Ni soni kuu Rais kwenda Kagera kwa mbwembwe muda huu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,065
2,000
Ni soni kuu. Ni soni kwa wote waliohusika na wanaohusika kufanikisha ziara ya Rais Magufuli mkoani Kagera. Haileti ladha,muda huu,Rais kutua Kagera kwa mbwembwe.

Lilipotokea tetemeko kule Kagera,wanaKagera walichangiwa. Kubwa zaidi,waathirika wa tetemeko walihitaji faraja. Faraja juu ya misiba iliyowakuta na mateso yaliyowakabili.

WanaKagera,kwa sauti na vitendo,vyao na vya wengine,walimhitaji Rais Magufuli. Walimhitaji kiongozi wao mkuu wa nchi akawaone na kuwafariji. Wakamsubiri bila kiburi na kwa hamu muhimu. Rais hakwenda. WanaKagera wakashangaa na kusinyaa.

Hainogi kuona au kusikia kuwa Rais anakwenda Kagera muda huu na kupanga kuhutubia kwa mbwembwe. Kisiasa,Rais hata-gain chochote!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom