Ni utapeli gani mkubwa ulishawahi kufanyiwa tujifunze kitu

Huu mchezo wa kurushiwa kibunda cha pesa....

Bwana tapeli alirusha kifurushi nikajua kweli mtu kadondosha pale juu kuna risiti kwamba zile ni pesa za kununua sare za mgambo, akaniambia sista shhhh usiseme twende tukagawane, kwani hapo umebeba nini nikamjibu maziwa napeleka pale akasema okay nenda halafu uje tugawane...

Nilikimbia chap nikarudi pale chocho namtafuta tapeli tugawane hela za mgambo
Hehehehehehe
 
Mwezi huu huu wiki iliyopita nilikuwa na jamaa yangu mmoja hivi ni mgeni wa jiji , sasa nilikuwa namtafutia sehemu za nguo za mitumba.

Tukapita pale Ilala Boma Kwenye ule ukuta wa TBL ambao kuna njia ya vumbi kuelekea Mchikichini. Sasa pale hua kuna Jamaa anafanya mnada wake Kwenye kijukwaa kidogo hivi , ambacho kakizungushia kitambaa kwenye hilo jukwaa lake , kiasi kwamba hata bidhaa alizo kuwa nazo huwezi ata kuziona.

Sasa mimi na jamaa yangu tukaona ngoja tumsikilize huyo jamaa wa mnada hapo, maana alikuwa ananadi nguo kisha kuna baadhi ya muda anatangaza kutoa ofa ya begi buree kwa atakaye nunua baadhi ya Nguo zake.

Jamaa wa mnada alitoa Pensi na Flana kisha akasema , Ofa kwa atakaye nunua hizo atapata na Begi , na hakika yale mabegi baadhi yalikuwa mapya kabisaa , basi jamaa yangu akanyoosha mkono ,yule jamaa akamrushia hizo nguo bila hata kumpa begi, kisha anakuwa na mkusanyaji hela wake anakusanya hizo hela .

Mara ya pili tena yule muuza nguo akatoa tena Flana 2 kisha akasema bei ni 10000 na begi la bure, sisi tukachukua tena bila hata kupewa lile begi .

Kumbe pale Kwenye ule Mnada pale hua kuna watu wengine wanakuwepo pale ambao ni kikundi kimoja na hao wapiga mnada, na hao kazi yao kubwa ni kupokea Ofa ya begi kisha wanaenda Kwenye mabanda ya pembeni wnaakusanya kishawanayarudisha tena, na wana sheria zao ukigombania begi na wenzako basi wanalichukua wao kwa maana kuwa hamtakiwi kugombania.

Tumekuja kushtukia jamaa kashatoa 15000 na bila hata begi kupata . Kumbe pale wanawatapeli tuu watakaokuja kununua kwa kisingizio cha kusema ni Ofa ya begi, ila mabegi wakitoa Ofa wanawapa watu wao pale pale kisha wanarudisha Kwenye kile kijukwaa . Na kuna wengine wamewekwa ili kugombea hilo begi ili mteja asipate na wapokonywe wote.

Huo mchezo tumekuja kuushtukia baada ya Jamaa mmoja kuniambia kwamba huyo mwenzio hapo anaibiwa na wala hapati begi.Dohhh hapo jamaa alichoka sana mana kanjnua nguo na yeye shida apate hilo begi na wala hakupata .Na ndio mchezo wao kila siku Huo na Mpaka leo bado wapo pale.
Ni hapa
IMG_20220420_101550_4.jpg
 
Dodoma hiyo mjtqa ya majengo jamaa kategesha kasimu kqje njiani mjda ya saa mbili usiku,ile kupita tu akaipiga ikawa inawaka taa,fqster niaokota jamaa akatokeq eti njoo tuione kuna mtu kaidondosha,aliona vumbi mbwa yule,nikasepa na simu
🤣🤣🤣
 
Sitosahau Dogo aliniuzia Mayai mawili nikampa Elfu 10, Bwana Dogo akasema anaenda kuomba chenji akaniachia Kleti lake la Mayai..... Bwana yule hiyo chenji ndo ikawa chenji mazima, kuanzia Saa 7 hadi 11 Mtu hajarudi.... kwa kweli nikaamua kuyapiga tu yale Mayai aliyoyaacha na Washkaji maaana ilikua Gereji
 

Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom