Ni sawa kwa Mama Tunu Pinda?

Status
Not open for further replies.
Kuna watu wana Roho Mbaya humu ndani!!!
(Hatari)
 

ukweli in ur heart,she deserve this?
 
hiyo sio habari ulitaka atumie taxi, mamabo mengine jamani hayana mashiko. tujadilini mambo yenye tija kwa taifa sio hilo la kufika hapo na gari laserikali mulitaka atembelee gari gani sasa.
 
ningependa kujua mama tunu ana kazi?? i mean kaajiriwa mahali? au ni mama wa nyumbani?

Huyu Mama CV yake huwa haieleweki sana, ila ukitafuta Threads za Februari 2008 wakati Pinda anapewa u-PM utakuta threads zenye tetesi za huyo mama alitokea wapi. JF kuna kila kitu.

Pamoja na hayo, kuna ka-utaratibu fulani kwamba wake za Rais, Makamu na Waziri Mkuu, once waume zao wakishakwaa hizo nafasi huwa hawatakiwi kuendelea na ajira zao. I guess utaratibu huu ulianza zama za Nyerere na mwajiri mkuu zama hizo alikuwa ni serikali, so kama Mrs PM alikuwa mfanyakazi wa serikalini then ingekuwa ngumu huko kazini kwake kupokea command kutoka kwa boss wake (assuming kwamba alikuwa ni junior staff).

Utaratibu huu ulikataliwa na mke wa Mzee Warioba, kwa hoja kwamba PM ni Presidential appointment, what if hiyo appointment ikidumu kwa mwaka mmoja, does it mean kwamba Mama Warioba aanze tena kusaka kazi kwa kuwa mumewe sio PM tena? Ni hoja ambayo ilikuwa na mantiki na mama aliendelea kufanya kazi, japo kwenye corridors watu walikuwa wanamuona kwamba ni mkorofi.

Kwa hiyo Mrs. Tunu Pinda hata kama alikuwa ameajiriwa mahali, inawezekana kabisa anaweza kuwa aliachia kibarua huko alikokuwa akifanya kwa kuzingatia hako ka-utaratibu ambako sina hakika kama kapo kisheria.
 
Reactions: EMT
 
hiyo sio habari ulitaka atumie taxi, mamabo mengine jamani hayana mashiko. tujadilini mambo yenye tija kwa taifa sio hilo la kufika hapo na gari laserikali mulitaka atembelee gari gani sasa.

Watanganyika inatakiwa muelemike sana, Hakuna kitu kidogo hapa hii ni mali ya umma lazima zisimamiwe, Unapolalamika sukari bei juu una maana gani? Uwezi kuesabu una unashilingi kama hakuna senti tano na vilevile walisema ndo ndo ndo si chururu. Kweli Watanganyika tunaitaji elimu ya juu sana.
 
hiyo sio habari ulitaka atumie taxi, mamabo mengine jamani hayana mashiko. tujadilini mambo yenye tija kwa taifa sio hilo la kufika hapo na gari laserikali mulitaka atembelee gari gani sasa.

Jitahdi kuelewa mada we b.we.ge, hatujakataa Mrs Pinda kuja na gari la serikali, binafsi ningehuzunika sana kama angekuja kwa taxi. Issue ni kuja na gari yenye National emblem au nembo ya taifa ambayo ni ya hadhi ya waziri mkuu. Umeelewa we juu kwa juu a.k.a waru waru/kilaza
 
ukweli in ur heart,she deserve this?

For sure she doen't deserve Neema. Viongoz wamepoteza maadili, ndo ivo ivo wanavyowapa watoto wao kazi ambazo hawadiserve, gabbege+++
 

umenikumbusha kenya bwana...wale jamaa wanaelekea pabaya...campain makanisani kitu cha kawaida....ni nchi ya ajabu kila kabila lina kituo chake cha redio...full kutetana humo
 
jamani eeeeeeeeeeh! ni saw kabisa kwa mke wa waziri mkuu kutumia lil gari la serikali kumbuka yeye
zaidi ya waziri nikiwa na maana ushauri,matunzo na kila kitu kwa jili ya ustawi wa afya yetu
ni yeye,ivyo kama anaenda mahali kwa jili ya kumwakilisha mumewe ni saw.
jamani mana JF sio kila kitu mnaweka QN MARK!
SAWA?.ANGALAU NA SISI TUONE WAAVYOTUMIA BILA KUJA PALE MSIBANI MNGEJUAJE YANAVYOTUMILA MPAKA K-PARTY?
YUPO RIGHT!KABISA.PALE ANAWALILISHA UBAVU!!
 
