barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,404
- 29,811
Za kazi. Kwa wale wenye uzoefu na walio katika ndoa tayari. Naombeni mnijuze endapo mwanaume yupo kwenye uhusiano na msichana na wao wawili wamekubaliana kuja kuishi pamoja kama mke na mume, ni taratibu gani mwanaume anatakiwa kuzifuata. Yaani kila kitu cha kufanya kama kuchagua mshenga na mengineyo je kuna taratibu za kuchagua mshenga au je ni lazima kutuma mshenga na taratibu za kutoa mahali zinakuaje? Na baada ya hapo nini ufuata? Rafiki yangu kaniuliza, ana mpango wa kuoa msichana wa kiha ndani ya miezi kama 15 hivi mimi mgeni bado sijaoa, kwa sasa wanaishi pamoja kama wapenzi.