Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Nimeenda kupima afya hasa ukimwi nikiwa na mke wangu. Hapa jijini Dsm. Nikiwa kwenye foleni watu wa4 kabla ya kumfikia daktari, kijasho chembamba kikaanza kunitoka, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi tofauti kabisa na nilivyozoea.Huku wife yeye akiwa na amani kabisa na bashasha tele.
Wife alinitangulia.Baadae dokta akasema tusubiri kidogo kama dakika 30 hivi ili afanye mambo yake. Kwakweli nilishindwa kuvumilia,nikamuaga wife kuwa nawahi kikao mahali.Nilimdanganya ili kurelease from tension aisee.Akanikubalia.Nikamwambia kuwa anichukulie majibu yangu na anipigie simu.
Nikiwa Kimara cha Mkaa nikinywa Lite baridi baa moja wanaita MTONGENI Bar, ghafla simu ikaita " Mama watoto Calling". Nikapiga pafu moja kisha nikapokea simu. Namshukuru Mungu majibu n mazuri baada ya kupiga picha na kunitumia WhatsApp. Kwa furaha niliyonayo, leo naangusha mbuzi home tule finyango za kutosha.
Ni kwann watu, hasa wanaume n maarufu sana wa kukimbia majibu ya afya? Nini huwa kinawasibu?