Ni sawa kununua gari ya TZS 15 Million huku ukiwa unaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule?

Jua kitu kimoja tu silazima mtu kujenga kila mahala anapofanyia maisha yake .naweza kywa na nyumba kibaha nikaipangisha na mm nikaenda kupanga masaki so it is like swaping houses.
Au nina nyumba bagamoyo maisha yangu(kazi)Dar napangisha nyumba ya bmoyo napanga Dar na usafiri wangu
 
Sioni tatizo lolote lile.

Kama mtu kanunua hilo gari kwa pesa zake na kama kapanga chumba au nyumba kwa pesa zake....tatizo liko wapi?
Wahindi wanakaa kwy nyumba za NHC lakini wanasukuma mpaka magari ya Million 250. Na wana maisha mazuri kuliko wewe mwenye iyo million 15 unakimbilia kujenga. Tumia Pesa kuwekeza katika madili ya Pesa na hata kama iyo nyumba unaijenga sehemu ya bihashara apo vizuri sana
 
Nina ongezea hapo mkuuu huyu Jamaa nimuulize kitu hivi unajua utu wa mtu ulivyo na thamani? Hivi unajua ule msemo kuwa kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza? Unakuwa na marafiki 100 Kati ya hao mia mia wote watajua una gari ila watakaojua una nyumba ni labda kumi tu, Mimi nataka niheshimike ili nipate marafiki kiurahis niweze kufanikiwa mambo yangu yawe yanaenda vizuri sasa nikiwa na gari watu watajua faster Lakini nyumba lazima nitangaze maana unakuwa na nyumba hata marafiki zako wengne wa mtaa huo huo hawajawahi kuiona, pia Rafiki yangu Akiwa na gari nitamheshimu maana atanipa lift Siku nyingne naweza kumuomba nikaendea mahali au nikiwa na sherehe itatumika sasa hilo la kukimbilia nyumba siwezi kuazima nyumba yako na haiwezi kunisaidia hata kidogo

Gari kitu kingne bhana maana hata ukikutana na demu au Rafiki yako mliopoteana Siku nyingi atakuuluza vipi ile gari yako ipo? Mbona hawaulizi nyumba?
 

Mimi ndugu yangu anamiliki gari ya mil 240 . Anakaa nyumba ya kupanga. Kodi $2,500. Lakini ana apartment zake

Sikuhizi gari ni basic need ya kukuingizia pesa, ikiwa tu unafanyabiashara ya inayohitaji utembelee sehemu nyingi au unaumuhimu kuwahi kazini na public transport sio rafiki kuwahi.

Mfano mimi nahitaji gari, sababu natembelea wateja karibu 10-15 kwa siku, nafanya kazi nikiwa kwenye gari zaidi ya ofisini. Kwahiyo hata nisipojenga sahizi ni sawa, maana najikusanya na gari ni kama mtaji wangu pia

Shida inakuja unapoamua kumiliki ili kujifanya au kushindana,
Usiigekuny.... Kwa tembo
 

Nimependa mistali yako mkuu
Ni mwendo wa usafi tu mwisho utakuwa raisi wa wasafi
Hahaha
Ila kiukweli anayeogopa kununia gari kisa hana nyumba au gharama za uendeshaji gari Huyo muhoga wa maisha na hajui kutafuta pesa
 

Ur very genius mkuu
Umetumia mfano hai kabisa wa mhindi asipokuelewa hapo basi tena
 
Nimependa mistali yako mkuu
Ni wa usafi tu mwisho utakuwa rahisi wa wasafi

Ila kiukweli anayeogopa kununia gari Lisa hana nyumba au gharama za uendeshaji gari Huyo muhoga wa maisha na hajui kutafuta pesa
Mkuuu hata nyumba ina garama kila Siku itabidi ufagie nje, ufyeke, ulipe umeme, ulipe maji, ulipe kodi Ya majengo, ulipe kodi Ya Ardhi uifanyie ukarabati
 
Kama ulivyosema kwanza inategemea na eneo lenyewe,kwa Dar kujenga ni gharama kuliko kununua gari ila mikoa mingine iliyobaki kujenga ni gharama ndogo kuliko kununua gari
Miji yote kujenga ni gharama kuliko kununua gari
 
Malazi, kula na kulala ili la kulala kwenye nyumba mwenyewe ni la kwako umeongezea
 
Bora ukaishi nje ya mji ila kwako kuliko uishi mjini ambapo 90% ni uswazi kubayaaa sababu wanaoweza kupanga kwenye apartments si wengi, wote mnaishia manzese, tandika, kwakina Chibu halafu mnajisifu mnakaa mjini huku kipaso, sienta and the likes unakipaki CCM
 
Hata gari yawezakua luability
Hata nyumba yawezakua liability
Kama nyumba yako uliyojenga yaweza kua liability vip kuhusu nyumba ya kupanga?
 
We jifariji tu yani aweze kununua gari ya 40m halafu ukadhani hana ujenzi sehemu unaendelea
 
Kuna Muhindi rafik angu ana gorofa mbili kariakoo ,ana gari tatu amepanga gorofa la NHC Pale karibu na kisutu secondary school.Mtanzania anaona kuwa na nyumba ndio kila kitu! Kuna watu wamejenga huko kimara,siju mbezi etc kwa siku mpaka afike posta mpya kazi kwake anaspendi 4500 au 10,000 kwenda na kurudi kwake! Kwa Mwezi mmoja anatumia kiasi kikubwa sana,bora angepanga Sinza akawa anawai mjini na akaokoa garama na muda,tunakufa mapema kwa kuamka saa 11 alfajiri kuwai saa mbili kazini.kirudi nyumbani ni masaa matatu njiani Dar hii hii....kulala late,jumamos na jumapili bize na vikao vya harusi....umejenga jumba kubwa,watoto wakianza secondary na chuo .nyumbani unabki na dada wa kazi na wife....mmoja wenu akiamia dodoma,jumba la 200 millions lipo tu alikusaidii kitu....maisha ni nini???
 
Ni rahisi sana kuwa na gari kuliko Nyumba, muheshimu sana mwenye nyumba narudia nyumba sio kibanda, yani mi hapa nilipofikia japo mdogo mdogo ningekuwa na kichaa cha magari ningekuwa nahesabu mac x tatu na ist moja
 
Unaposema ulimbukeni inamaana kwako wewe unaona kumiliki gari ni anasa? Hivi watu wengine huwa mnawachukuliaje watu wanaomiliki gari probably mnawaona Kama ni vibopa flani Hivi.
Mleta Mada elewa kuwa gari ni chombo cha usafiri tu na sio kwamba Mtu akiwa na gari basi ameamua kujionyesha au kuringa. Huwezi jenga nyumba kwa 10 OR 15 millions.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…