikasema walikuwa wanavutia wajinga tuu wanunue.

Na sisi hatukulijua hilo mpaka jamaa alipokuja kutuambia kwamba huwa hawatoi hilo begi,wanatangaza tuu kuwa ni Ofa ila, Hamna Kitu .
 
Duh pole sana........me nakumbuka last year nliingia Instagram nkakutana na account moja inaitwa Zanzibar electronics og......wanauza vitu bei rahisi sana Kuna kitu nikawa nmeagiza kwa laki tatu na 50... Nkatoa pesa yote.......Hadi leo sijapata mzigo angu....na badae nliona mdada mmja famous anaitwa Tunda anamtangaza huyo jamaa tapeli.....nkajikaza tu Mungu akanibariki nkapata ka ela kengine zaid ya hako nlikotapeliwa

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app

Wazee wa "tupo Mtendeni Zanzibar" 😂😂

Watu wamepigwa sanaaaa
 
Utapeli wa dzaini hiyo niliwahi kukutana nao ila sikuwapa nafasi hivyo ikafanya nisielewe wanatekelezaje lengo

Kuna siku nilikuwa naenda kununua material ya ujenzi wa nyumba, nikatoka na laki 8

Nilipofika road wakati naelekea hayo maeneo kulikuwa na watu nyomi wakisubiri magari yapungue wavuke upande wapili

Tulikuwa watu wengi sana eneo hilo tukisubiria magari yasimame tuweze kupita, ghafla nikamuona mchizi akitembea kwa speed na kuangalia angalia chini huku akionesha kuchanganyikiwa

Watu wengi tulimtazama kwasababu sura yake tu ilionesha amepoteza kitu chenye thamani sana.

Wakati tunaendelea kumshangaa huyo mchizi, kuna msela akanigonga bega na kuninong'oneza kwa sauti ya chini kuwa "oyaa mwanangu skia huyo mwana anayetembea kapoteza bahasha ambayo ndani yake ina hela"

Halafu akanionesha hiyo bahasha ikiwa imefungwa (hakuifungua nione kilichomo ndani yake)

Akaniambia unajua wewe ni nwanaume mwenzangu na hii ni rizki imeniangukia sasa sio mchongo kuwa mlafi kwa hiyo mwanangu sizi kikauzu usimstue ili hii pesa tukagawane mimi na wewe

Nikamjibu ok kwa hilo fresh mwanangu nimekusoma nakuahidi ntakuwa na utulivu kama wa kupe kwenye ngozi ya ng'ombe

Basi magari yakapungua na watu wakawa wanaanza kuvuka, ile naanza tu kuvuka mchizi akanidaka shati...nikauliza vipi?

Akasema kwani tumekubalianaje? Nikamuambia si ni makubaliano yetu kuwa hizo pesa tunaenda kugawana au umebadili gia?

Akasema ndio tunagawana sasa mbona unaondoka, nikamjibu hapa mazingira sio rafiki maana mchizi anaweza kusanuka kwa hiyo twende maeneo ya pale (nikamnyooshea kidole kwenye kituo kidogo cha polisi ambacho kilikuwa jirani)

Mchizi alivyoona mamwela wako nje na doka lime pack kushoto akasema basi nimeghairi hii pesa naichukua mwenyewe, nikasema fresh kama umeamua hivyo...nikawa nasepa

Akanifuata tena oya kwa hiyo mchizi ndio umekaza kabisa ina maana hutaki mgao?

Wakati huo macho yake yote hayabanduki kwenye mfuko wangu wa suruali ambao ulituna kutokana na zile hela nilizoweka

Nikamuambia fresh mwanangu kiroho safi nimeamua nikuachoe hizo pesa ujigawie mwenyewe sina kinyongo wala nini...jamaa akaondoka huku akisema utazikumbuka hizi pesa shauri yako

Sasa nimefika mbali nikageuka nyuma nikamuona yule mchizi aliyejidai kapagawa kwa kupoteza bahasha ya pesa wakiwa wanajadiliana na yule aliyekuwa ananishawishi tugawane zile pesa
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kisa chako na kinafanana na changu pia kina fanana na cha mtoa mada ....ilikuwa 2011 Buguruni pale nimeshuka kwenye gari jamaa anajifanya kapagawa kama kapoteza na mwenzie akanifata kama ww yahn iyo mbinu yao yahn

Sema me nilishtuka jamaa muonekano wake sio wa kuokota hela hafu anifate tugawane.
 
Nikiwa Darasa la 6 nilienda Mnada mmoja Hivi na UTOTO wangu nikaenda Kuangalia Ile michezo ya Karata na Vibunda vya Viberiti wakivichanganya halafu unabahatisha wapi sahihi. Ss Jamaa Walivyo matapeli wakaniambia Tunakupa Mtaji Dogo Ucheze bure.

Jamaa mmoja akaniambia Haya Bahatisha Hela natoa mimi. Si nikaona Kiberiti chenye Pesa nikaki-point sasa Kumbe ni mtego tu. Wakaniambia Ss. Dogo ongeza Pesa yako uliyonayo maana Ile ilikuwa nimekuwekea mimi tu.

Kumbe wakati wananiongelesha Hivyo Pale chini washabadilisha kile Kiberiti wameweka Kingine. Ss naangaika Kutoa buku 2 yangu mfukoni ili niweke pale kwenye kile Kiberiti cha Kwanza nilicho point. Wakaniuliza Uli point wapi mara ya Kwanza? Nikawaambia Pale.

Haya weka pesa yako, nikaweka buku 2.. Wakafunua Holaaaa nikaliwa kizembe sana na Nilivyokuwa mdogo hata Kupigana Sikuweza nikatembea zangu Maana Nauli walishaila
 
Mwezi huu huu wiki iliyopita nilikuwa na jamaa yangu mmoja hivi ni mgeni wa jiji , sasa nilikuwa namtafutia sehemu za nguo za mitumba.

Tukapita pale Ilala Boma Kwenye ule ukuta wa TBL ambao kuna njia ya vumbi kuelekea Mchikichini. Sasa pale hua kuna Jamaa anafanya mnada wake Kwenye kijukwaa kidogo hivi , ambacho kakizungushia kitambaa kwenye hilo jukwaa lake , kiasi kwamba hata bidhaa alizo kuwa nazo huwezi ata kuziona.

Sasa mimi na jamaa yangu tukaona ngoja tumsikilize huyo jamaa wa mnada hapo, maana alikuwa ananadi nguo kisha kuna baadhi ya muda anatangaza kutoa ofa ya begi buree kwa atakaye nunua baadhi ya Nguo zake.

Jamaa wa mnada alitoa Pensi na Flana kisha akasema , Ofa kwa atakaye nunua hizo atapata na Begi , na hakika yale mabegi baadhi yalikuwa mapya kabisaa , basi jamaa yangu akanyoosha mkono ,yule jamaa akamrushia hizo nguo bila hata kumpa begi, kisha anakuwa na mkusanyaji hela wake anakusanya hizo hela .

Mara ya pili tena yule muuza nguo akatoa tena Flana 2 kisha akasema bei ni 10000 na begi la bure, sisi tukachukua tena bila hata kupewa lile begi .

Kumbe pale Kwenye ule Mnada pale hua kuna watu wengine wanakuwepo pale ambao ni kikundi kimoja na hao wapiga mnada, na hao kazi yao kubwa ni kupokea Ofa ya begi kisha wanaenda Kwenye mabanda ya pembeni wnaakusanya kishawanayarudisha tena, na wana sheria zao ukigombania begi na wenzako basi wanalichukua wao kwa maana kuwa hamtakiwi kugombania.

Tumekuja kushtukia jamaa kashatoa 15000 na bila hata begi kupata . Kumbe pale wanawatapeli tuu watakaokuja kununua kwa kisingizio cha kusema ni Ofa ya begi, ila mabegi wakitoa Ofa wanawapa watu wao pale pale kisha wanarudisha Kwenye kile kijukwaa . Na kuna wengine wamewekwa ili kugombea hilo begi ili mteja asipate na wapokonywe wote.

Huo mchezo tumekuja kuushtukia baada ya Jamaa mmoja kuniambia kwamba huyo mwenzio hapo anaibiwa na wala hapati begi.Dohhh hapo jamaa alichoka sana mana kanjnua nguo na yeye shida apate hilo begi na wala hakupata .Na ndio mchezo wao kila siku Huo na Mpaka leo bado wapo pale.
Huku kuna wa design hiyohiyo

Anakuambia kitenge cha elfu ishirini na tano dukani nakupa kwa elfu kumi sasa wapenda mteremko wanakimbilia ukitoa tu hela umeliwa unakuta ni vile vitenge vya kama kuteleza flani halafu vinauzwaga elfu tano kama sikosei.

Pia kuna muda wanauza na kutangaza ofa ya mabegi au chochote kama nyongeza kumbe ndio michezo yao wanapeana wengine mnapigwa. Hua nikikutana na vitu kama hivyo napita kama vile sioni mana unaweza simama ukajikuta victim.
Nikikutana na mtu simjui ananichangamkia huwa wala sisemeshani naye namuangalia tu hasa nikijua nimetembea na hela nyingi yasijenikuta bure.

Kuna wale matapeli nasikia wakikusemesha tu ukawajibu hata kama ni salamu umeenda na maji japo sijui kama ni kweli au story tu za vijiweni.
 
Stori ya mtoa mada na Scars iliwahi nitokea nikiwa naenda kidato cha 3 katikati ya miaka ya 2000's.

Ilikua hivi; Nimetoka zangu melini ndani ya MV Victoria naelekea stand kufika mitaa ya makoroboi nikakutana na hao wapuuzi, staili ni hiyo hiyo ya kudondosha. Ile jamaa kadondosha kanifata kanipiga Bega oya mzee tukagawane mzigo huu jamaa kaangusha, kuangalia ndani ya bahasa kuna risiti imeandikwa Sh. Laki tatu malipo kwa ajili ya jezi za JWTZ.

Sasa na akili zangu za kianafunzi nikasema yes hapa ndio pa kuongeza pocket money. Jamaa akaniseti tukapita kule relini nyamagana kwa chini kama unaenda ziwani, na mida ile asubuhi kila mtu yuko busy kuwahi kibaruani kwake.

Sasa ile tumefika tu relini chini karibu na ziwani, mara wakaibuka jamaa kama 8 hivi wanatuambia wao ni maaskari na tuko chini ya ulinzi tukitoroka tu wanatupigia filimbi. Tukaulizwa hela zikowapi, jamaa akasema hizi hapa akaulizwa kulikuwa na risiti ipo wapi akaasema tumeitupa njiani na ni kweli alitupa nikaona.

Jamaa wakasema kusanyeni kila kitu hapa, nikaweka kimotorola changu na pocket money 50,000 na begi la vitabu na begi la nguo, halafu wakaamuru nifate ile risiti, sasa ile nimetembea tu kama mita 5 naona jamaa kila mtu anasepa kivyake na mizigo yangu ndio akili ikarudi inaniambia we mshenzi ushaibiwa embu anza kupiga mwano.

Piga mwano wapi masela washapandisha Sahara na wengine ziwani na kila mtu yupo na time yake, wakupiga mabango wanapiga tu mabango dogo Acha tamaa. Ikawa ndio hivyo na safari ya shule ikabidi iishie pale kwanza.
 
Dah
 
Huku kuna wa design hiyohiyo
Anakuambia kitenge cha elfu ishirini na tano dukani nakupa kwa elfu kumi sasa wapenda mteremko wanakimbilia ukitoa tu hela umeliwa unakuta ni vile vitenge vya kama kuteleza flani halafu vinauzwaga elfu tano kama sikosei.
Pia kuna muda wanauza na kutangaza ofa ya mabegi au chochote kama nyongeza kumbe ndio michezo yao wanapeana wengine mnapigwa.
Hua nikikutana na vitu kama hivyo napita kama vile sioni mana unaweza simama ukajikuta victim.
Nikikutana na mtu simjui ananichangamkia huwa wala sisemeshani naye namuangalia tu hasa nikijua nimetembea na hela nyingi yasijenikuta bure.
Kuna wale matapeli nasikia wakikusemesha tu ukawajibu hata kama ni salamu umeenda na maji japo sijui kama ni kweli au story tu za vijiweni.
Akijua umemshtukia tu utaskia unashangaa nn? Anakua mkali
 
Kuna siku nilkua nanunua nguo za kuuza pale Boma Kuna jama hata sielewi nilijikwaa vipi na kuniambia dogo mbona unanikwaa?

Nikamwambia samahani ile kufika mbele najiangalia mfukoni hata mia Sina.

Nikagungua wale jamaa hua wanakua kikundi cha hata watu 4 wanavyotembea hawakuachi salama.
 
Utapeli wa dzaini hiyo niliwahi kukutana nao ila sikuwapa nafasi hivyo ikafanya nisielewe wanatekelezaje lengo

Kuna siku nilikuwa naenda kununua material ya ujenzi wa nyumba, nikatoka na laki 8

Nilipofika road wakati naelekea hayo maeneo kulikuwa na watu nyomi wakisubiri magari yapungue wavuke upande wapili

Tulikuwa watu wengi sana eneo hilo tukisubiria magari yasimame tuweze kupita, ghafla nikamuona mchizi akitembea kwa speed na kuangalia angalia chini huku akionesha kuchanganyikiwa

Watu wengi tulimtazama kwasababu sura yake tu ilionesha amepoteza kitu chenye thamani sana.

Wakati tunaendelea kumshangaa huyo mchizi, kuna msela akanigonga bega na kuninong'oneza kwa sauti ya chini kuwa "oyaa mwanangu skia huyo mwana anayetembea kapoteza bahasha ambayo ndani yake ina hela"

Halafu akanionesha hiyo bahasha ikiwa imefungwa (hakuifungua nione kilichomo ndani yake)

Akaniambia unajua wewe ni nwanaume mwenzangu na hii ni rizki imeniangukia sasa sio mchongo kuwa mlafi kwa hiyo mwanangu sizi kikauzu usimstue ili hii pesa tukagawane mimi na wewe

Nikamjibu ok kwa hilo fresh mwanangu nimekusoma nakuahidi ntakuwa na utulivu kama wa kupe kwenye ngozi ya ng'ombe

Basi magari yakapungua na watu wakawa wanaanza kuvuka, ile naanza tu kuvuka mchizi akanidaka shati...nikauliza vipi?

Akasema kwani tumekubalianaje? Nikamuambia si ni makubaliano yetu kuwa hizo pesa tunaenda kugawana au umebadili gia?

Akasema ndio tunagawana sasa mbona unaondoka, nikamjibu hapa mazingira sio rafiki maana mchizi anaweza kusanuka kwa hiyo twende maeneo ya pale (nikamnyooshea kidole kwenye kituo kidogo cha polisi ambacho kilikuwa jirani)

Mchizi alivyoona mamwela wako nje na doka lime pack kushoto akasema basi nimeghairi hii pesa naichukua mwenyewe, nikasema fresh kama umeamua hivyo...nikawa nasepa

Akanifuata tena oya kwa hiyo mchizi ndio umekaza kabisa ina maana hutaki mgao?

Wakati huo macho yake yote hayabanduki kwenye mfuko wangu wa suruali ambao ulituna kutokana na zile hela nilizoweka

Nikamuambia fresh mwanangu kiroho safi nimeamua nikuachoe hizo pesa ujigawie mwenyewe sina kinyongo wala nini...jamaa akaondoka huku akisema utazikumbuka hizi pesa shauri yako

Sasa nimefika mbali nikageuka nyuma nikamuona yule mchizi aliyejidai kapagawa kwa kupoteza bahasha ya pesa wakiwa wanajadiliana na yule aliyekuwa ananishawishi tugawane zile pesa
Waliwahi kuja na gia ya kusema wana mgonjwa wanamtafuta dr special.
 
