Ni sheria ipi inaipa exemption TBC?

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Wanabodi ni hivi karibuni TCRA ilitangaza kusudio la kufuta leseni kwa baadhi ya makampuni ya Ving'amuzi kama yataendelea kuonyesha TV ambazo ni free on air, Kwa kuitikia mwito huo makampuni kama DSTV, Azam na wengineo walilazimika kuondoa TV channels za ndani. sisi tulio na decoder za DSTV tu hatuoni channel za ndani. Hii si tu imenikosesha haki yangu ya kikatiba inayonipa haki ya kupata habari lakini pia inakiuka msingi wa sheria unaosema kila mtu yuko sawa mbele ya sheria. Nasema hivi kwa kuwa pamoja na maagizo hayo TBC haikuondolewa kama TV zingine! je TBC ipo above the law? Je TCRA wanaweza kutueleza wametumia kifungu gani cha sheria kuziondoa TV channel binafsi na kuibakisha ya serikali? je huu si upendeleo mbele ya sheria?

Kwa tafsiri yangu kuna mkakati wa kijinga wa kutaka nchi iendelee kupata habari za upande mmoja za kusifu na kujipendekeza. Tunaomba wanasheria na TCRA wanaoingia humu JF watueleze ni kifungu kipi wametumia ili wasionekane wako biased.
 
sambamba na hilo leo ndio tarehe 5, bado sioni channels nyingine za ndani au muda bado??!?! kwa dstv
 
Back
Top Bottom