ningependa kujua mama tunu ana kazi?? i mean kaajiriwa mahali? au ni mama wa nyumbani?

Huyu mama na PM ni system aka nyoka aka TISS kipindi kirefu.

Tanzania tuna regulations za wapi magari haya yanaweza kutumiwa na wapi hayawezi? Kwa kazi za kishushushu kujichanganya na wananchi inatakiwa, hata kwa nembo, hata kwenye msiba, hata kwa mke wa Waziri Mkuu.

Asingetokea napo tungesema "Msiba wa Kanumba hakuna hata gari la serikali" labda wakaona kwa kuwa wakuu wako busy, mamaa anaweza kuwakilisha.

Kuongelea matumizi ya magari ya serikali kabla hujaongelea mambo ya msingi kwa nchi kama Tanzania ni overkill.

Alternative mtataka mama aendeshe ki Datsun cha mtoto wa mkulima, kikwame kwenye mashimo ya uswazi, muanze kulaumu "kwa nini hajachukua gari ya hakika ya serikali?"

Hapo mlikuwa mnaonyeshwa tu kwamba "uongozi wa juu wa serikali uko hapa".
 
Wakuu, nyie mlitaka aende na usafiri gani? Mlitaka aendeshe saloon yake binafsi ilihali ni mke wa waziri mkuu? Kwani yeye na Kanumba wana undugu gani? Hapo amekuja kwa label ya waziri mkuu na vyombo vya habari vitaandika kwamba mke wa waziri mkuu alikuwepo haviwezi kusema Tunu alikuwepo. Jamani haya ni madogo sana kuyafuatilia. Tuangalie yaliyo makubwa.
 
Kwa mfano waziri mkuu angekuwa mwanamke harafu mume wake aende na gari lake msibani namna hiyo ingekuwaje?. Just curious..
 
magari ya Serikali twayaona sana usiku kwenye magesti ya huku Sinza.

Na hawakomi coz kila kukicha yanapigwa power window na vikolokolo vengine vya kuuzika maeneo ya Kariakoo Gerezani...
 
Acheni hz ni kawaida mbona?mwisho mtasema asilalie kitanda cha waziri mkuu,mbona hata choo na shuka wanatumia moja? Tatizo nembo au gari? Kuweni great thinkers jamani
 
ila kwenye hizo picha nimeona wananchi wengi sana hapo! hivi hao wananchi sio serikali??

whatever we can say, sioni ubaya wowote ule......maana magari haya wanayatumia mpaka kwenye shughuli za ajabu, wanaendea mashambani kwao weekend n.k

kwa kifupi kama tumeishashindwa huko nyuma hatuwezi leo...labda kesho

imetoka hiyo
 
Reactions: Mbu
......acheni uvivu wa kufikiri....

huyu mama hana uwezo wa kuamrisha gari ya kwendea msibani,
waulizeni watu wa Protocol na wasemaji wa ofisi ya Waziri mkuu
kwanini 'itifaki' imemruhusu kutumia gari hiyo.

Kila siku mnayaona magari ya STK nk yakisubiri watoto shule mwajionea sawa tu..
Accountability mtihani ee?
 
Watu wengine bongolala sana yaani wameshabadilisha muktadha wa thread hii ili ioneka mtoa mada eti amepinga Mama pinda kwenda kwenda na gari ya serikali au gari ya hadhi yake msibani, thread iko wazi kabisa kuwa kwanini atumue gari lenye nembo ya serikali ambayo hutumiwa na viongozi wakuu wa nchi? Yeye si kiongozi wa nchi! Mbona mna fikra makengeza!!?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…