Ni ugonjwa au ni imani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ugonjwa au ni imani?

Discussion in 'JF Doctor' started by PSI Factor, Jun 17, 2011.

 1. PSI Factor

  PSI Factor Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Nina tatizo moja ambalo sijui kama binadamu wenzangu mnalo. Tatizo hili ni tangu nikiwa mtoto (miaka ya 70) na nimeendelea kuwa nalo.

  TATIZO:

  Nikikiangalia (au kusikiliza) kitu kwa muda mrefu huwa napata sura zaidi ya 4 ya kitu hicho. Sipendi hii hali na inaninyima raha sana.

  Mifano:

  Nikiiangalia picha moja naweza kukuonyesha hata vingine ambavyo wewe kama mwangaliaji hukuviona kwa haraka. Nikimwangalia mwadamu mwenzangu usoni wakati anaongea naweza kusahau kusikiliza nikaendelea kumwangalia kwa kama dakika 10 nikaweza kujua kama ni mwongo, mkweli, anafanya ushirikina n.k.

  Nimeoa, nikimwangalia sana mke wangu huwa najiuliza sana nini kilinisababishia nikaoana na mtu huyu, lakini nikiondoka kwenye concentration ya kuangalia basi namwona wa kawaida na anapendeza kweli.

  Hata kusikiliza hali ipo vilevile, nikisikiliza sauti ya mtu au mnyama napata hisia mbaya kiasi nafikia kusikia kama wanyama wanaongea, hii hunisaidia hasa nikikutana na mbwa au paka, nikikaa na mbwa hata kama ana kichaa huwa hanisumbui, wananikimbilia.

  Nakumbuka wakati JK anaanguka Jangwani nilikuwa namwangalia kwenye TV, aliposema "I see" nikamwambia jamaa yangu pembeni 'anaanguka' hata haikuchukua dakika akaanguka. Niliona kama ameanza kulegea, sikuwa namsikiliza nilikuwa namwangalia usoni.

  UTOTONI: Niliwahi kuiangalia picha nikaona kama inatoa machozi, picha hii ilikuwa ya Bikra Maria (mimi mkristo), lakini nilipomwambia marehemu mamangu yeye alisema ni hisia tu, akasema labda nilihadithiwa kuwa Maria analia. Tatizo ni kuwa niliiangalia sana picha ile kwakuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona sanamu kubwa kiasi kile. Sikuwa nimehadithiwa kama mama alivyofikiri.

  UKUBWANI: Niliwahi kuhudhuria semina moja ya kusoma body languages, hii haimaanishi kuwa ndiyo imeniletea tatizo hili, hata mwalimu aliyekuwa anatoa semina hii nilikuwa nikimwangalia sana niliona alikuwa hajiamini. Nilipomwambia kwa nje kuwa kuna vitu alitwambia lakini alionekana kutokuwa na uhakika navyo alikiri ni kweli.

  OMBI:
  Niliambiwa na rafiki yangu ninayefanya naye kazi ofisi moja kuwa nikiwauliza waungwana hapa kutakuwa na wataalam wanaoweza kunisaidia. Naomba msinichukulie kiutani mwenzenu, ni tatizo linaloninyima raha. Ningependa kujua ni tatizo? Chanzo ni nini? Nifanye nini? Kuna dawa ya kuzuia hali hii?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  kwa fikra zangu na mawazo yangu wewe katika Macho yako na akili yako Mwenyeezi Mungu kakupa kipaji na nguvu fulani ya asili ndio maana waweza kuhisi kitu na kikatokea watu wa namna hii ni wachache sana duniani. mimi pia nina tabia hiyo inafanana kama ya kwako lakini mimi

  huwa nikizungumza na mtu huwa namuangalia sana Usoni na nikaweza kumjuwa huyo mtu ni muongo au mkweli, mimi kwenye familia yangu nimezaliwa Mapacha yaani Tweens mwenzangu alikuwa ni Mwanamke mimi ni Mwanamme kwa lugha ya kizaramo tunasema hivi Kulwa na doto

  mimi ndio wa kwanza kutoka katika tumbo la mama yangu nikaitwa kulwa kwa jina la utani mwenzangu alichelewa dakika kutoka tumboni akaitwa doto. Na huyo mwenzangu alifariki Mwaka 1991 na kuhusu kifo chake niliwahi kumueleza mama huo mwaka kama kutatokea Kifo katika

  nyumba yetu mama yangu alishangaa sana na kuniogopa hicho ni kipaji toka kwa Mwenyeezi Mungu tu. Kwa hiyo inategemea wewe mwenzangu umezaliwa lini? na wewe ni wangapi katika familia yenu. wewe kwa mawazo yangu kama ungesomea kazi ya Uhakimu, Polisi, Utabiri,au kazi ya (psychology) saikolojia hizo kazi mojawapo ingelikufaa kwa hicho kipaji chako. huo sio Ugonjwa bali Nguvu fulani aliyekupa

  Mwenyeezi Mungu. Inapokutokea hivyo jaribu kujishughulisha na kazi yoyote ile ili mradi uwe busy kwa kitu fulani na usipende kila mtu kumueleza hayo sio maradhi jaribu kwenda kwa mchungaji akuombee kwa Mungu yatapunguwa au nenda kanisani kaombe Dua zako kwa Mungu matatizo yatakwisha huo ndio ushauri wangu.
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  mhhh huwa napenda sana kungalia hollywood series especially lie to me .. mhh jamaa ni lie detector so kumbe hivi vitu vipo..?
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Jibashirie Mkuu
   
 5. upele

  upele JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka kusema unataka kuwa kama sherh yy haya bwana hii bongo inia kichwa kichwa watu wakutoakafara
  ukiwa na shida hizo hisia zako zitatoka
  conquest-god knows than uuuuu
   
 6. p

  plawala JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama nimekupata vizuri nadhani una tatizo la udhaifu wa jinsi ubongo unavyotafsiri mwonekano wa vitu,distortion in sensory perception yaani illusion
   
 7. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,010
  Likes Received: 3,194
  Trophy Points: 280
  Ungekua mzungu, ungekua mbali sana.

  Wakina Newton, Galileo,nk walikua na maono kama yako, afu wakayafanyia kazi.
   
 8. k

  kisukari JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  labda wewe ni psychic.una uwezo wa kuona vitu ambavyo mtu wa kawaida hawezi kuona.kwa uonaji wako,ukimwangalia mtu au ukiona picha ya mtu au ukiangalia sehemu kwa makini unaona vitu ambavyo mtu wa kawaida hawezi kuona.ila sina uhakika/wengine huwaona mpaka watu waliokwisha kufa
   
 9. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Dellusions of grandeur plus visual hallucinations
   
 10. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,998
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  mkuu we ni moja ya watu wengi sana ambao wan super power..hii huwa wanazaliwa nayo...tatizo hapa tanzania ukimweleza mtu kuhusu wewe anabaki kukushangaa...ndo maana wengi hujificha na anyoona au kusikia inakua siri yake..mm nina jamaa tulisoma nae chuo alikua kama ww ila yeye alikua anaona visivyoonekana including wachawi...
   
 11. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  natural super power :A S 114:.. hakuna kitu kama hicho...!!! wewe haha, kuona visivyoonekana either you are psychic :der: or wewe ni mchawi pia .. ! mkuu usinambia unawaamini wale wanaocheza mazingaobwe, au unadhani mtu kama super he really do exist!
   
 12. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Mkuu huo si ugonjwa.Nakumbuka miaka 17 iliyopita niliwahi kuelezwa na classmate juu ya HALI HIYO,NA NILIPOJARIBU KUTAZAMA SEHEMU 1 NILIONA MAMBO MENGI.Kifupi ni suala hili limegawanyika makundi 2,la kwanza yaweza kuwa ni IMANI. Kuna IMANI inayoitwa MEDITATION & CONSTRATION FAITH. Ambao ibada yao huwa ni kutazama au kufikiria kitu kimoja hadi pale unaposikia/kuona vitu zaidi ya vile halisi unavyo sikia/kuona. IEPUKE ITAKUTESA!Na Upande wa pili huwa ni hali ya ama kuzaliwa nayo au inayohusiana na mambo ya NGUVU ZA GIZA. nitarudi kwa UFAFANUZI.ILA EPUKA KUTAZAMA/KUFIKIRI NA KUSIKILIZA KITU KIMOJA KWA MUDA MREFU
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,058
  Likes Received: 6,505
  Trophy Points: 280
  Lazima uzeeni utakuwa mganga wa kienyeji.
   
 14. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hivi vitu vipo ni nguvu za asili watu wengi wanavyo ila hawajitambui na wala watu wa karibu yao hawawezi kuwaamini sidhani kama ni tatizo la kidaktari, niliwahi kukaa na mtu kwenye daladala anaongea na simu anajibushana lakini hiyo simu haionekani wala haijaonekana ikiita alivyomaliza akarudisha kitu mfukoni.vp ulishaenda kwa madaktari na wakasemaje,
   
 15. m

  mhondo JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Inawezekana ikawa ni nguvu kutoka kwa Mungu au kutoka kwa shetani. Kama ni nguvu ya Mungu unaweza kuwa kama T.Joshua wa Emmanuel TV na kama ni ya shetani unaweza kuwa Mganga wa kienyeji au mnajimu ni vizuri ukaeleze shida yako kwa wachungaji wanaofanya huduma za maombezi ili iweze kujulikana ni nguvu ipi kati ya hizo mbili inatenda kazi ndani yako. Kwangu mimi naona ni suala la kiimani ila wanasayansi au watu wa saikolojia wanaweza kukuambia kuwa ni ugonjwa.
   
Loading...