Ni simu ipi kali kati ya hizi tatu na kwa sababu zipi?

performance
Performance wise sidhani Kama Kuna simu ya low end inayoipita A10 Samsung. Na sababu kubwa ni uwepo wa core mbili za Cortex A73, kwa daily activities itaperform vizuri zaidi kushinda hio Tecno na Infinix.

According to Gsmarena hio Tecno Ina Cortex A7 ambayo itakuwa slow Sana, 2019 kununua simu ya cortex A7 ni kujitia Kitanzi.

Hot s4 processor yake ni ok, Haina nguvu Kama A10 ila itafanya task nyingi bila matatizo.

4G LTE
Tecno Ina band 3(1800), 7(2600), 20(800)

Infix band zake 1(2100), 3(1800), 5(850), 8(900), 38(2600), 40(2300), 41(2500)

A10 band zake 1(2100), 2(1900), 3(1800), 5(850), 7(2600), 8(900), 20(800), 38(2600), 40(2300), 41(2500)

ukiangalia Hapo A10 Ina bands nyingi zaidi za 4G, na kwa Tanzania tunatumia 800, 1800 na 2300, ni A10 peke yake ndio inazo zote,

Tecno haina 2300 utamiss TTCL speed kubwa, ila utapata TTCL ya kawaida ya 1800

Infinix Haina 800 utamiss coverage kubwa ya 4G ya Tigo ila utapata 4G ya Tigo ya 1800 mijini.

ukaaji chaji
Hio tecno itakaa na chaji zaidi sababu ya uwepo wa cortex A7 na battery kubwa la 5000mah, Infinix na hio Samsung ni karibia zinalingana.

display
Zote ni Vimeo kwenye display Zina mavioo makubwa Sana around inch 6 wakati resolution ni Ndogo ya HD.

camera
Pia hapa hakuna Cha kuandika, ukiona simu Zina megapixel nyingiii kwa Bei Ndogo ujue hakuna kitu wanataka tu kudanganya watu wasiofahamu wanunue. Tegemea kuwekea beauty mode by default na blured pictures.

Kama ni Mimi nafanya hio decision ningenunua A10 Samsung na Bei ni around 250,000 mpaka 300,000 zaidi ya Hapo Kuna option nzuri zaidi.
 
Hzo band unaangalia wap kwenye cm au ukisoma Gsm arena specification basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