Huu mchezo wa kurushiwa kibunda cha pesa....😞

Bwana tapeli alirusha kifurushi nikajua kweli mtu kadondosha pale juu kuna risiti kwamba zile ni pesa za kununua sare za mgambo, akaniambia sista shhhh usiseme twende tukagawane, kwani hapo umebeba nini nikamjibu maziwa napeleka pale akasema okay nenda halafu uje tugawane...

Nilikimbia chap nikarudi pale chocho namtafuta tapeli tugawane hela za mgambo 🙄
 
Dodoma hiyo mjtqa ya majengo jamaa kategesha kasimu kqje njiani mjda ya saa mbili usiku,ile kupita tu akaipiga ikawa inawaka taa,fqster niaokota jamaa akatokeq eti njoo tuione kuna mtu kaidondosha,aliona vumbi mbwa yule,nikasepa na simu
 
Aisee
Natumai kila mtu alishawahi kuingizwa mjini kwa namna ambayo hatokuja kuisahau.

Pia nina amini hata uwe mjanja vipi wapo watu watakao kuzidi ujanja katika eneo ambalo huna ufahamu nalo vya kutosha.

Kisa Changu:

Kipindi kile simu zinatoka toka. Bi mdashi alininunulia simu flani hivi, sifa kubwa ya ile simu ilikuwa na mp3 (mpTHREE) ndani yake.

Kipindi iko vocha ya buku tu.Nayo ilikuwa inaitwa Dola moja. Hakukua kujiunga wala nini.

Unaweza kuplay muziki na wale wenye Nokia za tochi wakabaki wanakishangaa.

Siku moja nilikuwa nafanya safari kwenda kariakoo kununua mzigo wa familia. Tukashuka na basi katika mtaa ambayo una msongamano mkubwa sana watu. Sijatembea hatua 10 mbele, Jamaa akanishika bega uku akisema kwa sauti ya chini "Najua hunifahamu lakini tutembee kwa haraka kidogo ili nikushirikishe jambo". Nami nikatii.

Kufika mbele kidogo akaniambia noitazame nyuma ili nione kama kuna mtu yeyote anayetufuata kwa shauku. Ni kweli bhana kutazama nikaona kama kuna jamaa ambaye alikuwa alitufuata kana kwamba hana uhakika na watu anao wafuatilia.
Kumjibu ndio, akasema huyo jamaa ameibiwa pesa kwenye gari lakini hana uhakika na mtu aliye muibia. hivyo basi anatufuatilia sisi kwa nyuma ili kutaka kufahamu kama kuna muhusika kati yetu.

Nikamuuliza kwa hiyo shida yako nini, Akasema "Ni kweli nimezichukua ila hana uhakika kama ndimi ndiye niliyezichukua". Hivyo basi jamaa akatoa bahasha (Ile ya barua) ikiwa imejaa mithili ya vibunda vya pesa ndani yake. Jamaa akachana ile bahasha kwa juu nami nikaona noti moja ya buku 10 hivyo kupelekea kuamini kuwa zilizomo mule ndani zote ni noti.

Tukiwa tunaendelea kutembea huku yule wa nyuma akiendelea kutufuata kwa shauku, jamaa akashauri anipe ile bahasha yenye pesa ili tuachane kwa mbele llengo kuu ni kumpoteza maboya yule anayetufuatilia. Ila aliponikabidhi ile bahasha alisema kuwa ninaweza kukimbia na pesa la sivyo nimuachie kitu chochote cha thamani.

NDANI YA AKILI YANGU:- Yakiwa yote yanaendelea nami pia ubongo wangu ukanishauri nimpige tukio huyo jamaa. Akili ilisema jamaa akikupa kibunda na mkaachana njia basi wewe tokomea mbali na hilo eneo linaloitwa kariakoo.
Kitu cha thamani pekee ambacho nilikuwa nacho ni ile simu. Sikusita kumpatia simu kwa sababu niliona uwingi wa zile pesa ndano ya bahasha nimgeweza kununua hata simu kama zile 10. Basi nikampa huku akinisisitiza kuwa tuachane pale mbele na tukakutane roung about karibu na maduka ya kuuza simu.

Nimeisahau kidogo mitaa ya Kariakoo, kwakuwa niko nje ya mkoa kwa kipindi sasa. Lengo la kuachana ni kumpoteza maboya jamaa aliyekuwa akitufuatilia, na kweli baada ya kuachana njia jamaa wa nyuma alianza kumfuatilia jamaa niliyempa simu yangu, nami nikadhani mpango wetu umefanikiwa.

Kufika mbele kidogo nikachepuka njia tofauti na ile niliyoelewana na jamaa lengo lilikuwa kutoroka na pesa. Nikafika pahala ambapo nikaona choo cha kulipia nami nikalipa na kuingia. Humo nilikusudia kuanza kuhesabu pesa ili kufahamu ni kiasi gani.
NILIPIGWA NA BUMBUWAZI:-

Baada ya kufika nikatoa bahasha ile na kuichana, Loooooh Bahasha ilikuwa na noti moja ka Elfu KUMI na zingine zote hazikuwa noti bali ni magazeti yaliyochanwa kufuata size ya noti za buku kumi kumi. Hapo ndipo nikagundua kuwa NIMEKWISHA TAPELIWA.
Baada ya hapo nilianza kuchanganyikiwa na kuanza kukimbialia uelekeo ambao wale jamaa walielekea. Kuchanganyikiwa kwangu kulinipelekea hata kuanza kuuliza watu kuwa "WALE JAMAA WAWILI WAMEELEKEA WAPI?"

Nilihaha kama Mbwa aliye kosa maziwa ya mama yake. kariakoo nzima nilizunguka huku nikiwa na amatumaini kuwa huenda nikakutana nao kwa bahati mbaya.
Ikumbukwe kuwa Niliingia Kariakoo majira ya saa 3:45 asubuhi. lakini nilirudi home saa 12 jioni. Jambo zuri nilirudi na mzigo ambao niliagizwa ila nikakuta malalamiko kuwa kwanini nimechelewa kurudi na ilikuwaje sikuwa napatikana kwenye simu.
Nilimdanganya Bi mdashi kuwa tuliibiwa kila kitu simu pamoja na pesa za kufanya manunuzi ila kwa msaada wa Polisi tuliweza kupata pesa kutoka kwa mmoja kati ya wezi wawili walio dhaniwa, Ila yule mwizi mmoja alifanikiwa kuondoka na simu.

Mpaka leo hii sijawahi kumwambia ukweli Bi mdashi ila natumai kumwambia ukweli siku nikirudi kuonana naye. Jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba hatokuwa na kumbukumbu ya kukumbuka kama aliwahi hata kuninunulia simu ambayo nimeielezea.

TUPE KISA CHAKO.View attachment 2156223
 
Nilituma laki mbili kwa watu wa kukopesha fedha taslimu ama dhamana ya kukopesha milioni mbili ile tu nimeituma hiyo lakimbili nikablkiwa kwenye kundi la Facebook na kwenye namba ya simu niliyowasiliana nao ndipo nikapata akili kuwa nimetapeliwa.

Dedication.
Wale wanaosema tunakopesha fedha taslimu huko Facebook na kukutaka ufanye friend request nipo muanze mawasiliano ya namna ya kufanikisha mkopo wako Mara baada ya kuwatumua Amana ya asilimia flani ya mkopo unaoutaka ujue unaandaliwa mazingira ya kutapeliwa.

Huwa najicheka Sana nikikukumbuka namna nimetapeliwa kizembe namna ile tu kwakuwa nilikuwa nahitaji hiyo 2m Ili niboost kabiashara kangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom