Ni sawa Marekani kuwasaka Boko haramu Leader's? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sawa Marekani kuwasaka Boko haramu Leader's?

Discussion in 'International Forum' started by mshikachuma, Jun 24, 2012.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Jamani siku mbili zilizopita Serikali ya Marekani imetangaza kuwa imewaweka viongozi 3 wa kikundi cha Boko haramu
  cha Nigeria kwenye list ya most wanted people in the world...watawasaka kwa udi na uvumba mpaka wawashike no
  matter wakiwa hai au wamekufa lakini wanawahitaji tu. - Sasa maswali yangu ni

  1.Kwanini ni Boko haramu tu? mbona hawakutangaza hivi kwa Al-shabaab ya somalia while wote ni magaidi?
  2.Je ikatokea wamefanikisha kuwakamata na kuwauwa au kuwafunga maisha, Je Nigeria itakalika salama? au
  ndiyo itakuwa mwanzo wa vifo vingine kutoka kwa Boko haramu?.
  3.Je ni kweli Boko haramu ni watetezi wa dini ya kiislamu huko Nigeria au ni kikundi cha wahuni tu?

  Kwa wale wataalamu wa mambo ya kidiplomasia naombeni mnijuze Saga hili kwa faida yangu na wanaJF wengine.

  Shukrani....na nawasilisha
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Marekani wamechelewa sana kuchukua hatua hii wasakwe haraka sana hata ikibidi wakiuawa sawa tu! watu wanaua watu wasio na hatia wakkristo wakiwa makanisani! Al-shabab nao wanashugulikiwa, A-qaeda wanafuatiliwa! kwamba nigeria haitakalika? kwani kuwaacha ndio inakalika?? Vunja uti wa mgongo wa Boko Haramu!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Unauliza kama ni Boko Haram peke yake? Mbona muda mrefu Marekani imekuwa inawasaka Al Shabab kule Somalia kwa kutumia drones? Unakumbuka yule Mkomoro aliyekuwa Al Qaida aliyetafutwa kwa muda mrefu? Mbona alitunguliwa na kamzinga ka drone huko Somalia? Hawa magaidi kila wanakochipuka ni kuwatungua tu kwa sababu wakiachiwa washamiri wanatoa fursa kwa Al Qaida kujiimarisha.
   
 4. E

  Eberhard JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Watunguliwe tu ni wauaji hawa. Wafutiliwe mbali. Al- shababu, Al- Qaida, Al- Boko haramu ( Na kwa nini majini yao yanaanzia na Al Al tu?) Wanachafua dini ya kiislamu hawa. Wafatwe kote hata kama wamejificha misikitini. Nina imani Obama ataweza kazi hii. Mzigo mzito mpe mjaruo.
   
 5. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma mkuu!...Je kwa mtizamo wako unaona Boko haramu ni watetezi wa Uislam au ni kikundi cha wauni tu?
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye bold....sijawahi sikia hawa watu wanajificha misikitini ila mara nyingi nasikia hawa watu wanaishi porini na
  milimani
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wahuni watatangazaje vita ya JIHAD? Kwani Jihad ni ya wahuni au ya....?
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu, sijakusoma kabisa
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Ni Kikundi cha wahuni wanaotumia mwavuli wa dini najua uislamu siku zote unahubiri amani upendo na kuvumiliana sina utalaam sana na maandiko ya kiislamu ila nina uhakika hakuna uislamu unposema uchome makanisa, uue wakkristo na kuhamasisha vitendo vya kihalifu hao ni wahuni na magaidi ila wamevaa ngozi ya dini!!
   
 10. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  who is boko haram ????? jibu Boko Haram Is PDP & PDP Is Boko Haram- Gen Azazi - Politics - Nairaland

  ona hii video http://www.youtube.com/watch?feature=endscreen&v=z7yMRbYFUZE&NR=1

  ona hii interview Louis Farrakhan interview with Mike Wallace(1996).3gp - YouTube

   
 11. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Jibu la hilo swali linategemea uko upande gani. Kwa asiye muislam, ni wazi kabisa kwa akili ya kawaida kuwa kufanya ugaidi kwa kisingizio cha kuisafisha dini yao na ukafiri ni upuuzi na hakiupi uislam heshima mbele ya ulimwengu.

  Lakini ukiwa muislam ni stori nyingine. Kuna baadhi wanaona Boko Haram, au al qaeda, au taleban, ni wakombozi, mashujaa, watu wenye ujasiri wa kusimama dhidi ya ukafiri wa kikristo na kimagharibi. Ukipita pita kwenye mitaa ya hata hapa kwetu yenye waislam wengi, mfano Zanzibar, ni kawaida kuona vijana wakiwa wamevaa t-shirt zenye picha ya Osama bin Laden kama ishara ya kumuenzi. Gaidi anaenziwa.

  Kwa hiyo usiwasemee waislam au dini ya kiislam. Waislam walio wengi ni watu wa kawaida, kama sisi, kama wewe, wanawaza mkate wao wa siku kama watu wengine, wanawaza kusomesha watoto wao kama watu wengine. Lakini baadhi yao si watu wa kawaida, hawa wanawaza siku uislam utakapokuwa majority ulimwenguni, siku sharia itakapotawala, na hawa wapo tayari kufanya lolote ikiwemo kulipua vijana wao ili kutekeleza maluweluwe yao vichwani.
   
 12. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Minister Farrakhan Knows Who Killed JFK - YouTube
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,836
  Trophy Points: 280
  Boko haram sio watetezi wa waislam,bali ni majambazi na magaidi kama walivyo uamsho na sasa ni bora watafutwe na wapigwe risasi na washukuru marekani kwani wao hawasubiri mabomu yawalipukie watu bali mabomu yao huwalipukia magaidi.

  Kwakweli vitendo vinavyo fanya na haya makundi ni kutaka kuitawala dunia kwa kisingizio cha uislam.

  Siku si nyingi kikundi cha kigaidi cha uamsho kitatangazwa kuwa kikundi hatari na maghala ya silaha yatafunguliwa kukiangamiza.

  Nashangaa hii serikali yetu ina subiri nini kukiangamiza hichi kikundi kabla hakijasambaa.
   
 14. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  watafutwe na washikwe, acha marekan iwasake,kipi kikusistishacho
   
 15. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sijasikitika mkuu, ila nimeuliza ili nijue haya mambo....maani ni very complecated
   
 16. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,611
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu zaidi kuliko yote ni kuwa muuaji yeyote yule ni lazima asakwe na aangamizwe, iwe anafanya mauaji hayo huku ameshika biblia, msahafu, tasbihi au rozari, huyu ni mhalifu na hana nafasi katika ulimwengu wa kistaarabu. Hawa wasakwe na wamalizwe hata kama watatumia majina ya namna gani. Kama ni Al Shabab, Uamsho, Boko Haram, Talebani, Al Qaeda, Lords Resistance Army au Tamir Taigars, hiyo haijalishi, cha muhimu ni je, wanafanya nini? Kama wanafanya maovu malipo yao ni dhahiri, ni lazima waadhibiwe bila huruma. Tena katika hilo hakuna kuwa na haja ya kuwa na woga wa kuwa watalipiza kisasi. jamii ya Ulimwengu wa Kistaarabu haiwezi kupoteza muda wa kutofanya tendo la kuwadhibi kwa hofu ya kushambuliwa na watu hawa. Wanaweza kuvizia na kuwaua wachache wetu lakini mwisho wa yote ulimwengu wa Ustaarabu utashinda.
   
Loading...